Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, January 24, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 59

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA
Nikanyanyuka na kuanza kumzunguka jamaa huyu kama mara nne hivi huku nikiendelea kumdadisi huku nikihakikisha kwamba udadisi wangu hauwezi kunaswa na kamera hata moja iliyo kwenye chumba hichi kwani kila kiti kina rekodiwa. Nikajikuta nikitabasamu mimi mwenyewe huku nikikaa kwenye kiti nilicho kuwa nimekalia hapo awali. 
 
‘Waseng** hawa wamemleta bubu humu ndani sasa atazungumza nini?’
Nilijikuta nikizungumza kimoyo moyo huku nikimtazama jamaa wa watu jinsi anavyo chirizika damu, nikashusha mikono yangu chini kidogo usawa wa mweza hii na nikaanza kuzungumza na ishara za vidolea huku nikimuuliza jamaa huyu ni kosa gani ambalo limemfanya hadi kukamatwa na polisi. Nikajikuta nikishtajabu sana mara baada ya jamaa huyu kuniambia kosa la yeye kukamatwa na polisi ni kuiba kuku tena jogoo tena mitaa ya uswahilini, taratibu nikajikuta nikishusha pumzi huku nikitingisha kichwa kwa kumsikitia jamaa huyu mnyonge.
   
ENDELEA
Ili kudhibitisha hilo, nikamuuliza tena kwa ishara jamaa huyu kwamba ni kweli amaeiba kuku. Jamaa akakiri kwa kuapa kabisa huku machozi yakimwagika usoni mwake. Nikanyanyuka kwenye kiti changu na kutoka katika chumba hichi.
“Vipi?”
Biyanka aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu kwa umakini sana.
“Afande mumesema kwamba huyu ndio mtuhumiwa aliye nitumie meseje”
 
“Ndio”
“Sasa mbona hazungumzi?”
Niliuliza swali la kizushi kwa maana ishara zote ambazo nilikuwa ninazizungumza na jamaa huyu ni tofauti kabisa na ishara ambazo watu wa kawaida wamezizoea kuweza kuzungumza na watu wenye ulemavu wa kuzungumza(Mabubu). Ishara nilizi zitumia mara nyingi tunazitumia katika mchezo wa mpira pale wachezaji wanapo amua kubadilisha mfumo wa kucheza pasipo timu pinzani kufahamu kwamba kuna mkakati unapangwa.
 
“Nahitaji apelekwe mahakamani”
“Kuna mambo kidogo tunayahitaji kuyapata kutoka kwake, tukiyakamilisha basi tutampeleka mahakamani”
“Ahaa…Itachukua muda gani?”
“Kama siku moja au mbili hivi”
“Sawa afande acha sisi tuende”
Nilizungumza kwa msisitizo hadi Biyanka mwenyewe akashangaa. Tukatoka eneo hili na kuingia kwenye gari tulilo jia.
 
“Tunaelekea ofisini au nyumbani?”
“Ofisini, nimeiacha simu yangu kwenye chaji”
“Poa”
Tukaondoka eneo hili la polisi huku kichwani mwangu nikijaribu kupanga na kupangua mipango ya kuweza kumsaidia mtu huyu aliye kabambikiwa kosa kubwa toafuti na lile alilo lifanya.
 
“Nitampata tu”
Nilijikuta nikiropoka hadi Biyanka akanitazama.
“Nani tena mume wangu”
“Hakuna tatizo”
“Niambie tu mume wangu, kama kuna tatizo lolote ninakuomba uweze kuniambia?”
“Hakuna”
Tukafika ofisini, moja kwa moja tukaeleka ofisini kwangu.
“Mkurugenzi kikao tayari”
Sekretari wangu alizungumza mara baada kuingia ofisini hapa. Nikamruhusu atoke ofisini kwangu na akaendelee na kazi zake.
 
“Unaweza kuingia kwenye kikao na hali hiyo mume wangu?”
“Ndio ninaweza, kwani nipo vipi?”
“Unaonekana kutokuwa sawa. Kama ni adui yako ndio yote tumesha mkamata, askari wakimaliza kufanya upelelezi wao basi watampeleka mahakamani. Au unahitaji polisi wamuulie gerezani ili kusiwe na mlolongo mrefu mume wangu”
Nikamkata jicho kali Biyanka hadi akastuka, toka niwe naye kwenye mahusiano nina imani kwamba hajawahi kukutana na sura yangu ya kuchukizwa kama hii.
“A…ha….a….si..ku….a…w.a na mahaan hiyo mume wnagu”
Nikanyoosha kidole kuelekea mlangoni. Biyanka akautazama mlango kisha akanitazama mimi.
 
“TOKAAAAAAAAAAA”
Nilizungumza kwa hasira huku nikiibamiza meza kwa nguvu, nikamshuhudia Biyanka akiyumba na kujikuta akiakaa chini pasipo kupenda. Akaanza kuhema kama mtu ambaye amefanikiwa kuwatoroka mbwa walio kuwa wanamkimbizi kwa umbali mrefu sana.
“Nikiwa ninafikiria mambo yangu, sihitaji ushauri wa kipuuzi umenielewa?”
“Eheee”
“Nenda ofisini kwako na muda wa kazi ukiisha nenda nyumbani kwako. Leo ninahitaji kuwa peke yangu sawa”
 
“Unas…..”
“Hakuna cha ninasema, ni hivi leo nana hitaji kuwa peke yangu. Sihitaji kukupasua kichwa chako hicho Biyanka”
Nilizungumza kwa kujiamini huku nikimtazama kwa hasira, hadi mikoyo yangu ina nitetemeka. Biyanka taratibu akanyanyuka na kujiweka vizuri koti lake la suti hii ya kaki aliyo vaa. Akaanza kutembea kwa unyonge kuelekea nje. Nikaka kwenye kiti changu na kukiburuza hadi karibu kabisa na kioo kikubwa ambacho ni kama ukuta wa kuelekea nje. Nikaanza kutazama madhari ya magorofa ya jiji hili la Dar es Salaam.
 
Nikaanza kukumbuka kwamba, kipindi nilipo kuwa mdogo, kitu nilicho kuwa nina kihitaji ni nguvu. Nguvu ambayo ni lazima iweze kusimamishwa kwanza na pesa kisha niweze kuwa na watu ambao wanaweza kupigana kwa ajili yangu, iwe kwenye shida au raha.
 
‘Nahitaji kuwaangusha hawa washenzi’
Niliendelea kuwaza akilini mwangu.
‘Lazima niweze kumtafutia mwana sheria kijana huyu. Hapa ndipo ninaweza kuanza kupata nguvu’
Nikaitazama simu yangu sehemu nilipo iweka, nikaichomoa kwenye chaji. Nikaitafuta namba ya Qeen, nilipo ipata, nikataka kumpigia ila nikaona sio jambo zuri. Nikanyanyua na kueleleka katika ukumbi wa mikutano. Nikawakuta wafanyakazi wote pamoja na meneja wao, ambao wanahusika na maswala ya matangazo.
 
“Samahani kwa kuchelewa”
“Hakuna mashaka mkurugenzi”
“Sawa, kikao changu hakito kuwa kirefu sana zaidi ya kuhitaji kutoa maagizo machache kwenu nyinyi. Kama munavyo fahamu, nyingi nio watu muhimu sana katika kuhakikisha kwamba wateja wanatumia mtandao wetu wa simu. Ninahitaji kwa mwenzi huu unao kuja, tushushe kiwango cha bei za bando za internet, pia bando za watu kuzungumza. Asilimia ya kushusha iwe ni ishirini kwa kila kifurushi. Lengo ni kuwafikia watu wengi sana ambao wengi wao ni wa hali ya chini. Sijui nimeeleweka?”
“Ndio mkurugenzi una eleweka”
“Mfano mdogo tu, endapo wezetu bando zao zitaanzia buku si ndio munavyo sema”
“Yaa elfu moja”
 
Meneja alizungumza huku akitabsamu.
“Sisi tukaweka GB 1 kwa sh mia sita tu, nina imani kwamba katika mzunguko wa kibiashara tuatapa wateja wengi sana kuliko wale watakao weka GB moja kwa sh elfu mbili.”
“Wekeni matangazo mazuri, yakuvutia. Wekeni wadada wazuri na wakaka wazuri sana wanao vutia. Walipeni vizuri, sihitaji figisu figisu huko kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na malipo. Kama mtu atafanya kazi ya kutuingizia mabilioni ya pesa, munashindwaje kumlipa milioni mia au mia mbili kwa tangazo. Hilo meneja lifanyie kazi. Munaona tumeshika namba mbili, awamu inayo kuja nahiji tushike namb moja na kama ni moja basi tusing’oke kabisa. Nakaribisha maswali”
 
Nilizungumza huku nikiwatazama wafanyakazi wangu wote.
“Ahaa mkurugenzi unaonaje tukakuweka kwenye tangazo moja wapo kwa maana una lipa kwa kweli?”
“Haaha, mutanilipa kiasi gani?”
Jibu langu likawafanya watu wote kucheka humu ndani.
“Nilikuwa ninatania jamani. Kwa mimi kuwa katika matangazo ya kampuni yangu mwenyewe, kwanza itakuwa ni roho mbaya, kwani kuna vijana wanajitahidi masikini ya mungu kwenda gym kila siku kutengeneza vifua. Wadada wengine nao ndio hao kila siku kuweka diate kwa ajili ya kutengeneza miili yao. Sasa inabidi juhudi zao siku moja ziweze kuzaa matunda. Nina imani kwmaba nitakuwa nimekujibu kisiasa japo mimi sio mwana siasa”
 
Watu wakaendelea kucheka, japo moyoni mwangu nimejawa na chuki kubwa sana ila nina hakiksisha kwamba hakuna mfanyakazi wangu hata mmoja ambaye anaweza kutambua ni kitu gani kinacho endelea kwangu.
 
“Mkurugenzi mimi nikuahidi, hili jambo mimi na timu yangu tutalishuhulikia kwa haraka sana na baada ya mipango yote kuweza kukamilika basi tutakueletea taarifa”
“Sawa. Nina wazo jengine moja muhimu sana. Hivi munaweza kuanzisha mashindano ya mpira wa miguu kwa timu kubwa kubwa?”
 
“Ndio inawezekana mkurugenzi”
“Tunaweza kuanzisha kombe letu. Hivi hawa wanao shiriki ligi kuu ya hapa nchini wanagombania milioni ngapi?”
“Sabini au themanini hivi”
“Ni themanini mkuu”
“Ahaa, sasa sisi tuanzishe kombe letu, mshindi wa kwanza ana pata dola laki moja na nusu itakuwa kama kiasi gani?”
“Milioni miatatu na usheee”
“Ushee ndio nini jamani?”
“Hahaaa, mkurugenzi ushee inamaanisha ushenzi. Mara nyingi hutumika kwenye kuongezea vionjo vya pesa nyingi nyingi hivi. Kama milioni kumi na ushenzi hivi”
Meneja bwana George alinielewesha na kujikuta nikiwa na furaha sana ya kufahamu kishwahili cha aina hiyo.
 
“Sawa hilo anza kulifwatilia kisha utanipa ripoti. Ila hili la matangazo hakikisheni kwamba linafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo”
“Sawa sawa muheshimiwa”
“Kikao kimekwisha”
Baada ya kumaliza hivyo tukanyanyuka kwenye viti vyetu na kutoka ukimbini humu. Nikapita kwenye mlango wa ofisi ya Biyanka, nikapiga hatua mbili mbele kisha nikarufi nyuma. Nikasoma kibao kilichopo juu katika mlango wake huu. Taratibu nikafungua mlango wake na kuingia ndani.
 
“Nimesema sitaki watu h……..”
Biyanka mara baada ya kunyanyua uso wake alio kuwa ameuinamisha chini ya meza yake na kuniangalia ni mimi akakatisha sentensi yake. Mashvu yake yote yamelowana na machozi, macho yamekuwa mekundu, unyonge mwingi umemtawala hadi nikaanza kumuonea huruma. Taratibu nikatembea hadi alipo kaa, nikamnyoosha mkono wangu wa kulia na taratibu akaupokea, nikamnyanyua na kumshika kiunoni na kumsogeza kifuani mwangu.
“Una lia nini mpenzi wangu?”
Nilizungumza kwa sauti nzito kidogo ila iliyo jaa mahaba mazito hadi nikahisi mwili wangu ukinisisimka.
 
“We….w…e….si…umenifukuza”
Biyanka alizungumza kwa sauti ya kudeka, nikakiinamisha kichwa chake begani mwangu.
”Nisamehe mke wangu, haikuwa akili yangu. Unajua toka nimekutana na tukio lile la kutishiwa uhai wangu, basi limeniathiri kisaikolojia na nimejikuta ni mtu wa hasira na mtu wa kutamani kukaa peke yangu muda wote”
Nilijitetea kwa hilo ili kuweza kuficha yale ninayo yafahamu juu ya Biyanka na baba yake.
“Ohoo jamani mpenzi wangu. Kama vipi twende kwa mwana saikolojia akakupe japo ushauri mdogo unao weza kuirudisha furaha yako. Hivi leo ndio nimekona na kufahamu kwamba una tisha Ethan”
 
“Yaa nalitambua hilo mke wangu?”
“Nimeogopa kwa kweli, nimeshindwa kujizuia mwili wangu hadi nimeanguka chini mpenzi wangu. Nakuomba sana mpenzi wangu twende kwa mwana saikolojia tukitoka hapa kazini. Kwa hali ile tukiwa ndani peke yetu siku unaweza kunivunja hata kiuno changu”
“Sinto weza kufanya hivyo mpenzi wangu. Huko kwenda, tutakwenda siku nyingine sawa mama”
“Sawa, nitampigia ili atupangie siku yetu ya pekee na akatushauri juu ya hili swala”
“Poa mke wangu, mimi kuna kazi ninakwenda kuimalizia ofisini kwangu, nitahitaji utulivu wa kuto buguziwa”
 
“Sawa mpenzi wangu”
Tukanyonyana midomo yetu na Biyanka kwa sekunde kadhaa kisha nikatoka ndani humu. Nikarudi ofisini kwangu na kukaa kwenye kiti. Nikaindika barua pepe kwa wakurugenzi wote wanao simamia kampuni zangu zote duniani na kuwaarifu leo saa nane usiku kwa maasaa ya Afrika mashariki tutakuwa na kikao kwenye mtando wa skype na kila mmoja wao nimemuagiza kufika na ripoti ya mapato ya miezi takribani tisa ambayo sikuwepo katika bara la ulaya. Kila mmoja aliweza kujibu kwamba ameipata email yangu.
 
“Vipi”
Nilizungumza kwa sauti ya chini chini huku simu yangu nikiwa nimeiweka sikio la upande wangu wa kulia.
“Safi”
“Sasa nahiji namba ya yule shemeji yenu ambaye ni mbunge”
“Sawa mkuu”
“Jambo jengine, kuweni tayari muda wowote na wakati wowote kuna sehemu ninaweza kuwaita”
“Sawa mkuu”
 
Nikakata simu mara baada ya kuzungumza na Qeen na Latifa ambao simu zao niliweza kuziunganisha kwa pamoja. Muda wa kuondoka ofisini ukawadia. Tukaondoka na Biyanka huku nikimuomba anipeleke eneo ambalo wana uza laptop zenye ubora wa hali ya juu. Baada ya kununua laptop moja tukaelekea hotelini tunapo ishi.
“Laptop hii ya kazi gani?”
“Leo nina hitaji kuzungumza na wakurugenzi wezangu wa kampuni zangu”
“Ahaaa, sasa kwa nini usinge niambia nikupe laptop yangu?”
“Hapana unajua vitu hivi ni kama simu vile. Unaweza ukawa umeweka mambo yako ya siri ambayo mimi sipaswi kufahamu na mwishowe nikajikuta ninaviona na ikawa shida kwenye mapenzi yetu”
 
“Ni kweli lakini”
Simu ya Biyanka aikaanza kuita, akaipoke ana kuiweka sikioni mwake.
“Sasa ngapi mama?”
“Sawa ngoja nimuage mkwe wako hapa”
Biyanka akaka simu na kunieleza kwamba mama yake ana muomba waweze kuelekea mkono Arusha kwa ziara ya siku mbili, ikiwa ni moja ya mipango ya kutengeneza njia nzuri za baba yake atakapo pita kwenye kampeni aweze kupata wafuasi wengi bila shida na ukitegemea wanawake wengi ndio wanao penda chama tawala.
 
“Sawa, muunge mkono mama.”
“Acha basi nieeleke nyumbani kwake. Tutawasiliana mume wangu”
“Nashukuru”
Biyanka akanipiga busu na kutoka ndani humu. Majira ya saa sita usiku nikaondoka hotelini hapa na kwenda kwenye hoteli Ramada, nikawatarifu Qeen na Latifa waweze kufika katika hoteli hii na nikawapa maelekezo ya chumba nilichopo. Baada ya kama dakika aruboini hivi wakaweza kufika hotelini hapa.
 
“Mkurugenzi umetuita usiku sana vipi kuna tatizo?”
“Hakuna tatizo, ila tunakwenda kuianza kuianza kazi ya kumuangusha mgombea wenu munaye mpenda bwana Poul Mkumbo katika uchaguzi huu”
Qeen na Latifa wakabaki wakiwa wameduwaa, kwani wanafahamu uhusiano wangu wa kimapenzi na Biyanka na mtu ninaye hitaji kumfanyia ukatili ni baba yangu mkwe mtarajiwa.

==>>ITAENDELEA KESHO
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )