Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 7, 2019

Lugola Awataka Nida Wapitie Upya Usajili, Utoaji Wa Vitambulisho Vya Taifa Mikoa Ya Kagera Na Kigoma

adv1
Na Felix Mwagara, MOHA-Kyerwa.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) apitie upya usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa katika mikoa ya Kagera na Kigoma ili aweze kuwabaini  na kuwaondoa raia wa nchi jirani zinazoizunguka mikoa hiyo.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Kyerwa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa sokoni mjini humo, leo, Lugola alisema baadhi ya raia wa nchi jirani wamejipenyeza na kujipatia vitambulisho vya taifa ama kwa kuwatumkia wenyeji ama nguvu ya fedha.

“Hii haikubaliki na lazima tuwe makini katika hilo, nimepata taarifa kuhusu watu waliojipatia vitambulisho hivyo ambao hawastahili, kutokana na hilo natoa agizo kuwa, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ahakikishe anapitia upya zoezi la kusajili ili aweze kuwabaini ambao walijipatia kwa njia ambazo sio halali,” alisema Lugola.

Lugola alisema kuwa, utoaji wa vitambulisho hivyo katika mikoa hiyo unasuasua kwasababu ya umakini unaofanyika katika kusajili waombaji wa vitambulisho.

“Hakuna Mtanzania atakayekosa vitambyulisho vya taifa, kilka mtu anatapa ili mradi tu awe na sifa, na pia mpaka upate lazima upitie mchujo maalumu ili tuhakikishe wewe tunakupa kitambulisho ni Mtanzania halisi au sio.” Alisema Lugola.

 Aidha, Lugola pia juzi alimuagiza alimpa wiki mbili  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI) Dkt Anna Makakara, awe amefika katika mikoa hiyo kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa Wahamiaji haramu katika Mikoa hiyo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

Lugola aliyazungumza hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Karagwe akisisitiza kuwa katika mikoa hiyo kuna idadi kubwa ya wahamiaji haramu .

Lugola aliongeza kuwa, licha ya kutangaza operesheni hiyo, lakini viongozi wa uhamiaji katika mikoa hiyo wawe makini mara kwa mara kuhakikisha wanawafuatilia wahamiaji hao kwa kuwashirikisha wananchi waaminifu ili waweze kutoa taarfia sahihi za wahamiaji hao.

Waziri huyo pia aliwataka wananchi wa mikoa hiyo watoe ushirikiano na wasiwafiche wahamiaji hao kwasababu kumuhifadhi ni kosa kisheria, hivyo wanapaswa kuhakikisjha wanatoa taarifa za wahamiaji hao kwa maafisa uhamiaji ili waweze kukamatwa.

Lugola alisema alifanya ziara katika Mkoa wa Kigoma kwa kutembelea Wilaya zote kama anavyofanya Mkoa wa Kagera, anapewa kero hiyo katika ziara hiyo, hivyo anataka Uhamiaji wawaondoa wahamiaji wote ndani ya mikoa hiyo ili Watanzania waweze kuishi kwa amani wakiendelea kujionea maendeleo ya uongozi wa Rais Dkt. Magufuli.

Waziri Lugola amemaliza ziara yake Wilaya Kyerwa na Wilaya inafuata ni Ngara, Biharamulo na Muleba, ambapo akiwa katika ziara hiyo, pia uzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara pia ukutana na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni ambayo jukumu lake kuu ni kupunguza msongamano gerezani na kusimamia wafungwa waliopewa adhabu mbadala na Mahakama au wafungwa waliopata msamaha kupitia sheria ya huduma kwa jamii na kutumikia kifungo chao nje ya Gereza.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )