Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, January 16, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 54

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA
Tukafika katika moja ya jengo lenye baadhi ya benki na huduma kadhaa za kipesa, nikashuka kwenye gari nikiwa na kadi yangu, ya benki inayo niruhusu kuweza kutoa pesa kwenye benki zaidi ya mia moja duniani. Nikatoa kiasi cha dola elfu ishirini, dola elfu tano nikazibadilisha katika pesa za kitanzani kisha nikarudi kwenye gari. Ujumbe mfupi wa meseji ukaingia kwenye simu yangu na kujikuta nikiziweka hizi bahasha mbili zenye pesa pembeni yangu na kuitoa simu mfukoni. Nikaufungua ujumbe huu uambao umetumwa na namba ngeni.
‘ULIPO PAGUSA SIO SALAMA KABISA ETHAN. NITAHAKIKISHA NINAKUUA KABLA YA SIKU YA LEO HAIJAISHA. PUMBAVU SANA WEWE’
Meseji hii ikanistua sana hadi mwili mzima ukaanza kunitetemeka na jasho taratibu likaanza kunimwagika usoni mwangu hadi Queen na mwenzake wakagundua kwamba kuna tatizo lililo nipata.

ENDELEA   
“Mkurugenzi kuna tatizo gani?”
Qeen aliniuliza huku akinitazama jinsi mikono inavyo nitetemeka hadi kushika simu yangu nina shindwa.
“Unaweza kuendesha gari?”
“Ndio”
“Njoo uendeshe”
Nilizungumza huku nikiwa nimeishiwa hata ujasiri wa kuendesha gari hili. Nikahamia siti ya pembeni huku Qeen akiingia kwenye siti ya dereva.
“Tunaelekea wapi mkurigenzi”
“Kule kule”
 
Taratibu tukaanza kuondoka eneo hili huku kichwani mwangu nikiwa na mawazo mengi sana juu ya huu ujumbe nilio tumiwa. Nikaitafuta namba ya afande Kimaro na kumpigia simu, simu yake ikaita kidogo na ikapokelewa.
“Ethan nitakupigia nipo kwenye kikao”
Simu ikakatwa na kunifanya nishushe pumzi nyingi sana. Ukimya ukatawala ndani ya gari huku nikifirikia nimueleze Dany juu ya ujumbe huu, ila nikaona itakuwa sio sahihi, acha nipambane mwenyewe hadi dakika ya mwisho isitoshe yupo Ethan, rafiki yangu anaye nisaidia katika hali zote ngumu ninazo zipitia.
“Mkurugenzi tumesha fika Bagamoyo, sasa unahitaji twende kwenye hoteli gani?”
 
“Hoteli yenye hadhi kubwa ambayo haina watu wengi na wanao ingia hapo ni matajiri tu”
Qeen akatazamana na mwenzake.
“Unanitazama nini Qeen mimi sijiu hoteli nzuri za huko”
“Ila wewe si viwanja vyako?”
“Bwana Qeen mimi sijui”
“Labda twende pale Ocenic Bay Hotel”
“Haina watu wengi?”
“Hapana watu ni wacheche mkurugenzi”
“Sawa twendeni”
Tukafika katika hoteli hii kubwa, Qeen akasimamisha gari katika maegesho maalumu. Nikatazama eneo hili na kweli lime tulia na watu wengi hapa kidogo ni wazungu wazungu ambao kwa namna moja ama nyingine nina imani kwamba wananitambua.
“Nenda kachukue chumba kimoja chenye hadhi kubwa”
“Kimoja!!?”
Qeen aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao.
“Ndio”
“Sawa mkurugenzi”
“Mupende kuniita Ethan nikiwa nje ya ofisi”
“Saw sawa”
Nikamkabidhi Qeen kiasi cha kutosha cha pesa kisha akashuka kwenye gari na kuelekea eneo la mapokezi. Nikabaki na rafiki yake ambaye sio muongeaji sana.
“Hivi unaitwa nani wewe?”
“Latifa”
“Ahaa, mwenzako ni Qeen na wewe ni Latifa?”
“Ehee?”
“Muna muda gani katika kampuni yangu pale?”
“Huu ni mwaka wa pili mkuu”
“Ahaa, kati ya uongozi ulio pita na uongozi huu, upi ni ongozi mzuri?”
 
“Wa kwako kwa kweli, kwa maana unajua kuwajali wafanyakazi wako. Yule mkurugenzi aliye toka alikuwa anajali wale viongozi wa ngazi za juu hususani ma meneja wale. Ila sisi wa chini huku tulikuwa tunafanya kazi hiyo basi kwa maana hatuna pa kwenda na hapa ni mjini ukiacha kazi ni kazi kupata kazi”
“Poleni sana”
“Tumesha poa, kwa sasa kidogo tunaweza hata kuingia saloon hata mara mbili kwa wiki, ila zamani. Kwa wiki mbili una ingia mara moja, tena sisi tunao hudumia wateja tunatakiwa kuwa safi muda wote ila wala hawakuwa wanatujali, hakuna marupu rupu, yaani tulipitia mtoso mkubwa sana mkurugenzi”
 
Tukamuona Qeen akija eneo la gari na ikabidi mazungumzo yaishie hapa. Akafungua mlango na kuingia ndani ya gari.
“Nimepata vip room moja ni dola mia moja na hamsini”
“Umechukua?”
“Ndio mkuu”
“Ni gorofa lipi?”
“Lile pale”
Qeen alituonyesha moja ya gorofa, kwa maana katika eneo hili kuna gorofa kadhaa.
“Basi tangulieni nina kuja”
“Sawa”
Qeen na Latifa wakashuka kwenye gari hili,kabla hawajafika mbali nami, simu yangu ikaanza kuita na kukuta ni namba ya Biyanka. Nikaitazama simu yake kwa muda kisha nikaipoke na kuiweka sikioni.
 
“Mume wangu za muda?”
“Safi vipi?”
“Poa upo wapi?”
“Ahaa nipo sehemu nina pata lunch”
“Ahaa, kuna mtu ameniambia amekuona polisi leo ni kweli kwa maana nilimbishia”
“Hapana sio mimi”
“Amesema pia ameona gari lako polisi”
“Ni nani?”
“Rafiki yangu mmoja hivi?”
“Hapana atakuwa amenifanisha, mimi polisi ninakwenda kufanya nini sasa?”
Ilinibidi niongopee ili kuficha udadisi wa Biyanka.
“Ndio hapo sasa, sawa, sisi tunajianda kuingia kwenye mkutano na mama”
“Sawa”
“Nakupenda mume wangu, nakuomba uwe makini”
“Nashukuru, nakupenda pia”
 
Nilizungumza hiyo basi ili kumridhisha, akakata simu, kabla sijairudisha mfukoni nikaupitia ujumbe huu nilio tishiwa maisha yangu. Nikafungua kisanduku kidogo cha kuhifadhia vitu ndani ya hili gari nikaiingiza kiasi cha pesa na nikashuka na kiasi cha kutosha cha pesa za kitanzania mbazo zipo kwenye mfuko huu wa kaki, nikafunga mlango wa gari langu kwa funguo na kuelekea walipo elekea Qeen na Latifa. Nikafika katika chumba alicho niambia, nikagonga kidogo na mlango ukafunguliwa na Qeen. Nikapitiliza moja kwa moja hadi kitandani na kijitupa na wote wakabaki wakinitazama.
 
“Agizeni vyakula na vinywaji”
“Unatumia chakula gani mkuu”
“Chochote mutakacho kula nyinyi. Alafu Latifa usipende kuniita mkuu tunapo kuwa eneo kama hili. Niiteni Ethan tu nitajisikia vizuri”
“Samahani Ethan nilijisahau”
“Je kinywaji unatumia kinywaji gani?”
“Kichwa changu leo hakipo vizuri hivyo nahitaji ninywe wnye hadi nitakapo jisikia vizuri”
Qeen na Latifa wakatazamana.
“Mimi nitakwenda”
Latifa alizungumza, nikamuonyesha bahasha yenye pesa na kumuagiza achukue kiasia nacho kihitaji kwa kwenda kununulia vyakula na vinywaji.
“Ethan unaonekana una mawazo sana boss wangu, hembu niambie ni kitu gania mbacho kina endelea kwako?”
Qeen aliniuliza swali hili mara baada ya Latifa kutoka chumbani humu, nikakaa kimya kwa muda huku nikimtazama usoni mwake.
 
“Niambie tu unaweza kuniamini”
“Kuna mtu anahitaji kuniua leo”
Qeen akastuka huku akiushika mdomo wake kwa kushangaa sana. Nikamuona naye akianza kujawa na woga fulani.
“Kwa nini?”
“Kwenye maswala ya kibiashara kuna mambo mengi ila potezea naamini kwamba hato weza kufanya jambo hilo ndio maana nime amua kuja kukaa huku Bagamoyo kwa muda kidogo hadi hili jotojoto litakapo pita.
 
“Jamani, wasije wakatuulia mkurugenzi wetu na maisha yakabadilika kwetu jamani”
“Usijalia hakuna kitu kama hicho. Nikuulize swali?”
“Niulize tu”
“Wewe na Latifa muna urafiki wa muda gani?”
“Mmmm toka tupo chuo IFM hadi mwaka huu tunatimiza mwaka wa tano kama sikosei”
“Na muna ambiana sana mambo yenu ya siri?”
“Ndio, siri yake siri yangu. Hatufichani jambo lolote”
“Sawa”
Latifa akarudi na kukaa kwenye moja ya sofa.
“Ninaweza kuwaamini?”
Latifa na Qeen wakatazamana kwa sekundee kadhaa, kisha latifa akwahi kujibu kabla ya Qeen
“Ndio Ethan kwa maana mimi na Qeen tuna amainiana kwa kipindi kirefu sana, hatujawahi kukorofishana wala kutoleana siri kwenye maisha yetu”
“Ohoo sawa sawa nimewaelewa. Sasa nahitaji muwe ni wapelelezi wangu wakubwa na muweze kufanya kazi moja hatari sana ambayo kwa nama moja ama nyingine inaweza kuhatarisha maisha yenu. Ndio maana nimewaita mazunngumzo haya tuje kuyazugumzie nje ya Dar es Salaam”
 
Qeen na Latifa wakawa wanyonge kiasi huku kila mmoja akionekana kutafakari juu ya jambo ambalo ninalizungumza.
“Najua nyinyi bado ni mabinti wadogo  kama mimi. Bado munatafuta maisha kwa udi na uvumba ila kwa maisha ya Tanzania nina imani kwamba hakuna ambaye anaweza kutusua na kuwa tajiri kwa mshahara wa kupangiwa na bosi wako si ndio”
 
“Ni kweli Ethan”
Qeen alijibu kwa unyonge sana.
“Kazi ambayo mutaifanya sio ya muda mrefu ila nitawapatia pesa nyingi sana pale ambapo wote kwa pamoja tuta fanikisha kuhakikisha lie ambalo nimelikusudia limekalimilika. Hivyo basi nahitaji kujua mupa tayari au hamupo tayari katika kuifanya hii kazi, na sijawatajia kazi gani kwa maana nina hitaji kuona muitikio wenu, kwa maana usije ukasema nitafanya kazi kutokana kwa kiasi cha pesa ambacho labda nitakitaja au kwa sababu tu unamfanyia Ethan, tahadhari kazi inahitaji usiri, kazi inahatarisha maisha, kazi inahitaji umakini. Sasa kazi ni kwenu”
Qeen akashusha pumzi nyingi sana huku  akimtazama Latifa usoni mwake, ambaye naye anaonekana kuwajawa na wasiwasi mwingi sana. Ukimya ukatawala ndani ya chumba hichi huku wote wawili wakiwa wanatafakari sana kwa hichi nilicho waeleza.
“Mimi nipo tayari japo sifhamu ni kazi gani ila nipo tayari Ethan”
 
Latifa alizungumza kwa ujasiri ambao kwa namna moja ama nyingine ukanifurahisha.
“Nami nipo tayari, nitapambana bega kwa bega hadi kuhakikisha kwamba lile ambalo unatueleza linakwenda kukamilika Ethan”
Maneno ya Qeen nayo yakanipa furaha na hamasa ya kuwaamini japo si kwa asilimia mia moja.
“Nafurahi kusikia hivyo, ila jambo kubwa na la umakini sana ni kutunza siri, kama mutashindwa kutunza siria, hakika mpango mzima unakwenda kuvunjika na ukivunjika. Mimi na nyinyi kila mmoja atakwenda kuuwawa kwa wakati wake”
“Tuamini Ethan hata mama zetu hatuto kwenda kuwaeleza hili jambo”
 
“Nashukuru. Mimi nipo Tanania kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa adui aliye niulia wazazi wangu kipindi cha miaka mingi sana iliyo pita. Nimenunua ile kampuni ili mradi niwe karibu tu na adui yangu. Hadi kwa sasa hivi nina shukuru Mungu ni kwamba nimesogelea kwa asilimia takribani stini. Asilimia arobaini zilizo salia nina hitaji kumuangamiza kutokea nje kabisa na ninahitaji anguko lake liwe anguko la taifa kwa maana halito mgusa mtu mmoja, litawagusa watu wengi sana”
 
Nilizungumza kwa mafumbo kidogo ili kuendelea kuwajua Qeen na Latifa kama akili zao zipo vizuri au ni za aabu ajabu.
“Anguko la taifa, una maanisha mtu huyo ni kiongozi au?”
Qeen aliniuliza huku akinikazia macho.
“Si kiongozi ila anatarajiwa kuwa kiongozi”
“Ahaa nahisi hilo swala litakuwa linahusiana na wanao gombani urahisi si ndio bosi”
Latifa aliniuliza, nikamtazama kwa sekunde kadhaa kisha nikatingisha kichwa nikimaanisha kwamba alicho kizungumza yeye ni sahihi kabisa.
“Duu, hilo jambo kweli ni gumu”
“Ndio maana ninazidi kuwa sisitizia kwamba linahitaji kila mmoja wenu kuwa makini na msiri. Ukiropoka hata kwa boyfriend wako basi ujuje unakwenda kufa”
“Sote hapa hatuna wanaume”
“Kweli?”
“Ndio Ethan tuamini”
 
“Sawa, kwa leo mazungumzo yaishie hapa, ili kila mmoja aweze kujiandaa kisaikolojia kuweza kumpokea huyo mtu ambaye tunakwenda kumshuhulikia. Ninawahakikishia enepo tutafanikiwa basi kila mmoja wenu ninakwenda kumpa kiasi cha dola za Marekani milioni tano na nina uhakika kwamba mutakuwa matajiri wakubwa na nyinyi mutafungua kampuni zenu ndogo ndogo kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi zaidi”
Qeen na Latifa wakwa kama watu walio changanyikiwa wakaanza kuruka ruka huku wakikumbatia kwa furaha sana, jambo lililo nifanya nicheke kidogo.
“Boss tunakuhakikishia kwamba tutafanya lolote utakalo tuamrisha tufanye. Haki ya Mungu ni lazima tumuangamize yule unaye hitaji kumlipizia kisasi”
Qeen alizungumza kwa furaha sana.
“Mimi nipo tayari hata kufa ili mradi huu mpango uweze kukamilika.
 
“Nafuraha kuweza kusikia hivi. Mbona wanachelewa kutuletea chakula na viywaji”
“Kidogo kulikuwa na foleni ila watatuletea chakula humu ndani”
“Sawa, hivi kila mtu anaishi kwake au?”
“Tumepanga nyumba moja, kila mmoja ana cheke, ila tuna seble moja”
“Basi mpango ukiisha, mutaniambia ni wapi munahitaji kuishi kama ni kuwajengea niwajengee kila mmoja nyumba yake na kama ni kununua basi kila mmoja niwanunulie nyumba yake, hiyo ni nje tu ya kiasi cha pesa ambayo nimewaabia nitakwenda kuwalipa na nilazima tuweze kuandikishana mikataba ya siri ambayo ni sisi watatu tu ndio tutakuwa tunafahamu juu ya mikataba hiyo. Mumenielewa?”
Furaha ikazidi kutawala kwa Qeen na Latifa. Muhudumu akatuletea vijwaji na chakula. Simu yangu ikaanza kuita, nikaitazama na kukuta ni namba ya Afande Kimaro, nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
 
“Ndio Ethan”
“Kuna meseji na namba nitakutumia, nina omba uweze kuniwekea ulinzi mkuu”
“Sawa nitumie”
“Kitu kingine ninaomba umtazame Clara hapo hospitali nitaonana naye kesho”
“Sawa sawa”
Nikakata simu na kumtumia meseji ya vitisho niliyo tumiwa na mtu nisiye mfuamu, nikaituma na namba yake ya simu kisha tukaendelea kupata chakula hichi cha mchana huku tukiendelea kufakamia wyne zilizo letwa hapa. 
 
“Ethan kuna zawadi na kazi ambayo na sisi tuna hitaji utusaidie kuifanya”
Qeen alizungumza kwa sauti nyororo huku macho yakiwa yamemlegea kwa pombe nyingi aliyo kunywa, wakasimama na kunishika mikono yangu, nikatembea nao hatua chache hadi kitandani, kisha wakanisukumia kitandani, wakatazamana kisha wakacheka kidogo. Taratibu wakaanza kun ndimi zao huku wakianza kuvuana nguo zao jambo lililo nishangaza sana na kunitamanisha sana kihisia na kunifanya nipate msisimko mkali sana wakimahaba hadi nami nikajikuta nikianza kuvua 

==>ITAENDELEA KESHO
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )