Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 27, 2019

Lipumba atangaza maombi Leo Jumapili

adv1
Mwenyekiti wa chama Chama cha Wananchi (CUF), anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, Leo Jumapili Januari 27, 2019 ametangaza kuwa watafanya maombi baada ya miaka 17 kupita tangu vurugu za mwaka 2001.

Aliyasema hayo jijini Dar es salaam jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo alisema kuwa imepita miaka 17 tangu zitokee vurugu hizo hivyo chama hicho kimeona kina sababu ya kuwaombea waliopoteza maisha wakati wakidai demokrasia.

“Maombi hayo ni kwa ajili ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha katika vurugu zilizojitokeza mwaka 2001 ikiwa ni baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2000,”alisema Profesa Lipumba

Alisema kuwa maombi hayo yatafanyika katika viwanja vya Mnyamani Buguruni jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni ambapo maombi hayo yataenda sambamba na ofisi zote za chama kupeperusha bendera nusu mlingoti.

Chama Cha Wananchi (CUF) kimekuwa na migogoro isiyokuwa na mwisho baada ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini, Prof. Ibrahim Lipumba kutofautiana na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )