Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 28, 2019

Majungu, fitina na chuki Vyamkera RC Paul Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaa, Paul Makonda amesema kuwa moja ya vitu vinavyomkera katika Mkoa wa Dar es salaam ni namna ambavyo watu wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi kuwasema wenzao huku wao wakiwa hawafanyi kazi.

Paul Makonda ametoa kauli hiyo Jijin Dar es salaam katika hafla aliyoalikwa na Msemaji wa Klabu ya Soka ya Simba Haji Manara iliyofanyika wa kuamkia usiku wa leo ambapo viongozi mbalimbali walishiriki.

"Afrika kwa miaka mingi ina laana ya umasikini na imepokelewa kwa muda mrefu na sisi tumepokea laana hii na ukitaka kujijua una laana ni pale unanuna mwenzako akiwa amefanikiwa.

"Sisi ndiyo tunaongoza kurogana wenyewe kwa wenyewe, ila kwa mjini uchawi ni majungu fitina na chuki ili mtu akwame", alisema  Makonda na kuongeza;

"Kuna watu tumewakuta kazi yao kusema amekuja hapa hajui kuvaa, je wewe uliyekuwepo umefanya nini? kuna watu wako mjini kwa maneno tu hatuwezi kupiga hatua kwa kupigana majungu."
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )