Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 6, 2019

Marekani Yapeleka Wanajeshi Gabon ili Kukabiliana na Machafuko yoyote yanayoweza Kutokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

adv1
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema nchi yake imewapeleka wanajeshi 80 mjini Libreville, Gabon kuwalinda raia wa Marekani na ubalozi wa Marekani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Katika barua aliyowasilisha Bungeni jana, Trump alisema wanajeshi Zaidi huenda wakapelekwa katika eneo hilo kutokana na uwezekano wa kuzuka maandamano yenye ghasia.
 
Barua ya Trump imesema wanajeshi hao: “watabaki katika eneo hilo hadi hali ya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo utakapokuwa imara na uwepo wao usihitajike tena.”
 
Mwishoni mwa wiki Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni ya Marekani ilitoa wito kwa Tume ya Uchaguzi – CENI kuhakikisha kuwa kura zinahesabiwa kwa umakini na kutishia kuwawekea vikwazo watakaohujumu mchakato huo au kutishia Amani na utulivu wa nchi hiyo.
 
Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika ziliiongezea mbinyo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zikiitaka iheshimu matakwa ya wapiga kura wakati muda wa mwisho wa kutoa matokeo ukikaribia.
 
Kuna ongezeko la matarajio kuwa wasimamizi wa uchaguzi watachelewesha matokeo ya mwanzo yanayotarajiwa Jumapili – hatua inayoweza kuongeza hofu katika nchi hiyo isiyokuwa na utulivu.
 
“Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iko katika wakati wa kihistoria kuelekea mpito wa kidemokrasia,” umesema Umoja wa Ulaya. 
 
Umetoa wito kwa maofisa kuhakikisha mat okeo yananayosubiriwa yatatimiza matakwa ya wapiga kura. 

Ombi sawa na hilo limetolewa na Umoja wa Afrika – AU baada ya kupewa tathmini kutoka kwa mkuu wa timu ya uangalizi wa uchaguzi yenye wanachama 80.

“Ni muhimu kuheshimu matokeo ya uchaguzi,” amesema mkuu wa AU Faki Mahamat kwenye Twitter.
 
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana katika kikao cha faragha kuujadili uchaguzi huo, lakini baada ya masaa mawili ya mkutano likashindwa kukubaliana kuhusu taarifa kwa vyombo vya habari. 

Wanadiplomasia wamesema nchi kadhaa yakiwemo mataifa ya Kiafrika yalisema hatua ya aina hiyo itakuwa ya mapema mno.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )