Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, January 27, 2019

RC Makonda Kumuenzi Askofu Pengo Kwa Kuipa Barabara Jina Lake Kama Zawadi Ya Heshima


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda katika kuthamini na kutambua mchango mkubwa wa Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo katika kuhubiri umoja na mshikamano ndani ya Jamii ametangaza kumuenzi kwa kuchagua Barabara moja ya kisasa mkoani humo na kuipa jina la Baba Askofu ili azidi kukumbukwa vizazi na vizazi.

RC Makonda amesema Baba Askofu Pengo amekuwa mfano wa kuigwa katika kuhubiri Amani, Upendo na umoja wa kitaifa na hajawahi kuona haya kukemea uovu wowote jambo ambalo Kama Mkoa umeona ni vizuri kumuenzi kwa kumpatia heshima hiyo.

Kwa upande wake, Baba Askofu Mwadhama Polycarp Kadinari Pengo amemshukuru RC Makonda kwa kutambua mchango wake ambapo amesema ataifanyia maombi barabara hiyo isiwe na matukio ya uhalifu wa ajali.

Hayo yote yamejiri jana wakati wa ufunguzi wa majengo mapya ya Bweni la wasichana, Ukumbi na gari ya shule ya Sekondari St. Joseph Millennium ya Goba.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )