Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, January 16, 2019

Rais Magufuli Apokea Hati Za Utambulisho Kutoka Kwa Mabalozi Watatu Ikulu Jijini Dar Es Salaam

Rais John Magufuli leo Januari 16, 2019,  amepokea hati za utambulisho wa mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mabalozi hao ni Cho Tae-ick wa Korea Kusini, Glad Munthali wa Malawi na Antonio Cesar wa Brazil, wote wakichukua nafasi za watangulizi wao ambao walimaliza muda wao Desemba, mwaka jana.

Cho Tae-ick ambaye aliwasili nchini Desemba 14, 2018, amechukua nafasi ya mtangulizi wake, Balozi Song Geum Yong ambaye alimaliza muda wake.

Naye Glad Munthali ambaye aliwasili nchini Desemba 28, amechukua nafasi ya mtangulizi wake, Balozi Hawa Ndilowe ambaye muda wake ulikwisha Julai, 2018 na kuondoka nchini mwishoni mwa mwaka jana.

Kwa upande wake, Cesar aliwasili nchini Januari 3 na kuchukua nafasi ya Balozi Carlos Alfonso Puente ambaye pia muda wake ulikwisha Desemba 2018. Mabalozi wote watawakilisha nchi zao kwa muda wa miaka mitatu.

Katika mazungumzo yao na Rais Magufuli, walijadili kuhusu kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na nchi zao na Rais Magufuli aliwaeleza dira ya Serikali yake na kuwakaribisha kushiriki katika biashara na uwekezaji hapa nchini.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Damas Ndumbaro.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )