Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, January 15, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 53

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  
         
“Ohoo anaendeleaje?”
“Yupo vizuri”
“Sawa, ila samahani mume wangu, leo hatuto weza onana kwa sababu, tutatakiwa kwenda Mwanza na mama kuna wanawake wengine anakwenda kuonana nao hivyo tunaweza kurudi usiku na ndege au tukarudi kesho asubuhi.”
“Ohoo sawa, ila kuwa makini”
“Usijali mume wangu, nipo makini sana katika kila hatua ya maisha ninayo ipiga”
“Sawa mimi nitashinda hapa na huyu binti kisha nitakwenda kazini mara moja. Tutawasiliana”
“Sawa mume wangu, nakupenda sana”
“Ninakupenda pia mke wangu”
Biyanka akakata simu na nikairudisha mfukoni mwangu, nikarudi chumbani humu na kujikuta nikiwa nimejawa na mshaongo kwa maana dokta nimemkuta akiwa amelala chini huku damu nyingi zikiwa zinamwagika shingoni mwake na Clara akiwa hayumo ndani ya chumba hichi huku dirisha  moja la chumba hichi likiwa lipo wazi jambo lililo nipa ishara kwamba kuna jambo  la hatari lililo tokea katika eneo hili.
   
ENDELEA
Nikatoka chumbani humu kwa haraka na kuwaita madaktari wawili waliopo kwenye kordo. Nikaingia nao ndani ya chumba hichi na wakastuka sana kumkuta mwezao akiwa yupo chini katika hali mbaya sana.
 
“Nini kimetokea?”
“Mimi pia sifahamu ila kuna watu wamefanya hivi na wamamteka mgonjwa wangu”
Nilizungumza huku nikitazama dirisha la chumba hichi lililo achwa wazi, kwa haraka nikaruka dirishani humu na kuanza kukimbia huku nikiangaza macho yangu huku na huku ili niweze kumuona Clara ni wapi alipo pelekwa. 

Nikawaona wanaume wawili wakiingia kwenye gari ndogo aina ya Toyota Alteza huku wakiwa wamevalia nguo nyeusi. Nikakimbilia eneo la maegesho ya magari na kuingia kwenye gari langu, nikaliwasha na kuanza kufukuzia gari hii ndogo huku nikiamini moja kwa moja watu hawa ndio walio mteka Clara na ndio watu ambao wamefanya shambulizi kwa daktari. Uwezo wa gari yangu BMW X6 ni mkubwa kuliko hata Toyota Alteza, haikuwa kazi ngumu kwangu kuweza kuwakaribia. 

Ila nikajikuta nikifunga breki za gafla mara baada ya jama mmoja kujichomoza ndani ya gari hili huku akiwa amekaa siti ya nyuma na akaanza kunishambulia kwa risasi ambazo cha kumshukuru Mungu kioo cha mbele cha gari langu hakiingizi risasi kirahisi.
 
“Fuc***”
Nilizungumza huku nikianza kuendelea kulifukuzia gari hili pasipo kukata tamaa. Baada ya kutambua ubora wa gari yangu katika kuingiza risasi nikazidi kuongeza mwendo kasi hadi nikaanza kuligonga gari la watekaji hawa kwa nyuma. Kila jinsi nilivyo ligonga gari la watekaji hawa ndivyo jinsi nilivyo zidi kuwayumbisha na kwa mara kadhaa walijikuta wakitoka nje ya barabara. 

Nikaanza kusikia ving’ora vya gari  za polisi vikitufwata kwa nyuma, hapa ndipo nikapata matumaini kwani sina silaha yoyote ambayo ningeweza kupambana na hawa watekaji. Nikaongeza mwendo, kisha nikaligonga gari  hili kwa pembeni na kumfanya dereva kupoteza muelekeo wa gari lake na likaanza kuzunguka na kuyumba na mwishowe likaparamia moja ya nguzo za taa za barabarani na kutulia kimya. 

Ndani ya sekunde kadhaa askari wakafika katika eneo hili huku wakituamrisha watu wote kushuka kwenye gari huku mikono yetu ikiwa juu. Nikatii amri, nikashuka kwenye gari huku mikono yangu ikiwa ipo hewani. Mtekaji mmoja akajifanya anahitaji kuwashambulia askari ila akawahiwa kwa kupigwa risasi nne za kifuani na kufa hapo hapo.
“Wamemteka rafiki yangu, yumo ndani ya gari hilo”
Nilizungumza kwa kujiamini huku nikiwatazama askari hawa wanao nipapasa mwili wangu ili waweze kufahamu kama nina silaha au laa.
 
“Sina chochote”
Nilimuambia askari huyu mara baada ya kumuona akinipapasa sana pasipo mafanikio ya aina yoyote.
“Kuna binti mdogo ndani ya hilo gari mtoeni bwana”
Askari wawili wakalisogelea gari hilo kwa umakini wa hali ya juu, wakafungua mlango wa sti ya nyuma kama vile nilivyo waeleza ndivyo jisni walivyo mkuta Clara akiwa amelazwa kwenye siti.
“Nahitaji kumuona huyo binti”
“Wewe ni nani yake?”
“Mimi ni kaka yake”
Ilinibidi kuongopea ndipo polisi walipo niruhusu kushusha mikono yangu chini. Wakamtoa Clara kwenye gari hilo, kitu kilocho niogopesha ni ukimya wa Clara, hatikisiki wala hapumui.
 
”Ohoo Mungu wangu inabidi tumuwahishe hospitalini”
Gari kadhaa za polisi nazo zikafika katika eneo hili, nikamuona mkuu wa polisi kanda maalumu bwana Kimaro naye akishuka kwenye moja ya gari. Moja kwa moja akafika hadi sehemu nilipo simama, hakuamini kumuoana Clara akiwa eneo hili akipatiwa huduma ya kwanza na maaskari hawa.
“Ethan nini tena kimetokea?”
“Walimteka hospitalini, nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kwamba nina mkomboa na kweli Mungu amesaidia tumempata”
 
“Ohoo Mungu wangu. Afande vipi hali yake?”
“Mapigo yake ya moyo yanadunda vizuri, wamemchoma sindano ya usingizi”
“Muingizeni ndani ya gari na mumpeleke hospitali na ulinzi mkali sana uimarishwe”
“Sawa mkuu”
“Na kule hospitalini wamfanya shambulio la daktari aliye kuwa akimuhudumia Clara”
“Hali yake vipi?”
“Wakimuahi wezake atapona ila wakichelewa basi anaweza kupoteza maisha”
“Mmmm….hapa kuna mtandao mkubwa sana Ethan, nawe ingia kwenye gari tuelekee hospitalini”
“Sawa, hii gari yangu siwezi kutembea nayo, tazama ilivyo pondeka pondeka”
“Nitaagiza askari walichukue na kulipeleka kituoni, kuna maelezo utatoa kisha nitakuelekeza ni gereji gani nzuri hapa jijini Dar es Salaam unaweza kuitumia kwa kulitengeneza gari lako”
 
“Nashukuru mzee”
Tukaingia kwenye gari la mkuu  huyo wa polisi kanda maalumu na kuondoka eneo hili. Tukafika hospitali nyingine niliyo fanikiwa kusoma bango lake lililo andikwa Agakhan Hospital. Clara akawahishwa kwenye chumba cha matibabu, mimi na mkuu huyu wa polisi tukabaki nje ili kusubiria majibu ya madaktari. Baada ya dakika kama ishirini hivi, daktari mwana mama mwenye asili ya kihindi akatoka katika chumba alicho ingizwa Clara, akatusalimia huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake.
 
“Hali ya mgonjwa inaendelea vizuri, sindano aliyo chomwa kidogo haito kuwa na madhara makubwa sana zaidi ya kulala kwa masaa kadhaa”
“Tunashukuru sana daktari ila kule tulipo toka niliambia kwamba ana Malaria pamoja na UTI, na vyoye alisha anzishiwa dozi”
“Hili nimelizingatia pia, usiwe na shaka kila jambo litakwenda sasa sawa na mpango unao hitaji kijana”
“Nashukuru sana daktari. Je anatarajia kuamka baada ya muda gani?”
 
“Masaa matano au sita kutoka hivi sasa”
“Sawa, nitaacha vijana wangu wawili hapa watamlinda binti huyo. Ninakuomba muweze kuwapatia ushirikiano mkubwa kwa maana huyo binti hadi tumemleta hapa alitekwa kwenye hospitali iliyo pia na binti huyo ni muhimu sana kuweza kuakamata wahalifu ambao tunawatafuta ndio maana wanajitahidi kumteka teka sawa daktari”
“Usijali kamanda, nikuhakikishie mgonjwa wako atakuwa salama hadi pale utakapo rejea”
 
“Sawa, ila sura hizi mbili, mimi na huyu bwana mdogo hapa ndio watu wa pekee ambao turuhusiwe kuingia ndani ya wodi hiyo, isije akatoke mti mwengine kutoka wasipo eleweka aseme amekuja kumuangalia mgonjwa musimrihusu sawa”
“Nimekuelewa kamanda na nitahakikisha hilo linazingatiwa na mimi nitajitahidi kwamba niwe ni daktari ambaye nitamuhudumia hadi hili jambo litakapo kwisha”
“Nashukuru sana. Ethan tueleke kituoni”
“Sawa”
Tukaondoka eneo hili la hospitali na tukaianza safari ya kuelekea kituo kikuu cha polisi. Tukafika katika eneo hilo na nikaikuta gari yangu ikiwa imeegeshwa kwenye mageesho ya magari yaloyo kamatwa na askari. Tukapitiliza moja kwa moja hadi ofisi kwa mkuu huyu.
 
“Kesi ya huyu msichana tumeanza kuifanyia uchunguzi. Pale mwanzo tuliitazama kwa macho ya kawaida na tukahisi kwamba ni ndogo, ila ni kesi kubwa sana ambayo imehusisha baadhi ya mabosi wangu, yaani hapa muda wowote na saa yoyote basi naweza kupigiwa simu ya kuwaachia wale watuhumiwa”
Bwana Kimaro alizungumza kwa suati ya upole na iliyo kata tamaa kabisa.
“Imekuwaje kubwa kiasi hicho?”
“Yaani…ila bado tupo kwenye upelelezi, ila ninacho taka kukuambia tu kama kijana wangu kuwa makini, kwa maana sasa umesha anza kuonekana kuwa kikwazo kwao tena kwa jambo hili la leo ni lazima watakuwa wanakuwinda.”
 
“Nchi hii inaongozwa vipi mkuu?”
“Mwanangu nchi hii wewe ione kwa nje, ila ukifukunua mambo ya ndani unaweza ukalipuka. Ila siwezi kukuambia mambo mengi sana kwa maana mambo mengine ni ya kipolisi. Ila nimekupa tahadhari kuwa makini”
“Usijali nipo makini mkuu”
“Sawa, nitakupa kijana wangu mmoja, atakupeleka kwenye gereji moja ya Wahindi ni wataalamu sana wa kutengeneza hayo magari yenu ya kifahari”
Bwana Kimaro alizungumza huku akinyanyua mkonga wa simu iliyo mezani kwake na kuminya batani kadhaa kisha akaweka mkonga huo sikioni mwake.
 
“Njoo ofisini kwangu”
Bwana Kimaro baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akaurudisha mkonga huu wa simu sehemu alipo utoa. Akaingia askari mmoja marefu na mweusi sana.
“Afande Nyasesa, huyu ni Ethan. Ethan huyo ni afanye Nyasesa”
“Nashukuru kukufahamu”
Afande Nyasesa alizungumza huku akinikabidhi mkono wake wa kulia. Tukapeana mikono huku akinitazama usoni mwangu.
“Mpeleke Ethan kwenye ile gereji ya Wahindi niliyo peleka ile V8”
 
“Sawa mkuu
“Ethan kumbuka nilicho kueleza mwanangu.”
“Nitayafanyia kazi, alafu sijapata namba yako ya simu”
“Ohoo lete simu  yako nikuandikie”
Tukapeana namba zetu za simu na mkuu huyu wa polisi. Tukatoka nje na kuingia kwenye gari langu na taratibu tukaanza kuondoka katika eneo hili. Afande Nyasesa akanielekeza hadi ilipo gereji hiyo, tukapokelewa na mzee mmoja wa kihindi. Alipo muona afanye Nyasesa akasalimiana naye kwa furaha sana.
“Aisee muna shida sana nyinyi watu”
Mzee huyu wa Kihindi alizungumza huku akitazama gari langu jinsi lilivyo shambuliwa kwa risasi.
“Hiyo ndio maana ya kuwa askari mzee”
“Kweli ehee nawasikiliza”
“Ethna mzee huyu anaitwa Barachuna”
“Nashukuru, mzee nahitaji gari langu lirudi kwenye upya ni kiasi gani na itachukua muda gani?”
“Ahaa……!!! Itagarimu kama milioni kumi na mbili hivi na itagarimu siku tatu”
 
“Sawa ninaweza kulipia hivi sasa?”
“Ndio hakuna tatizo katika hilo”
Mzee Barachuna akaniingiza ofisini kwake, nikamuhamishia pesa kutoka kwenye benki akaunti yangu na kuingia kwenye akauti yake ya benki.
“Unaitwa Ethan nani?”
Mzee Barachuna aliniuliza huku akiandika risiti ya malipo niliyo yafanya.
“Klopp”
Nilijibu huku nikitazama tazama baadhi ya magari mapya yaliyomo katika jengo hili.
 
“Hizi gari mpya zinauzwa?”
“Ndio zipo zinazo uzwa na zipo zinazo kodishwa”
“Nahitaji ya kuuzwa kabisa, ila mpya”
“Gari gani?”
“Rang Rover Voge au Sport”
“Umepata kijana”
Mzee huyu alizungumza huku akitabsamu. Tukatoka ofisi kwake na kuzunguka eneo la nyuma la jengo hili, nikakuta magari mengi ya kifahari yakiwa yamewekwa katika eneo moja zuri. Nikatazama magari yote na nikapenda Range Rover moja yenye rangi nyeusi.
 
“Ile pale ni milioni ngapi?”
“Ni dola laki mbili na hamsini, ila kutokana umekuwa mteja wetu basi tutakupa punguzo kidogo hadi dola laki mbili na ishirini”
“Nahitaji nilikague gari kwanza”
Mzee Barachuna akakubali niweze kuingia ndani ya gari hili, kusema kweli nimelipenda hili gari.
 
“Pia unaweza kulijaribu”
“Hapana, nitalijaribia barabarani. Malipo nitayafanya kwa nje ile ile”
“Hakuna tatizo”
Nikafanya malipo kwa njia ya kuhamisha kiasi hicho cha pesa kuingia katika akaunti ya bwana Barachuna. Bwana Barachuna alipo pewa ripoti na benki kwamba kiasi hicho kimeingia, akanikabidhi funguo, kadi ya gari, tukaandikishiana kila kitu kinacho takiwa kufanyika katika manunuzi ya magari. Simu yangu ikaanza kuita, nikaitoa mfukoni na kukuta namba ngeni kidogo, nikajifikria kwa muda kidogo kisha niaipokea.
“Haloo mkurugenzi”
Niliisikia sauti ya kike ambayo moja kwa moja iliweza kunikumbusha wasicha ambao nilipatia kadi yangu ya biasha na niliweka ahadi nao ya kukutana leo.
 
“Ndio habari”
“Salama naamini umenikumbuka”
“Yaa si wale tulio kutana jana kwenye kordo?”
“Ndio mkurugenzi, mupo wapi?”
“Tupo Mwenge ndio tumetoka saluni, tumesha jiandaa”
“Barachuna mwenge ni wapi?”
Nilimuuliza mzee huyu huku nikiwa nimeizima simu yangu ili wasiweze kunisikia.
“Ukitoka nyoosha barabara hii moja kwa moja hadi utakapo kutana na taa za barabarani basi hapo ndio Mwenge”
 
“Nashukuru”
Nikaingia ndani ya gari langu mara baada ya kumaliza kufungwa plate namba, nikaagana na bwana Barachuna na nikainza safari ya kuelekea Mwenge huku nikiwa na gari langu jipya kabisa ambalo tayari limesajiliwa kila kitu. Nikafika Mwenge na nikasimama kwenye moja ya sheli, kisha nikawapigia wasichana hawa na kuwaelekeza sehemu nilipo simamisha gari langu.  Baada ya dakika tatu hivi nikawaona wakifika katika eneo hili, nikafungua loki za milango ya gari langu na wakaweza kufungua milango na kuingia ndani.
 
“Mumependeza”
Niliwasifia huku nikiwatazama jinsi walivyo pendaza.
“Asante mkurugenzi”
“Hivi tunavyo kwenda huku kuna benki?”
“Ndio zipo”
“Sawa, sasa mmoja si angekuja kukaa hapa mbele ili anielekeze njia, si munajua kwamba hapa Dar es Salaam mimi ni mgeni.
 
“Sawa, Queen nenda”
Msichana aliye elezwa na mwenzake, akashuka kwenye gari na kuzunguka upande wa pili wa gari hili, akaifunagua mlango wa siti ya mbele kisha taratibu tukaanza kuondoka katika eneo hili. 

Tukafika katika moja ya jengo lenye baadhi ya benki na huduma kadhaa za kipesa, nikashuka kwenye gari nikiwa na kadi yangu, ya benki inayo niruhusu kuweza kutoa pesa kwenye benki zaidi ya mia moja duniani. Nikatoa kiasi cha dola elfu ishirini, dola elfu tano nikazibadilisha katika pesa za kitanzani kisha nikarudi kwenye gari. Ujumbe mfupi wa meseji ukaingia kwenye simu yangu na kujikuta nikiziweka hizi bahasha mbili zenye pesa pembeni yangu na kuitoa simu mfukoni. Nikaufungua ujumbe huu uambao umetumwa na namba ngeni. 
 
‘ULIPO PAGUSA SIO SALAMA KABISA ETHAN. NITAHAKIKISHA NINAKUUA KABLA YA SIKU YA LEO HAIJAISHA. PUMBAVU SANA WEWE’
Meseji hii ikanistua sana hadi mwili mzima ukaanza kunitetemeka na jasho taratibu likaanza kunimwagika usoni mwangu hadi Queen na mwenzake wakagundua kwamba kuna tatizo lililo nipata.

==>>ITAENDELEA KESHO
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )