Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, January 3, 2019

Ridhiwani Kikwete Amvaa Kingwangallah kwa Kushindwa Kutangaza Utalii

Mbunge wa Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete amesema bado Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala hajafanya kazi yake vilivyo katika kutangaza vivutio vya utalii nchini.

Ridhiwani ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 3, 2019 katika uzinduzi wa redio ya kutangaza utalii ya 'Hakuna Matata'.

Amesema hivi karibuni alimuona Dk Kigwangalla akipiga picha katika moja ya mbuga za wanyama kama moja ya njia ya kuhamasisha kutembelea vivutio vya utalii.

"Nilipoiona picha ile, nilimkosoa kwa kweli na kumwambia bado hajaweka nguvu kubwa kwenye ushawishi, ingekuwa vizuri kama angetumia wasanii  ambao wana watu wengi wanaowafuatilia kwenye mitandao ya kijamii," amesema Mbunge huyo

Kuhusu ujio wa redio hiyo, Ridhiwani amesema ni jambo zuri ukizingatia kuwa ni ya mtandaoni ambako dunia imehamia huko.

Awali akieleza lengo la kufungua , Mkurugenzi wa redio hiyo, Beatrice Ndungu, amesema  moja ya sababu ni kutangaza utalii na pia kuzalisha ajira kwa vijana.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wasanii mbalimbali akiwemo Miss Tanzania, Elizabeth Makune, Mzee Chilo na  Monalisa,.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...