Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 14, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 52

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  
     
“Mbezi ya chini”
“Ndio ipi?”
Niliwauliza walilinzi.
“Hapo anazungumzia Mbezi ya Kimara”
“Si unapakumbuka nyumbani?”
“Ehee napakumbuka”
“Wewe na wewe ingieni kwenye gari tuelekee huko”
“Sawa mkurugenzi”
Tukaingia kwenye gari na walinzi wa kampuni yangu na taratibu tukaianza safari ya kuelekea Mbezi ya kimara huku Clara akituelekeza njia ya kuweza kufika kwao.
   
ENDELEA
“Mkurugenzi”   
Mlinzi niliye kaa naye siti  ya mbele aliniita kwa sauti ya upole, nikamuitikia huku nikimtazama usoni mwake.
“Bila ya kukuvunjia heshima, nina wazo”
“Zungumza tu”
 
“Kwa mtazamao wangu ninaona kuelekea nyumbani kwa huyu binti sio jambo sahihi, unaonaje tukaanza na taratibu za kisheria kwa mfuno kuelekea polisi, kule kuna kitengo kabisa kinashuhulika na watoto wa aina hiyo na tukitoka huko basi tutakuwa na hata nguvu ya kuelekea kwao”
Nikajifikiria kwa muda kwani wazo  hili alilo litoa huyu mlinzi  wa kampuni yangu ni zuri sana.
“Alfau kweli, sasa tunaelekea katika kituo gani cha polisi?”
“Kituo kikuu cha kati nina imani kwamba ndio kituo kizuri, wanaweza kusikiliza shida yetu”
“Sawa nielekezeni”
 
Mlinzi huyu akaanza kunielekeza njia za kupita kwa maana jiji hili la Dar es Salaam, mimi bado ni mgeni kwa baadhi ya maeneo. Tukafika katika kituo hicho, tukakaguliwa kabla  ya kuingia ndani. Baadhi ya askari walianza kuulizana mara baada ya kuniona nikiwa nimesimama kwenye moja ya foleni huku nikiwa nimemshika mkono Clara.
“Samahani kaka sogea hapa”
Askari mmoja wa kike ambaye yupo eneo la mapokezi  aliniita, taratibu tukasogea eneo alipo.
“Tuwasaidie nini?”
“Ahaa kuna swala la huyu binti hapa, kama tunaweza kuzungumza ofisini basi ningeomba msaada huo”
“Afande Mwanaidi hembu mchukue huyu kaka na mukafanye mazungumzo naye ofisini”
Afande huyu wa kike alitoa maelekezo kwa mwenzake, tukaongozana na Afande Mwanaidi hadi kwenye moja ya ofisi, akatukaribisha na tukaketi kwenye viti vilivyomo katika eneo hili. Nikanza kuelezea jinsi nilivyo kutana na mtoto huyu, kisha Mery naye akahojiwa historia ya maisha yake. Kila ambacho ytulikizungumza afande Mwanaidi alikiandika kwenye faili.
“Nisubirini”
Afande Mwanaidi alizungumza huku akinyanyuka kwenye kiti chake na tukatoka ndani ofisi hii. Baada ya muda kidogo akarejea na baba mtu  mzima mwenye kitambi kikubwa kiasi huku begani mwake akiwa na nyota kadhaa ambazo sifahamu ana cheo gani katika jeshi hili la polisi.
“Kijana kwa maelezo niliyo pewa ni kwamba umemuokota huyu binti”
“Ndio hujakosea mzee”
“Sawa. Binti unapakumbuka kwenu?”
“Ndio”
“Mwanaidi andaa askari wanne ninakuja”
“Sawa mkuu”
Afande Mwanaidi akatoka humu na kutuacha na huyu mzee.
“Naitwa Kimaro ni mkuu wa polisi kanda maalumu”
“Nashukuru  kukufahamu mzee mimi ninaitwa Ethan”
“Sura yako sio ngeni machoni mwangu. Wewe ndio yule mchezaji  wa mpira?”
“Ndio mimi”
 
“Ohoo karibu sana Tanzania”
“Nashukuru, kuna jambo jengine ambalo hatukukueleza afande aliye toka. Kuna haya makovu mgongoni mwa huyu binti hakika yameniumia sana moyo wangu”
Nilizungumza huku nikiinyanyua tisheti hii ya Clara mgongoni mwake, mkuu  wa polisi akashikwa na butwaa, kwani ni makovu makubwa sana.
“Yaani kwa uzee wangu wote huu na mambo mengi niliyo pitia katika jeshi la polisi ila sijawahi kuwa na makovu kama haya. Aisee kuna watu wanyama sana hapa duniani. Binti aliye fanya hivi ni nani?”
“Baba mdogo na mke wake”
Mlango ukafunguliwa akaingia afande Mwanaidi.
“Mkuu tayari”
“Sawa ninakuja”
 
Afande Kimaro alizungumza huku akiendelea kutazama majeraha ya Clara mgongoni ambayo kwa namna moja ama nyingine pia yalimshangaza afande Mwanaidi. Tukatoka ofisini humu, askari wakaingai kwenye gari lapo pamoja na mkuu wao nasi tukaingia kwenye gari tulilo jia na walinzi wa kampuni yangu kisha tukaanza safari ya kueleka nyumbani kwa baba mdogo wa Clara huku gari  letu likiwa limetangulia mbele. Kutokana na foleni za hapa na pale ikatuchukua lisaa zima kufika katika nyumba moja kubwa ya kifahari ambayo ina gorofa moja kwa juu. Tukashuka kwenye magari, mkuu wa polisi kanda maalumu, akatembea hadi getini, akagonda kwa muda kidogo na mlango ukafunguliwa na mlinzi wa nyumba hiyo.
 
“Bosi wako tumemkuta?”
“Nd…ioo…o”
Mlinzi alijibu kwa kigugumizi, mkuu wa polisi akaanza kuingia na askari wengien wakimfwatia kwa nyuma akiwemo askari anaye mlinda. Nami nikaingia ndani ya nyumba hii huku tukiwa nimeshika mkono Clara. Akatoka msichana mmoja mweupe kiasi huku akiwa amevalia kijisketi kifupi.
“Kuna nini kinacho endelea?”
Clara akajificha nyuma yangu mara ya msichana huyo kutazamana nasi.
“Huyo ndio ma mdogo”
“Mpigeni pingu huyo kwanza, na mume wako yupo wapi?”
“Jamani kuna nini, munanikamataje nikiwa sina kosa jamani”
Maneno ya msichana huyu hayakuwazuia askari hawa kumpiga pingu mikononi mwake. Akatoka kijana kwa kukadiria ana umri wa miaka kama thelathini hivi.
 
“Baby nini kinacho endelea?”
Alizungumza kwa sauti ya mapozi,  Clara huku machozi yakimwagika usoni mwake, akanyoosha  mkono kwa mwanaume huyu.
“Ndio baba mdogo?”
Nilimuuliza Clara huku nikimtazama usoni mwake, Clara akanijibu kwa kutingisha kichwa kwamba ndio huyo baba yake mdogo. Askari wakamkamata kijana huyu naye akapigwa pingu, askari wakawaingiza nani ya nyumba hii nasi tukaingia, hatukuamini macho yetu kukuta pakti kadhaa za madawa ya kulevya zikiwa mezani eneo  la hapa sebleni, huku misokoto ya bangi na pombe kali nazo zikiwa juu ya meza hii.
 
“Washenzi kabisa, kagueni nyumba nzima”
Mkuu wa kituo kanda maalumu  alizungumza na askari walianza kutawanyika huku wengine wakipandisha gorofani wakiwa na bunduki zao. Clara akakimbilia moja picha iliyopo pembezoni mwa meza ya tv kubwa. Akaikumbatia picha hiyo huku akiendelea kulia kwa uchungu sana, nikamsogelea na kuitazama picha hiyo na kukuta, akiwa yeye pamoja na wazazi wake baba na mama.
“Mkuu tumekuta begi hili, lina pesa za kigeni”
Askari mmoja alizungumza huku akiwa anashuka kwenye ngazi na kuelekea gorofani. Begi kubwa kiasi la mgoni likawekwa mbele ya mkuu wa polisi. Pesa za kigeni, dola za kimarekani zimejaa katika begi hili.
 
“Pumbavu hawa ni wauzaji wa madawa ya kulevya. Clara unafahamu juu ya hilo swala?”
Mkuu wa polisi alimuuliza Clara. Clara akatingisha kichwa akimaanisha kwamba ana fahamu.
“Ohoo Mungu wangu. Pigeni picha vidhibitisho vyote kisha hakikisheni kwamba hawa waalimu  wanafika kituoni”
“Sawa mkuu”
“Wewe mtoto wewe mtoto hujakomaa eheee?”
Baba mdogo wa Clara alizungumza huku akimtazama Clara kwa hasira sana. Askari mmoja akamzaba kofi zito la usoni.
“Kaa kimya, washenzi nyinyi”
 
“Nikitoka Clara nakata shingo yako hiyo, nakuapia haki ya Mungu nakata shingo yako”
“Twende bwana”
Baba mdogo wa Clara alisindikizwa na mateke ya askari walio wakamata. Wakapakizwa kwenye gari la polisi huku sisi tukibaki na mkuu wao pamoja na mlinzi wake.
“Hawa watu ni washenzi sana, kumbe chanzo cha kummpa mateso huyu binti ni kutokana na hii biashara yao”
“Hata mimi nahisi hivyo mkuu”
“Tunashukuru sana Ethan na hawa tunakwenda kuwabana na kuhakikisha kwamba wanatueleza juu ya wasambazaji wezao wa madawa ya kulevya”
 
“Sawa sawa mkuu nitashukuru sana kama mukilichukulia hatua jambo hili na kama inawezakana wakapolelee kabisa jela, kwa maana kama mulivyo msikia baba mdogo, anakiri kwamba lazima atamuua huyu binti, sasa hiyo ni hali ya kumtishia”
“Kweli, ila nitahakikisha kwamba sheria inafwata mkondo wake”
“Nashukuru, huyu binti mimi ngoja nimpeleke sehemu hivi akafanyie matibabu na usafi wa mwili wake, nitajitahidi kumuwekea wana sheria wenye uwezo mkubwa, kuhakikisha kwamba wanasimamia kesi yake na mali za wazazi wake zinarudi mikononi mwake.”
“Sawa sawa Ethan, laiti kama Tanzania tungekuwa na vijana kumi kama wewe, wenye mioyo kama yako nina imani kwamba nchi hii isinge kuwa na omba omba wengi hivi”
“Nashukuru sana mkuu”
Polisi wengine wakafika katika eneo hili, tukaaga na nikaondoka na Clara, tukiwa njiani ndani ya gari nikampigia simu Biyanka na kumueleza kila jambo lililo tokea, Biyanka akashangazwa sana na akaniomba nimpeleke Clara nyumbani kwake akapatie huduma na msichana wake wa kazi.
“Ngoja kwanza nimpeleke hospitalii, akifanyiwa huduma zote za kiafya ndio aelekee nyumbani”
“Sawa mume wangu, naona nitachelewa kurudi, si unajua mambo ya siasa haya”
“Usijali mpenzi wangu”
“Sawa baadae”
Nikakata simu na kuelekea hospitali. Nikalipa matibabu ya Ckara yoye na madaktari wakanishauri waweze kumpumzishwa kwa siku ya leo kwa maana wanahitaji kumuongezea maji mwilini pamoja na damu  kwani afya yake ime dhohofika sana. Nikakubaliana na madaktari hawa huku nikiahidi kwamba nitarudi siku inayo fwata ili nimjulie hali kisha nikaanza safari ya kuelekea hotelini kujipumzisha.
                                                                                                               ***
Asubuhi na mapema nikaelekea hospitalini na kukuta hali ya Clara ikiendelea vizuri sana.
“Naamini akikaa hapa kwa siku ya leo, kesho basi tunaweza kumruhusu”
Daktari niliye muaachia jukumu la kumtazama alizungumza huku tukiwa tumesimama pembezoni mwa kitanda cha Clara.
“Je vipimo vingine vipo vizuri”
“Ndio, ila ana Malaria pamoja na UTI ila magonjwa yote hayo tumesha anza kumpatia dozi kwa kumchoma sindao na kesho atamalizia sindano hizo”
“Clara unajisikiaje?”
“Safi tu Ethan, nashukuru kwa msaada wako”
Clara alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
 
“Ohoo usilie mtoto mzuri, ni jukumu langu kuhakikisha kwamba unakuwa salama, sawa”
“Sawa”
Simu yangu ikaanza kuita, nikaitoa mfukoni na kukuta ni Biyanka ndio anaye nipigia. Nikatoka nje ya chumba hichi ili niweze kuzungumza naye.
“Umeamkaje mume wangu”
“Salama, vipi wewe”
“Safi upo hoteli au?”
“Hapana nipo hospitalini hivi sasa, nimekuja kumtazama mtoto”
“Ohoo anaendeleaje?”
“Yupo vizuri”
“Sawa, ila samahani mume wangu, leo hatuto weza onana kwa sababu, tutatakiwa kwenda Mwanza na mama kuna wanawake wengine anakwenda kuonana nao hivyo tunaweza kurudi usiku na ndege au tukarudi kesho asubuhi.”
“Ohoo sawa, ila kuwa makini”
 
“Usijali mume wangu, nipo makini sana katika kila hatua ya maisha ninayo ipiga”
“Sawa mimi nitashinda hapa na huyu binti kisha nitakwenda kazini mara moja. Tutawasiliana”
“Sawa mume wangu, nakupenda sana”
“Ninakupenda pia mke wangu”
Biyanka akakata simu na nikairudisha mfukoni mwangu, nikarudi chumbani humu na kujikuta nikiwa nimejawa na mshaongo kwa maana dokta nimemkuta akiwa amelala chini huku damu nyingi zikiwa zinamwagika shingoni mwake na Clara akiwa hayumo ndani ya chumba hichi huku dirisha  moja la chumba hichi likiwa lipo wazi jambo lililo nipa ishara kwamba kuna jambo  la hatari lililo tokea katika eneo hili.

==>>ITAENDELEA KESHO
ad
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )