Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 13, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 51

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA 
      
“Kivipi?”
“Kwanza unatakiwa kukipa nguvu chama pinzani kwa siri sana. Pili  hakikisha kwamba una wapa mipango yote ya adui yako ambayo anakwenda kuifanya. Unajua kwamba siasa ni vita, pasipo kuwa na silaha basi adui yako  hawezi kuanguka”
“Ehee na huyu binti yake je nitaachana naye vipi?”
“Huyo muage muambie kwamba asimamie kampuni kuna mambo yametokea Ujerumani na unahitaji kwenda kuyashuhulikia kwa haraka sana”
“Unahisi kwamba hilo swala atalielewa?”
“Wewe ni mwanaume hakikiasha kwamba ana kuelea na hiyo ndio itakuwa tiketi ya kumuacha”
“Je kampuni yangu akiamua kuisambaratisha kutukana na kulipa kisasi cha mapenzi je itakuwaje?”
“Nitashuhulika naye mimi hapo”
“Utamfanya nini?”
“NITAMUUA”

ENDELEA
Nikaa kimya huku nikijifikiria sana kwani maamuzi ambayo anataka kuyachukua Ethan kwa Biyanka kwa namna moja ama nyingine hastahili kufanyiwa hivyo.
“Unahisi kumuua Biyanka ni muhimu kweli?”
“Nitamuua pale atakapo hitaji kulipiza kisasi juu yako”
“Ahaa hapo sawa, ila kabla sijaondoka nchini Tanzania nitahitaji kufanya jambo moja”
“Jambo gani?”
“Nahitaji kukutana na mgombea uraisi wa chama pinzani, ninahitaji kuzungumza naye mambo mawili matatu”
“Sawa ila hakikisha kwamba unakutana naye kisiri”
 
“Sawa, ila nitaonana naye vipi ikiwa Jojo simuoni kwa sasa toka alivyo niaga hadi sasa sina mawasiliano naye?”
“Ngoja nitakufahamisha baadaye jinsi ya kuonana naye”
“Sawa”
Ethan akandoka na nikabaki peke yangu ofisini. Mlango ukafunguliwa na akaingia Biyanka huku akionekana akiwa na furaha kubwa sana kwani kitendo cha baba yake kuchaguliwa kuw amgombea uraisi wa chama tawala basi ni moja ya sifa kubwa sana kwenye familia yao.
“Mume wangu unaendeleaje?”
Biyanka alizungumza huku akizunguka kwenye meza yangu, akanibusu mdomoni mwangu kwa furaha sana.
“Salama mama watoto”
“Ahaa nimekuja kukuomba ruhusa mara moja”
“Ruhusa gani?”
 
“Kuna mkutano wa wamama, kidogo mama anakwenda kuzungumza nao hivyo ameomba nimsindikize, si unajua maswala ya kampeni”
“Ahaa sawa sawa, unaweza kwenda. Mimi nitaelekea hotelini nikitoka hapa. Kama utapata nafasi basi unaweza kufika”
“Usijali mpenzi wangu tutawasiliana”
“Sawa”
Tukanyonyana lipsi zetu na Biyanka kisha akatoka ofisini kwangu, nikachukua simu yangu na kumpigia Camila, simu yake ikaita hadi ikakatika, nikarudia kupiga kwa mara ya pili ikaita kwa sekunde kadhaa kisha akapokea.
“Niambie mpenzi wangu?”
“Safi mume wangu vipi?”
“Poa, unendeleaje?”
“Ninaendelea hivyo hivyo”
“Kwa nini hivyo hivyo?”
 
“Nina hamu na wewe mume wangu, nimechoka kukaa huku porini peke yangu. Nahitaji kuja huko huko Dar es Salaam au nirudi nyumbani Ujerumani”
Maneno ya Camila yakanifanya nikae kimya kwa sekunde kadhaa huku nikifikiria ni nini cha kuzungumza.
“Mpango ninakwenda kuukamilisha mpenzi wnagu, ninaomba muda kidogo wa kuvumilia. Sawa mama?”
“Sawa, ila lini utakwisha mpango?”
“Ndani ya wiki moja hivi au mbili”
“Nakupa wiki moja ya mwisho. Ninahitaji haki yangu mume wangu, nimekuwa ni mtu wa kufanya mazoezi magumu ili tu nipoteze hamu  ya kufanya mapenzi, tafadhali Ethan naomba nije”
 
“Sawa mpenzi wangu. Hivi Jojo yupo huko?”
“Nilimuona wiki kadhaa zilizo pita, kwani huko hayupo?”
“Hayupo”
“Unaishije peke yako sasa huko?”
“Nimesha yazoea maisha ya hapa mpenzi wangu”
“Hapana, kesho ninamuomba Dany aniletea huko”
“Kesho”
“Ndio kesho, sahau mambo ya wili moja niliyo kueleza. Kwaheri mume wangu, ninamalizia kufanya mazoezi”
Camila akakata simu na kujikuta mwili wangu mzima ukianza kujawa na joto kali, jasho likaanza kunitiririka usoni mwangu hadi nikajikuta nikivua koti langu la suti. Nikanyanyuka na kuanza kuzunguka zunguka ndani ya ofisi yangu, kwani ujio wa Camila jijini Dar es Salaam unaweza kuniharibia mipango yangu yote niliyo ipanga. Nikapata wazo la kumpigia Dany simu yake, nikaitafuta namba yake na kuipata, nikampigia, simu yake ikaita baada ya muda akapokea.
 
“Ndio Dany”
“Vipi mbona unazungumza kama una wasiwasi mwingi”
“Nina shida”
“Shida gani?”
“Nimetoka kuzungumza na mke wangu hivi sasa, keso anahitaki kuja Dar es Salaam, sasa mpango wangu bado sijaumaliza utanisaidiaje katika hilo ndugu yangu?”
“Ni kweli alisha nieleza hilo jambo leo asubuhi, sasa wewe unatakeje?”
“Nahitaji umlete baada ya wiki moja?”
“Mmmmm sawa nitajaribu, kwa maana hivi sasa mke amekuwa ni king’ang’anizi na anahitaji kuondoka huku”
“Naomba unisaidie kwa kweli”
“Sawa nitajaribu”
“Nashukuru sana”
Nikakata simu, nikatoa kitambaa changu mfukoni na kujifuta jasho langu usoni, hamu ya kukaa ofisini hapa ikaniisha kabisa, nikachukua koti langu na kutoka. Nikiwa katika kordo nikakutana na wadada wawili walio umbika vizuri sana na wamevalia sare za wahudumu wa wateja mapokezi.
 
“Habari yako mkurugenzi”
“Salama, aahaaa…mune elekea wapi?”
“Ofisi ya meneja masoko”
Nikajifikiria kwa muda kidogo.
“Leo ni lini?”
“Ijumaa”
“Okay nani anaye fahamu sehemu inaitwa Bagamoyo?”
Mabinti hawa wakatazamana huku wakitabasamu.
“Sote tunapafahamu”
“Okay, sasa kesho naomba kama hamto jali tuweze kuelekea pamoja kwa maana nahitaji kutembea tembea eneo hilo na mimi ni mgeni hapa jijini Dar es Salaam”
“Sawa mkurugenzi hakuna tatizo”
 
Nikatoa waleti yangu mfuko wa nyuma na kutoa kadi ya biashara zenye namba zangu za simu nikawakabidhi kila mmoja kadi yake, wasichana hawa wakaonekana kufurahi sana kwani namba yangu ni adimu kwa wafanyakazi wa kawaida.
“Ila musimueleze mtu yoyote juu ya hili swala sawa”
“Sawa mkurugenzi, siri  yako ipo salama kwetu”
“Nashukuru. Muna magari?”
“Hapana”
Nikatoa noti mbili za dola mia moja, nikawakabidhi kila mmoja.
“Kesho saa nne mutanipigia simu na nitawaelekeza wapi kwa kuja sawa”
“Sawa mkurugenzi”
 
Wasichana hawa wakazidi kufurahi, hakika Tanzania ina wanawake wazuri sana. Nikaachana hao huku kwa mara kadhaa nikigeuka nyuma, nikaingia kwenye lifti, na moja kwa moja ikanipeleka hadi chini ya ardhi ambapo ndipo yalipo maegesho ya magari ya wafanyakazi wa kampuni hii. Nikaanza kutembea kuelekea kwenye gari langu nilipo liacha, nikiwa hatua chache kutoka lilipo gari langu nikahisi kuna mtu ananifwata nyuma. Nikasimama kisha nikageuka, ila sikuweza kumkuta mtu yoyote, wasiwasi kidogo ukaanza kuniingia kwani eneo  hili limetulia na halina watu kabisa zaidi ya magari mengi yapatayo zaidi ya mia moja.
Nikaanza kutemebea kwa mwendo wa haraka hadi kwenye gari langu, nikatoa funguo mfukoni mwangu na kufungua mlango wa gari kisha nikaingia ndani huku nikijaribu kutazama eneo nilipo toka ili niweze kumuona mtu ambaye alikuwa ananifwatilia.
 
Nikawasha gari hili na taratibu nikaanza kuondoka katika eneo  hili, kabla sijafika katika mlango wa kutokea, gafla mbele yangu akasimama mtoto mdogo mwenye umri kama miaka minne au mitano hivi, jambo ambalo lilinilazimu kufunga breki za gafla ili nisimgonge.
Mtoto huyu akabaki akiwa ameduwaa tu huku hali yake akionekana kudhohofika kwa shida, kwani mavazi yake ni machafu kiasi. Nikashika kitasa cha kufungulia mlango ila roho yangu ikasita kabisa kufungua mlango kwani sifahamu huyu mtoto ameandamana na nani. Nikampigia honi kadhaa, ila mtoto huyu hakusogeza zaidi ya kumwagikwa na machozi usoni mwake. 
 
‘Ametumwa au?’   
Nilizungumza huku nikigeuka na kutazama pande zote za eneo hili ila sikuweza kumuona mtu yoyote. Nikatoa simu yangu mfukoni na kuwapigia walinzi wa eneo hili, nikawaomba waje eneo hili la maegesho ya magari haraka sana, walinzi hawakuchukua muda mrefu sana wakafika nami ndipo nikatoka kwenye gari hili.
“Ninamshangaa huyo mtoto amekataa kutoka mbele ya gari langu kabisa”
 
Niliwambia walinzi hawa mara baada ya kumtoa mtoto huyu mbele ya gari langu.
“Wewe umeingiaje ingiaje humu?”
Mlinzi mmoja alimuuliza kwa kufoka sana.
“Usimfokee hembu mlete”
Nilizungumza kwa upole, mlinzi huyu akamleta mtoto huyu sehemu nilipo simama. Taratibu nikachuchumaa ili niweze kuwa kimo sawa na huyu mtoto, ambaye katika kumtazama kwa ukaribu nikagundua ni mtoto wa kike.
“Unaitwa nani?”
Mtoto huyu akabaki akinitazama huku akiendelea kulia sana kwa uchungu, jambo lililo tushangaza watu wote katika eneo hili.
 
“Binti usilie ehee”
Nilizungumza huku nikitoa kitambaa changu na kuanza kumfuta machozi yake usoni.
“Unaitwa nani?”
Binti huyu hukunijibu zaidi ya kunishika shavu langu la upande wa kulia, taratibu akanikumbatia kwa nguvu sana huku akiendelea kulia. Akatoa kipande cha gazeti kwenye mfuko wa suruali yake hii iliyo chakaa, akanikabidhi kipande hichi cha gazeti, tartibu nikakifungua, sikuamini macho yangu mara baada ya kukuta picha yangu nikiwa uwanjani na timu ya shule ninayo soma.
 
“Mimi ni shabiki yako”
Alizungumza kwa upole sana huku machozi yakimwagika usoni mwangu, nikajikuta nikilengwa lengwa na machozi huku nikimuonea huruma sana huyu binti.
“Nimelitunza hilo gazeti, na jana nilipo kuwa nina omba omba nje ya geti la ofisi yako nilikuona, nilijua nimekufananisha kumbe ni kweli wewe ndio Ethan ohooo”
Binti huyu alizungumza kwa upole na uchungu sana, akanikumbatia tena huku akilia sana. Nikajikuta nami nikimwagikwa na machozi. Sikujali harufu ya uchafu inayo mtoka binti huyu, nikaendelea kukumbatiana naye hivyo hivyo. Nikamnyanyua binti huyu na kuanza kutembea naye hadi kwenye gari langu.
 
“Unaitwa nani?”
“Clara”
“Ohoo Clara?”
“Ndio”
“Una jina zuri sana, nyumbani ni wapi?”
Binti huyu akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akinitazama usoni mwangu. Akatingisha kichwa jambo lililo nifanya nimshange kidogo.
“Uma…maanisha nini?”
“Mimi ni omba omba, sina nyumbani kokote mimi nina lala. Hayo ndio maisha yangu”
 
Nikahisi maumivu makali sana moyoni mwangu, kwani binti mdogo kama huyu hana makazi maalumu.
“Wazazi wapo wapi?”
“Walisha fariki miaka miwili iliyo pita, walipata ajali ya gari hivyo baba mdogo alinichukua na kunilea, ila kwa mateso walio kuwa wakinipatia yeye na mke wake niliamua kutoroka nyumbani na walichukua kila kitu cha baba yangu na kuniacha kama hivi nilivyo”
Maneno ya binti huyu yakazidi kuniumiza moyo wangu. Akafunua shati lake mgongoni, mimi na walinzi wote tukabaki tumejawa na mshangao, kwani ana makovu ya majeraha mengi sana, kiasi kilicho nifanya nizidi kumwagikwa na machozi.
 
“Baba yako mdogo yupo wapi?”
“Anaishi Mbezi kwenye nyumba ya baba”
“Mbezi ni wapi?”
Niliwauliza walinzi hawa huku nikiwatazama kwenye nyuso zao.
“Zipo Mbezi mbili, ni Mbezi Beach au Mbezi ya kimara mtoto?”
Mlinzi alimuuliza mtoto huyu huku akimtazama usoni mwake.
“Mbezi ya chini”
“Ndio ipi?”
Niliwauliza walilinzi.
“Hapo anazungumzia Mbezi ya Kimara”
“Si unapakumbuka nyumbani?”
“Ehee napakumbuka”
“Wewe na wewe ingieni kwenye gari tuelekee huko”
“Sawa mkurugenzi”
Tukaingia kwenye gari na walinzi wa kampuni yangu na taratibu tukaianza safari ya kuelekea Mbezi ya kimara huku Clara akituelekeza njia ya kuweza kufika kwao.

==>>ITAENDELEA KESHO
ad
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )