Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, January 23, 2019

Rais Magufuli Awapa Nafasi Viongozi wa Dini Wafunguke Yote Waliyonayo Moyoni

Rais John Magufuli amesema kukutana na viongozi wa dini ni aina mpya ya kuukaribisha mwaka wa 2019 huku akiwataka kuongea wanayoyaona na kuwakosoa walipokosea kiutendaji.

Amesema kufanya hivyo huenda ikawa ni nafasi ya kupata ushauri kutoka kwa viongozi hao kwa sababu wameona utendaji wao kwa miaka mitatu.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumatano Januari 23, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam ambako anakutana na viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali ili kuzungumza nao masuala yanayohusu nchi.

“Naamini leo inaweza kuwa siku ya kwanza kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali kukaa pamoja Ikulu, hii inaashiria umoja na mshikamano na inaweza kuwa siku ya upatanisho kiroho,” amesema Rais Magufuli na kuongeza:

“Karibuni. Nitapenda kusikiliza kutoka kwenu, mimi leo nitasikiliza tu na ninyi  mtazungumza kama yatakuwapo machache nitayaongea.”

Amesema kila alipokuwa anaomba wamuombee walikuwa wakifanya hivyo ndiyo maana akaona atafute namna ya kuwashukuru.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...