Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, January 10, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 48

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
Biyanka akanijibu kwa heshima zote, kiburi na dharua zote alizo kuwa akinifanyia jana usiku zote zimemuisha. Tukarudi hotelini na Jojo huku tukiwa na furaha kubwa sana kwani mpango wetu umekwenda kama vile tulivyo panga.
“Hongera”
“Nashukuru Jojo, nakushukuru sana kwa kile ulicho nifanyia”
“Usijali, huyu binti amesha nipatia namba yake”
“Waoo sasa muda wa kwenda kuwaangusha maadui zangu hivi sasa umewadia. Umeona jinsi dharau zake zilivyo muisha”
“Yaa sasa kama unafanya kweli kweli mapenzi hakikisha kwamba unafanya kweli na ukimpata hakikisha ana kupenda kupitiliza na akisha kolea hakikisha kwamba una mpa pigo kubwa sana yeye na baba yake naamini kwamba huo ndio utakuwa anguko lao umenielewa”
“Nimekuelewa nanitafahanya hivyo kuhakikisha kwamba ninawaangusha chini yeye na familia yake.”

ENDELEA           
Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na tabasamu  pana sana usoni mwangu. Jojo akampigia Dany na kumpa habari hii.
“Camila anahitaji kuzungumza nawe”
“Sawa sawa”
Nikaipoke simu hii na kuingia bafuni.
“Niambie mke wangu”
“Safi ehee niambie ni nini kinacho endelea?”
“Mipango inakwenda vizuri na hadi ninavyo zungumza hivi sasa nimenunua kampuni moja ya simu inaitwa ZAiartel”
“Wooo kweli mume wangu?”
 
“Ndio na kupitia hi kampuni sasa nitaanza kumsogelea adui yangu na nikimtia mikononi basi nitahakikisha kwamba anajutia kwa yale yote ambayo amenifanyia kwenye maisha yangu”
“Sawa mume wangu nina kuamini sana nina imani kwamba huto niangusha”
“Usijali mpenzi wangu nitahakikisha kwamba, tunarudi Ujerumani tukiwa na ushindi mkubwa sana, sawa mama”
“Sawa mume wangu”
 
“Nitakufahamisha kila jambo ambalo litatokea”
“Sawa mume wangu, nakupa muda na uhuru wa kuweza kufanya jambo lolote ili mradi uhakikishe kwamba una fanikisha kile kitu ambacho unakihitaji kukifanya”
“Nashukuru mke wangu”
Tukamaliza kuzungumza na Camila na kukata simu. Jioni ikawadia na Jojo akawasiliana na Biyanka na kumpa maelekezo ya wapi anaweza kutukuta. Tukajianda ana kueleeka katika hoteli nyingine ambayo nayo ina hadhi ya nyota tano. Biyanka akafika katika eneo hili la hoteli akiwa ameongozana na walinzi wake wa kike, nikamkaribisha kwa furaha pasipo kuonyesha kwamab niliweza kuchukizwa na tabia yake ya kunidharau jana jioni.
 
“Pole kwa kuweza kukusumbua”
“Usijali mkuu ni jukumu langu nami nakuomba msamaha kwa yale yote ambayo nilikufanyia jana. Kichwa changu kidogo hakikuwa sawa ndio maana yakatoka yale yaliyo tokea”
“Nimekusamehe, ehee kampuni sasa ipo mikononi mwangu, niambie biashara inakwenda vipi na changamoto ni zipi kwa wafanyakazi walipo hivi sasa?”
“Biashara kwa sasa imeweza kuyumba kidogo kwa nchi yetu ya Tanzania. Uchaguzi kidogo umeyumbisha uchumi, ila nina imani raisi ajaye anaweza kufanya mambo mazuri sana na kusimamisha tena uchumi wa hii nchi”
 
“Ni kweli, japo sipo Tanzania kwa miaka mingi kidogo ila naipenda sana nchi yangu”
“Nafurahi sana kuweza kusika hivyo mkuu”
“Ehee ni nini ambacho natakiwa kuongeza na nini natakiwa kupunguza katika kuhakikisha kwamba ninadumisha kampuni yangu?”
“Kwa haraka haraka mkuu unachotakiwa kukifanya ni kujali maslahi ya wafanyakazi, kwani kwa miezi ya hivi karibuni, kampuni iliweza kupunguza wafanyakazi kutokana na kuyumba. Pili ushindani katika soko, wenzetu wenye mitandao wanajua jinsi ya kupangilia ofa zao. Kupangilia matangazo yao, ila sisi tulishindwa kutokana na kuyumba kiuchumi”
 
“Ohoo sawa hili nitalitazamia kwa jicho la umakini. Ehee jambo jengine?”
“Kitu kingine ni kuwa karibu na serikali, hususani mgombea anaye gombani kiti cha uraisi kwa chama tawala.”
“Ambaye ni baba yako…..”
“Ohoo kumbe umesha mfahamu?”
“Ndio nimemfahamu na mimi ni shabiki yake namba moja na kama atahitaji nimuunge mkono, kwangu haito kuwa shida kabisa nitahakikisha kwamba anashinda kwa kishindo”
“Ohoo asante sana mkuu”
 
“Niite Ethan, mkuu ni Mungu pekee ila sisi wote tusimame kwa majina yetu”
“Sawa sawa”
Biyanka alizungumza kwa furaha kubwa sana huku moyoni mwangu nikijiapiza kwamba furaha hiyo itakuw ani huzuni na mateso makubwa sana kwake pale nitakapo hakikisha kwamba nimemuweka mikononi baba yake aliye nipotezea wazazi  wangu.
“Kesho naomba uitishe kikao na wafanyakazi wote, hata wale wa hali ya chini namaanisha wale wafagizi, nahitaji kuzungumza nao kisha baada ya hapo tutajua nini cha kufanya”
 
“Sawa sawa Ethan”
“Kitu kingine, kumbuka kwamba mimi ni kijana mdogo sana. Hivyo mambo yangu nayapeleka kasi sana. Uvivu na uzembe ni adui mkubwa sana kwangu. Kama atakuwepo mtu mwenye asili  hiyo katika kampuni yangu basi nitahakikisha kwamba ninamtoa mara moja kwenye kazi yangu”
“Usijali bosi kila jambo litakwenda kama vile unavyo hitaji”
“Nafasi yako haito kuwa na mabadiliko yoyote”
“Nashukuru sana Ethan, nitahakikisha kwamba nina ifanya kazi hii kwa uwezo wangu wote hadi pale utakapo nichoka”
“Siwezi kukuchoka”
Nilizungumza huku nikimtazama vizuri Biyanka usoni mwake, ni binti mzuri, anaye jipenda na ana vigezo vyote vya kuitwa mwanamke mzuri, taratibu nikamshika kiganja chake cha mkono wa kulia na kuanza kuupapasa na kidole changu gumba.
 
“Eth…”
“Ohoo samahani”
Nilizungumza huku nikimuachia kiganja chake.
“Hapana ila kidogo nimejawaliwa aibu”
“Hahaa….vipi shemeji anasemaje?”
“Hapana sina mwanaume Ethan”
“Kwa nini?”
“Bado sijamuona mwanaume wa kuwa naye”
“Mmmmm”
“Kweli wanaume wengi ni wadanganyifu na mimi huwa nina linda heshima yangu na usichana wangu”
 
“Hongera sana”
“Ahaa kawaida”
Tukazungumza mambo mengi sana katika usiku huu, hadi majira ya saa tano nikamruhusu Biyanka na akaondoka na walinzi wake. Hatukuona sababu ya kuendelea kuwemo hapa hotelini, tukaanza safari ya kurudi katika hoteli yetu.
“Vipi umefanikiwa?”
Jojo aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Asilimia sabini na tano hizo ishirini na tano nitazimalizia siku kadhaa zijazo”
“Kazi nzuri, ila angalia usije ukamsahau Camila kwa maana nimekuona umejiachia sana kwake”
“Hahaa usijali siwezi kumsahau mpenzi wangu, Camila nimekua naye toka tupo watoto dogo sana”
“Sawa”
                                                                                                          ***
    Alfajiri na mapema tukafika ofisi, nikamkuta Biyanka pamoja na wafanyakazi kadhaa, nikasalimiana nao na Biyanka akaanza kunitembeza kwenye jengo hili zima la kampuni hii niliyo inunua. Hadi inatimu saa mbili asubuhi tukawwa tumemaliza kulitembea jengo hili. Kama nilivyo agiza ndivyo jinsi Biyanka alivyo fanya. Wafanyakazi wote hadi wafagizi wa hii kampuni wakakusanyika katika ukumbi mkubwa wa kampuni hii. 

Biyanka akaanzisha kikao cha kampuni hii huku akinitambulisha kuwa ndio mmiliki mpya wa kampuni hii. Wasaa wa mimi kuzungumza ukawadia, taratibu nikasimama kwenye kiti nilicho kikalia na kusimama eneo lenye kipaza sauti. Nikawatazama wafanyakazi hawa kwa sekunde kadhaa kisha nikatabasamu kidogo.
 
“Habari za asubuhi”
Wafanyakazi wote wakaitikia salamau yangu. Kitu nilicho kigundua kwa haraka juu ya wafanyakazi hawa ni hali  ya woga pamoja na kukatishwa tamaa na kazi ambayo wanaifanya.
“Nashukuru kwa uwepo wenu hapa. Machache ambayo nitahitaji kuyazungumza ni mshikamano, umoja, upendo na kufanya kazi kwa juhudi ndio kitu muhimu katika kuhakikisha kwamba maisha yanu yanakuwa mazuri”
 
“Nitahakikisha kwamba ninapitia mikataba ya kila mfanyakazi mmoja mmoja na wale ambao hawajapewa mikataba nao tutawapa mikataba yao na nitaongeza mshahara ndani ya mwezi ujao.”
Wafanyakazi wote wakapiga makofi huku wakiwa na furaha kubwa sana.
“Napenda kuhakikisha kwamba ndani ya miezi michache kampuni yetu inakuwa ni namba moja kwa mauzo hapa nchini Tanzania, ila mukinipa ushirikiano wenu nina imani kwamba tutafikia malengo hayo ambayo nimewaeleza hivi sasa. Nashukuru sana kwa muda wenu na ninaomba tuendelee na majukumu yetu”
 
Nilipo maliza kuzungumza wafanyakazi wakaanza kuondoka huku wakiwa na furaha kubwa sana, tukaongozana na Biyanka hadi ofisini kwangu.
“Nani ni mkurugenzi wa waajiriwa?”
“Yupo”
“Basi muambie ahakikishe kwamba mikataba ya wafanyakazi wote inapitiwa upya nikiwa ninaidhibitisha au fanya hivi nahitaji mikataba ya wafanyakazi wote ofisini kwangu”
“Sawa Ethan, ila kuna jambo moja ambalo umelizungumza pale na sasa tupo mwanzoni mwa mwenzi je hadi mwenzu ujao kweli litakuwa limekamilika?”
 
“Jambo gani?”
“Juu ya kuwaongezea mishahara wafanyakazi?”
“Usijali nitajua ni jinsi gani nitavyo hakikisha kwamba hili swala linakwenda kwenye mstari na hivi benki muna kiasi gai kama kapuni hivi sasa?”
“Pesa ziliszo acha na mmiliki aliye pita ni milioni mia mbili za Kitanzania”
“Hayo ni mauzo ya muda gani?”
“Sio mauzo ya muda, ni pesa alioyo iacha kwenye kampuni ili mmuliki mwengine atakapo kuja aweze kuziendelezea katika kuendesha kampuni”
 
“Sawa nimekuelewa fanya nilicho kuambia”
“Sawa Ethan”
Biyanka akatoka chumbani humu na kuniacha ofisini kwangu, baada ya dakika kumi, mkurugenzi anaye shuhulika na maswala ya waajiriwa akafika ofisini kwangu akiwa na mikataba ya wafanyakazi wote. Nikamsalimia mwana mama huyu kisha akaanza kunionyesha mikataba ya wafanyakazi wa ngazi za juu ikiwemo wakurugeni wa vitengo vyote.
“Nashukuru mama yangu, niwekee hapo nitaipitia leo”
“Sawa mkuu”
 
“Niite tu Ethan mama yangu”
“Sawa mimi ninaitwa Bi Agatha Kimaro”
“Ahaa nashukuru mama Kimaro”
“Naweza kuzungumza nawe kidogo?”
“Ndio kuwa huru tu mama yangu”
“Hakika nimependa kile ulicho kizungumza, ni ndani ya dakika mbili ila umezungumza vitu vyenye poiti kubwa na nisikufiche, umenipa moyo wa kuitumikia hii kampuni. Naomba maneno yako yasimame mwanangu katika kile kitu ulicho kusuida kufanya juu yetu na Mungu akubariki mwanangu”
 
“Nashukuru sana mama, naamini mutazidi kunisaidia”
“Wala usijali katika hilo mama yangu, nipo pamoja nanyi”
Mama Kimaro akatoka ofisini kwangu. Nikaendelea kupitia taarifa kadhaa za kampuni hii, hadi inafika muda wa wafanyakazi kutoka ofisini hapa sikuweza kumaliza kazi nilizo kusudia kumaliza hapa na kunilazimu kuongeza muda wa ziada katika kuifanya kazi. Nikamruhusu Jojo kurudi hotelini na kumpa maagizo ya kuja kunichukua saa tatu usiku. Mida ya saa moja usiku mlango wa ofisi kwangu ukagongwa, nikamruhusu anaye gonga mlango aweze kuingia ndani.
 
“Ethan kumbe bado hujaondoka?”
Biyanka alizungumza huku akiingia ofisini kwangu. Nikamsindikiza kwa macho hadi kwenye kiti alicho kikalia. Taratibu nikasimama na kuzunguka kwenye meza hii kubwa ya hapa ofisini kwangu, nikakaa juu ya meza huku nikimtazama Biyanka kwa macho makali, taratibu nikamshika kidevu chake kwa kiganja cha mkono wangu wa kulia kisha nikamnyanyua uso wake na tukatazama. Biyanka akasimama taratibu akasimama na mikono yake akaiweka juu ya mapaja yangu huku tukitazamana na midomo yake akianza kuing’ata ng’ata akiashiria kwamba ana haja ya kuhitaji kile nilicho kikusudia kumfanyia na sasa ndege niliye mtega anaanza kuingia kwenye tundu bovu.

==>>ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )