Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, January 12, 2019

Ndege Nyingine Mpya Dreamliner kutua nchini Novemba Mwaka Huu

adv1
Serikali imesema inatarajia kupokea ndege nyingine aina ya Boeing Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262 iliyotengenezwa nchini Marekani.

Dreamliner hiyo  itakuwa ni ya pili baada ya ile ya kwanza ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyotua hapa nchini Julai 8, mwaka jana amabyo hadi sasa inafanya safari zake Entebbe nchini Uganda, Bujumbura nchini Burundi na Visiwa vya Comoro.

Akizungumza jana  katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Airbus 220-300 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema Serikali ilipanga kulifufua Shirika la Ndege nchini (ATCL) kwa kununua ndege mpya Saba.

“Rais Magufuli alipoingia madarakani aliahidi kuifufua ATCL kwa kununua ndege saba lakini juzi kanipigia simu kuniagiza tununue nyingine ziwe nane kabisa, ”alisema Waziri Kamwelwe.

Naye Rais Magufuli alisema pamoja na kuwa aliahidi kununia ndege saba na nyingine zimeshawasili lakini huo si mwisho kwani ana mpango wa kuagiza ndege nyingi zaidi.

“Nataka mjue kuwa ndege hii tunayopokea leo sio ya mwisho nataka kununua ndege nyingine zaidi ambazo zitakuwa zinapishana katika masafa ndani na nje ya Afrika,” alisema Rais Magufuli.

Hadi sasa ndege sita zilizonunuliwa na Serikali zimeshawasili hapa nchini ukiachana na hizo za Airbus 220-300 na Dreamliner nyingine ni Bombadier Dash 8 Q400 tatu zenye uwezo wa kubeba airia 76 kila moja.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )