Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, January 15, 2019

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Apigania Haki za Walimu

Na Tiganya Vincent,
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Leah Ulaya, amewaomba Watendaji Wakuu wa Halmashauri ya Manispaa, Wilaya na Mji mkoani Tabora kujali haki za watumishi walio chini yao, ili kuondoa manung’uniko yanayoepukika.
 
Amesema hatua hiyo itasaidia kuendeleza mshikamano na ushirikiano baina ya watumishi na serikali na kufanya kuwepo na utendaji wa pamoja.
 
Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa elimu mkoani hapa, Ulaya alisema mambo mengine yanayodaiwa na watumishi wakiwemo walimu yako ndani viongozi kama vile Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Maofisa Utumishi na Maofisa Elimu, hivyo hayaitaji viongozi wa wizara ndio mtumishi apate haki yake.
 
“Ombi langu kwa viongozi wetu wa mkoa wa Tabora maofisa utumishi, maofisa elimu na wengine wote tuhakikishe tunajali haki za watumishi wetu husasani walimu, yapo mambo ya kawaida ambayo yapo chini yenu kama Mkurugenzi,” alisema.
 
Aidha, Ulaya alisema mwelekeo wa CWT ni kuhakikisha inasimimia wajibu wa Mwalimu kufanyakazi zake kwa ufanisi kwa sababu inaamini bila ya kutumiza wajibu walimu hawatakuwa na haki ya kudai kile wanachostahili kudai.
 
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, aliwataka Wakurugenzi Watendaji na maofisa wanaoshughulikia masuala ya utumishi wanapowapandisha madaraja watumishi wakiwemo walimu wahakikishe wanabadilisha na mishahara yao na sio kubaki na ile ya cheo cha zamani.
 
Aliongeza kuwa wanaohamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine pia wanapaswa kuwalipa stahili zao kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya utumishi wa umma inavyotaka kabla hajaondoka katika kituo chake za zamani kuelekea kipya.
 
Naye Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Tabora, Hamis Lissu, alisema wamekutatana kwa lengo kujenga desturi ya uwajibikaji wa pamoja katika kufikia malengo yaliyokusudiwa ya utoaji elimu bora katika Mkoa wa Tabora.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )