Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, January 12, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 50

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA             
      
Nikarudi ofisini kwangu huku kichwa changu kikiwa kimechoka kwa kweli kwani kazi niliyo ifanya kwa siku ya leo ni kubwa kuliko kawaida.
“Pole mpenzi wangu kwa kuchoka”
Biyanka alizungumza huku akizunguka meza yangu na kusimama nyuma ya kiti changu na kuanza kuniminya minya mgongoni mwangu.
“Nashukuru mpenzi wangu”   
“Nimezungumza na baba leo na nimemueleza juu ya mahusiano yetu na sifa zako zote, ameniomba leo usiku twende nyumbani kwake tukajumuike chakula cha usiku.”
Habari hii kidogo ikanistua sana, kwani sikutarajia kwa haraka hivi ninaweza kukutana na adui yangu ambaye nimejiapiza moyoni mwangu kwamba ni lazima niweze kumfanyia kitu ambacho hakuwahi kufanyiwa kwenye maisha yake yote.
   
ENDELEA
“Mbona umestuka mpenzi wangu vipi?”
“Ni suprize uliyo nifanyia kwa maana sikutarajiua kuweza kukuata na raisi mtarajiwa wa hii nchi”
Nilizungumza kwa unafki kidogo kwani chuki na mipango ya kumuangusha baba yake ni mikali sana.
“Yaa ni kweli nimekufanyia suprize mpenzi wangu, yote nahitaji ufahamu kwamba nina kupenda na kukuhitaji kwenye maisha yangu.”
“Nashukuru sana”
“Ngoja nielekee ofisini kwangu, kuna kitu ninakwenda kukichukua muda si mrefu”
“Sawa”
Biyanka akatoka ofisini humu, nikampigia simu Jojo na kumuomba aweze kufika ofisini kwangu. Baada ya sakika kadha Jojo akaingia na kukaa katika mojawapo ya kiti.
“Mipango inazidi kwenda vizuri”
 
“Kivipi?”
“Biyanka anahitaji  leo twende kwa baba yake”
“Weee”
“Haki ya Mungu vile tunakwenda kupata chakula cha usiku”
“Mmmm sasa hapo kazi inakwenda vizuri. Ila kwa ushauri wangu wa haraka haraka kwako. Hakikisha kwamba hasira yako unaificha, usimuonyeshe ishara ya aina yoyote mzee huyo. Umenielewa?”
“Nimekuelewa”
“Na kigtu kingine nimepokea simu kutoka kwa baba kuna kazi anahitaji niweze kumsaidia kuifanya”
“Kazi gani?”
“Bado hajaniweka bayana ila akinipatia maelezo nitakujulisha”
 
“Sawa, basi jiandae jioni tunaeleka nyumbani kwao”
“Mmmm unaonaje ukaenda peke yako”
“Peke yangu?”
“Ndio, kumbuka kule ni ukweni kwako kwa uwongo, hivyo unatakiwa kujiandaa vizuri”
“Mmmmm”
“Yaa”
“Sawa kutokana nipo na walinzi  wake basi naamini nitakuwa salama”
“Sawa sawa, nikusubirie nje au unaelekea ukiwa na nguo zako”
“Nitakwenda hivi hivi hakuna haja ya kubadilisha nguo”
“Basi acha nieelekee hotelini”
“Sawa”
Jojo akaniaga na kutoka ofisini kwangu, baada ya muda kidogo Biyanka akaingia huku akiwa ameshika faili moja.
“Tunaweza kwenda sasa mpenzi wangu. Tupitie nyumbani kwangu, tujiendae kisha twende huko”
 
“Mmmm sawa, kwa mimi hivi si nipo poa?”
“Yaa hapo cha kubadilisha labda ni shati, ila tutapitia katika maduka na kununua shati jengine”
Tukaondoka ofisini hapa, tukapita katika moja ya duka la nguo, tukanunua nguo zangu za kuvaa usiku huu kisha tukaelekea nyumbani kwa Biyanka. Tukajiandaa na kuelekea nyumbani kwako, njia nzima Biyanka ametawaliwa na furaha kubwa sana. Furaha ambayo kusema kweli kwa upande wangu nina jiapia ipo siku moja watakuja kulia kilio kimoja cha kusaga meno.
 
Tukafika katika moja ya jumba la kifahari, ulinzi mkali umeimarishwa kwenye kila eneo la nyumba hii. Tukapokelewa na mwana mama mmoja aliye valia mavazi ya thamani kubwa.
“Huyu ni mama yangu”
Biyanka alinitambulisha, nikampa heshima zote mwana mama huyu, akanikumbatia huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.
“Mama mchumba wangu anaitwa Ethan. Ethan huyu ndio mama yangu mzaa chema.”
“Nashukuru kukufahamu”
“Hata mimi ninashukuru kukufahamu. Karibuni ndani”
Mwana mama huyu alizungumza kwa furaha kubwa sna. Tukaingia ndani, sebleni tukamkuta mzee Poul Mkumbo, akanyanyuka kwenye sofa na kusalimiana nasi kwa furaha.
“Biyanka njoo”
 
Mama alizungumza na wakaondoka na Biyanka sebleni hapa na kuniacha na mzee huyu.
“Ndio kijana habari yako”
“Salama kabisa baba”
“Umesema unaitwa nani?”
“Ethan Klopp?”
“Ohoo wewe ndio yule kijana mchezaji mpira?”
“Ndio mimi mzee”
“Safi sana sifa zako nimezisikia sikia uwanjani, nina imani kwamba binti yangu amepata kijana mzuri atakaye mjali”
“Ndio muheshimiwa”
Nilizungumza kwa kujikaza tu, ila kusema kweli moyoni mwangu ninajisikia vibaya sana kukaa eneo moja na mzee huyu.
 
“Ehee niambie asili yako wewe ni nani, umetoka wapi kwa maana sura na muonekano wako ni wakitanzania kabisa”
“Mimi ni Mtanzania kwa kuzaliwa hapa. Walenzi wangu ambao ni mzee Klopp walinichukau kwenye moja ya kituo cha kulelea watoto yatima, nikiwa mdogo sana. Hivyo nimekulia Ujerumani”
“Ahaa kwa hiyo hawakuweza kukuambia maisha yako ya nyuma kwa undani sana?”
“Hapana kwa maana maisha ambayo walinieleza ni kuhusiana kituo hicho cha watoto ya tima na waliniambia kwamba hicho kituo kwa sasa hakipo”
Ilinibidi kuongopea historia ya maisha yangu ya nyuma ili nizidi kuficha uhalisia wangu kwao.
“Ahaa sawa sawa. Ila pole sana kwa kuto weza kuwafahamu wazazi wako”
 
“Ninashukuru sana mzee”
“Jamani chakula tayari”
Mama alizungumza huku akitutazama.
“Ohoo mkwe twende tukapate ridhiki kidogo”
Tukanyanyuka hapa sebleni na kuelekea kwenye eneo ilipo meza ya chakula. Tukakuka vyakula vingi vikiwa vimeandaliwa. Mimi na Biyanka tukaka kwenye viti vya karibu kabisa huku tukiwa tunatazamana na mama huku mzee Poul Mkumbo akiwa amekaa upane mwengine wa hii meza. Biyanka akaniandalia chakula changu kisha akaanda chakula cha kwake kisha taratibu tukaanza kula taratibu.
“Ethan maswala ya mpira na biashara una yahimili vipi kwa wakati mmoja”
Mzee Poul Mkumbo alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
 
“Kila kitu kina ratiba yake. Kutokana bado sijaanza kucheza mpira kama mchezaji maalumu wa timu fulani, hivyo kwa kipindi hichi ninaweza kujali biashara zangu pamoja na makampuni makubwa ambayo nimeachiwa na baba yangu”
“Ahaaa sawa sawa. Una kampuni ngapi?”
“Hii niliyo inunua ni kampuni ya kumi na nne”
“Waooo zote ni mali yako?”
“Kwasasa zipo chini yangu kwa maana baba amenirithisha”
“Sawa sawa”
Tukamaliza kupata chakula cha usiku, mzee Poul Mkombo akaniomba nikazungumze naye katika ofisi yake iliyomo ndani ya jumba lake hili. Tukaingia katika ofisi yake na akanikaribisha kwa furaha sana.
“Kijana wangu kwanza nafurahi sana kuweza kuwa na binti yangu, nina mambo machache ya kuzungumza nawe nikiwa kama baba”
 
“Sawa sawa mzee”
“Hivi una mpenda kweli mwanangu au upo naye kwa maslahi binafsi ya kibiashara kwa maana ninakwenda kuwa raisi, sasa usije ukaitumia nafasi hiyo kuwa ngao katika serikali yangu nitakayo kwenda kuitengeneza?”
Nikamtazama kwa sekunde kadhaa mzee Poul Mkumbo kisha nikatabasamu.
“Nimempenda binti yako. Na sina mpango wowote wa kumfanya kama ngao katika biashara zangu kwa maana nimewekeza katika nchi karibia zote za barani Ulaya na nina ingiza kiasi kikubwa ana cha pesa hivyo swala la kununua kampuni hapa Tanzania, si kwamba nina shida ya kiuchumi, hapana ni moja tu ya kuifanya serikali yangu iweze kuongeza mapato yake ya kiuchumi kwa kupitia kodi ambayo nitalipa nikiwa kama mmiliki wa kampuni yangu”
 
“Ahaa sawa sawa, nafurahi kusikia hivyo kijana, je utanisaidia vipi baba yako mkwe katika kuchukua kiti cha uraisi?”
Nikaka kimya huku moyoni mwnagu nikiwa nimejawa na furaha kubwa sana, kwani ndege mjanja anakwenda kuingai kwenye kumi na nane zangu.
“Siasa kama siasa, sijajua siasa za huku Afrika kutokana sijaishi sana miaka mingi. Ila siana inahitaji pesa na kama ni pesa basi isiwe ni pesa ndogo. Pesa nyingi, wananchi wanatakiwa kupata imani kwa yule ambaye wanakwenda kumPa dhamana ya kuwaongoza. Hivyo msaada wangu hapo mkubwa utakuwa ni pesa”
 
Mzee Poul Mkumbo akatingisha kichwa huku akiwa amejawa na furaha.
“Ndio maana sina mashaka kabisa na wewe katika swala zima la kuwa na binti yangu kwa maana ukiona mtu ana uwezo wa kumiliki kampuni zaidi ya kumi na basi ana akili ya ziada”
“Ni kweli”
“Nitataka kujua mpango wako wa kampeni upo vipi, kisha nijue ni jinsi gani ninaweza kukuunga mkono”
“Sawa sawa, sasa hivi tunakwenda kwenye mchujo wa kichama. Huo nimesha andaa watu wangu ambao  wataniunga mkono na nina imani kwamba jina lango halito katwa”
 
“Sawa ni mpango mzuru, jina lako likipita basi nitahakikisha kwaba unaichukua ikulu”
“Nafurahi kusikia hivyo na nina kuahidi nitahakikisha kwamba ninakupa nafasi kubwa ya kuweza kuwekeza katika kila jambo ambalo utalihiaji kulifanya hapa Tanzania”
“Nashukuru baba mkwe”
“Ehee vipi mumesha zungumzia swala zima la ndoa yenu?”
“Hapana, ila ukiwa tayari katika kufunga ndoa na Biyanka basi tutawafahamisha”
“Basi niwaombe muwe wavumilivu kidogo, nikisha chukua ikulu basi nitawaruhusu kufunga ndoa”
“Sawa baba”
Tukamaliza mazungumzo na mzee Poul Mkumbo, kisha tukatoka ofisi humu na kurudi sebleni. Tukazungumza mambo mawili matatu na mama mkwe kisha tukaaga na kurudi nyumbani kwa Biyanka.
 
“Nimefurahi kuoanana na wazazi”
Nilizungumza huku nikivua koti langu la suti na kumkabidhi Biyanka.
“Kweli?”   
“Ndio mpenzi wangu. Nimefurahi sana na kuna mambo mengi sana nimeweza kuzungumza na baba, nina imani kwamba nitamsaidia kwa asilimia mia moja kuhakikisha kwamba anaingia ikulu”
“Kweli?”
“Ndio mpenzi wangu, kwa sasa tumesha kuwa familia moja”
“Asante mepenzi wangu”
Biyanka alizungumza huku akinikumbatia kwa nguvu
                                                                                                              ***
    Siku zikazidi kusonge mbele huku kampuni yangu ya mawasiliano ikikua kwa kasi sana. Ndani ya mwenzi mmoja kampuni yangu ikashika namba mbili kwa mauzo kati ya kampuni kumi zinazo shuhulika na maswala ya mawasiliano ya Tanzania. Kama nilivyo waahidi wafanyakazi wangu, nikaongeza mishahara yao kwa asilimia ishirini na tano kwa kila mmoja, jambo lililo zidi kuniletea sifa kubwa kwa wafanya kazi wangu. Kadri siku zilivyo zidi kwenda ndivyo jinsi Biyanka alivyo zidi kunipenda na kuchanganyikiwa kwa penzi langu, kichwani mwangu sikuweza kumsahua Camila, ambaye kila siku huwa nina zungumza naye kupitia simu.
Mzee Poul Mkumbo akafanikiwa kuchaguliwa jina lake kuwa mgombea uraisi katika chama chake cha siasa.
“Ethan”
Niliisikia sauti ya Ethan mwenzangu ikiniita katika ufahamu wangu wa akili
 
“Ndio”
“Muda wa kurudi Ujerumani sasa una karibia, na binti wa watu hivi sasa anahitaji kuwa nawe, kila siku ninajitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kwamba anakuwa ni mtu mwenye furaha pasipo kuwa nawe”
Nikashusha pumzi yangu huku nikijishika paji langu la uso kwa mkono wangu wa upande wa kulia.
“Huku mipango yangu sasa ndio inakwenda kukamilika”
“Itachukua mud asana”
“Kwa nini sana?”
“Kumbuka kwamba tayari baba Camila amesha shinda uchaguzi na zimebaki wiki chache kabla hajaapishwa kuwa raisi wa Ujerumani”
“Kwa hiyo unataka turudi Ujerumani pasipo mimi kufanya jambo lolote kwa huyu mzee?”
“Ukiwa Ujerumani unaweza kukamilisha mipango yako”
“Kivipi?”
“Kwanza unatakiwa kukipa nguvu chama pinzani kwa siri sana. Pili  hakikisha kwamba una wapa mipango yote ya adui yako ambayo anakwenda kuifanya. Unajua kwamba siasa ni vita, pasipo kuwa na silaha basi adui yako  hawezi kuanguka”
 
“Ehee na huyu binti yake je nitaachana naye vipi?”
“Huyo muage muambie kwamba asimamie kampuni kuna mambo yametokea Ujerumani na unahitaji kwenda kuyashuhulikia kwa haraka sana”
“Unahisi kwamba hilo swala atalielewa?”
“Wewe ni mwanaume hakikiasha kwamba ana kuelea na hiyo ndio itakuwa tiketi ya kumuacha”
“Je kampuni yangu akiamua kuisambaratisha kutokana na kulipa kisasi cha mapenzi je itakuwaje?”
“Nitashuhulika naye mimi hapo”
“Utamfanya nini?”
“NITAMUUA”

==>>ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )