Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, January 27, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 61

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
Muda wa mchana, Qeen akanieleza ni eneo gani ambalo tunatakiwa kukutana na watanielekeza kwa simu kuweza kufika huko. Nikamjulisha bwana Samweli ni eneo gani tunaweza kuonana saa nane ya usiku ili tuweze kupanga mipango ya kuweza kuonana. Nikiwa ndani ya gari langu nikielekea ofisini kwangu nikitoka kupata chakula cha usiku, Biyanka akanipigia simu, tukasalimiana kwa furaha sana.
“Vipi mipango yenu?”
“Inakwenda vizuri na tunarudi leo by saa nne usiku tutakuwepo Dar es Salaama, baba anatuhitaji mimi na wewe nyumbani anasema kuna kikao muhimu sana cha kuweza kufanya kama wana familia”
Nikajikuta nikiishia na furaha yangu, kwani sikutarajia kumuona Biyanka akirudi leo jijini Dae sa Salaam kwani anaweza kuwa kipingamizi kikubwa sana cha mipango yangu niliyo ipanga kwa siku ya leo.

ENDELEA
“Kikao cha usiku hicho cha namna gani mpenzi wangu?”
“Hata sisi hatufahamu mume wangu. Yaani tulipanga kurudi kesho, ila ndio kama unavyo ona mambo yamebadilika”
“Sawa nimekuelewa”
“Nashukuru mume wangu upo wapi?”
“Ninatoka kula chakula cha mchana kwenye huu mgahawa hapa ambao tumezoea kula”
“Jamani pole, leo umekwenda mwenyewe mume wangu?”
“Ndio mke wangu. Ila usijali katika hilo”
“Sawa, tutaonana baadae basi”
Nikakata simu huku nikifikiria ni jambo gani ambalo ninaweza kulifanya ili kikao nilicho kipanga leo kiweze kwenda vizuri. Nikatoa simu yangu ndogo na kumpigia  Qeen, simu yake ikaita baada ya muda ikapokelewa.
 
“Qeen upo wapi?”
“Nipo ofisini mkuu”
“Sasa nisikilize, huyu bibie atarudi usiku wa leo na kuna kikao nyumbani kwao”
“Ohoo itakuwaje bosi wangu?”
“Jambo la kufanya sasa hivi, hembu muambie Latifa aweze kuwasiliana na wale watu kama ikiwezekana tuonane saa kumi na mbili”
“Jioni hii!!!?”
Qeen aliniuliza kwa mshangao mkubwa sana.
“Ndio kwa maana tutakosa muda wa kuweza kuoana nao na kama unavyo fahamu kwamba kikao hichi ni muhimu sana kwetu.”
 
“Sawa mkuu nitawajulisha kwamba muda wa kuonana umebadilika, ila sehemu si ile ile?”
“Ndio”
“Sawa nitafanya hivyo mkuu”
Nikakata simu, nikafika ofisini na moja kwa moja nikapitiliza hadi ofisini kwangu. Ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yangu kutoka kwa Qeen, nikaufungua na ananifahamisha kwamba kila jambo lipo vizuri. Majira ya saa kumi na moja nikaondoka hapa ofisini kwangu na kuelekea hotelini nilipo pangisha. Simu yangu ndogo ikaanza kuita, nikaitoa mfukoni na kuipokea.
“Latifa”
“Mkuu ndio tunaelekea eneo la mkuatano”
“Sawa mimi nipo hotelini, ila nitakodisha taksi na sinto hitaji watu waweze kuniona huko”
“Poa itakuwa ni vizuri pia”
 
Nikavaa nguo zangu za mazoezi kisha nikachukua begi langu dogo na kuweka laptop kisha nikavaa earphone masikioni mwangu. Nikachukua kiasi cha pesa kidogo cha kutosha, nikavaa raba ili hata wahudumu walio weka kwama wapelelezi watakapo niona basi wasiweze kustukia juu ya kuondoka kwangu katika hii hoteli. Nikatoka nje ya geti la hoteli, nikatazama barabara huku na kule kisha nikaanza kukimbia hadi kwenye kitu kimoja cha waendesha bajaji. Nikaingia kwenye moja ya bajaji na kumuekeleza dereva huyo sehemu ambayo ninahitaji kuelekea.
“Huko bosi nitakuepelekea kwa ishirini”
“Ishirini elfu au ishirini nini?”
“Ndio mkuu”
“Sawa twende”
 
Kwa mara yangu ya kwanza kupanda bajaji maishani mwangu ni leo. Dereva huyu kwa utaalamu wake kila muda ana jipenyeza penyeza pembezoni mwa barabara ili kuikwepa foleni hii kubwa ya magari majira haya ya jioni. Tukafika eneo la Kunduchi, ambapo ndipo nilipo elekezwa na Qeen. Tukasimama kwenye nyumba moja yenye geti jeusi, nikamlipa dereva huyu elfu thelathini kisha nikaingia ndani ya geti hili na kukuta walinzi takribani ya kumi walio walia suti nyeusi wakiwa wamesimama katika maeneo mbalimbali ya nyumba hii huku kukiwa na magari kadhaa ya kifahari. Nikamkuta Latifa akiwa amesimaa nje ya nyumba hii, tukaingia ndani na nikawakuta wazee watano huku akiwemo na Samweli shemeji wa Latifa, nikawasalimia wazee hawa kisha nikaa kwenye moja ya sofa.
 
“Nashukuru kwa kuweza kufika kwenu hapa”
Nilizungumza huku nikiwatazama
“Sisi pia tunashukuru”
“Nina imani kwamba bwana Samweli ameweza kuwaeleza lengo na dhumuni la mimi kuwepo hapa. Mimi ni mfanya biashara na si mwana siasa ila ninahitaji nyinyi muweze kufanya mabadiliko ya uongozi wa hii nchi.”
Wazee hawa wakakaa kimya huku wakinitazama sana usoni mwangu.
“Nahitaji kuwawezesha kifedha zaidi ya chama tawala. Ni nani mume mteua kugombania uraisi hapa?”
 
“Mimi hapa”
Mzee mmoja mwenye mvu kiasi alizungumza huku akinyanyua mkono wake wa kilia juu kidogo.
“Okay, bajeti yenu muliyo ipanga ni kiasi gani?”
“Tumewekeza bilioni mia mbili?”
“Wapinzani wenu je wamewekeza kiasi gani ulisema?”
“Trilioni moja”
“Nikiwekeza trilioni mbili je mutaweza kufanikiwa kukiondoa chama hicho madarakani?”
Wazee wote wakatazamana huku nyuso zao zikiwa na furaha kubwa sana.
 
“Inawezekana, unajua kitu ambacho kinatuangusha sana katika hizi siasa ni pesa”
“Sawa, mimi Poul Mkumbo ni baba yangu mkwe mtarajiwa, ila sipo kwake kwa ajli ya kuoa ila nipo kwake kwa asili ya kumuangusha chini. Ninacho kihitaji ni kurudisha mgodi wa baba yangu alio uchukua miaka mingi iliyo pita”
“Unataka kusema kwamba mgodi wa Poul Mkumbo ulikuwa ni wa baba yako!?”
Mzee mmoja aliuliza kwa msahangao sana.
 
“Ndio”
“Aisee huyu jamaa ni mshenzi sana”
“Mzee wangu unaitwa nani?”
“Jonson Malisa”
“Unakwenda kuwa raisi wa hii nchi, ila nina kuomba endapo utachukua hichi kiti, hakikisha kwamba unataifisha mali zake kisha mgodi huo unanipatia, kama ana mali nyingine ambazo amezichukua kwa ubadhilifu basi hakikisheni kwamba muna warudishia wale ambao wameweza kupokonywa mali zao sawa”
 
“Hilo linawezekana na halina saka kabisa, nilazima niweze kupambana na ufisadi ulio tukuka katika Tanzania hii”
“Nashukuru kusikia hivyo. Kuna mkatababa nimeuandika hapa, ni wa kusaidi kati yanu na mimi kwani kiasi hichi cha pesa ni kikubwa sana na siwezi kufanya kazi ya kanisa ya kujitolea si ndio jamani”
 
“Ni kweli”
Wazee hawa walizungumza huku wakitabasamu sana. Nikawasha laptop yangu na kuwaonyesha fumo maalumu ambayo wanatakiwa kuijaza kama mkataba, kwa uzuri wa laptop yangu unaweza kundika chochote kwa kugusa kioo chake. Kila mmoja akaanza kuusoma mkabata huu kisha nikawakabidhi kalamu ndogo ya kuandikia katike laptop hiyo. Kila mmoja akaandika saini yake sehemu maalumu huku Qeen na Latifa wakitia saini kama mashahidi.
 
“Kijana tumesaini ila hatujaona hicho kiasi.”
“Ndio tunapo elekea muheshimiwa raisi mtarajiwa”
Nilizungumza huku nikiingia katika mfumo wa benk ya Bacrays ambao ndio nina hifadhia pesa zangu binafsi za kibiashara.
 
“Naomba namba yenu ya benki”
Wakanitajia namba yao kisha nikaanza hatua za kuamisha pesa hizi ambazo ndani ya dakika kadhaa kila kitu kikwa kimesha idhinishwa na pesa kuingizwa kwenye akaunti yao. Kila mmoja akaonekana kufurahi sana kwa kazi makubaliano haya. 
 
“Kila mmoja ninaomba email yake”
Wakanitajia email address zao na nikawatumia huu mkatabasa na meseji maalumu ambayo benki ina dhibitisha kwamba wametuma kiasi hicho cha pesa kwenye akaunti yao.
“Kila mtu ana mkataba wake kwenye email yake. Kumbukeni kwamba mambo haya ni ya siri. Jambo jengine, kuna kiwanda changu cha utengenezaji wa nguo nchini China, nitahakikisha kwamba sare zenu munaweza kuzitolea kwenye kiwanda hicho. Nina imani kwamba ni sare nzuri sana zitakazo wapendezesha wafuasi wenu”
 
“Ndio ndio, ila katika siasa za Kitanzania kuna maswala ya kishirikina”
“Kishirikina ndio nini?”
“Maswala ya kurogana. Je katika hilo tutaweza kuwateka kweli wapinzani wetu?”
Nikaka kimya huku nikiawatazama wazee hawa kwa maana kama ni pesa nimesha wapatia ila kwenye maswala ya uchawi sijui nitawashauri vipi.
 
“Inabidi na sisi tutafute waganga manguli”
“Tutawapatia wapi mwenyekiti?”
“Kwa kuwapatia, humu humu Tanzania”
‘Waambie nitawasaidia, wasitafute Mganga’
Niliisikia sauti ya Ethan masikioni mwangu.
‘Utawasaidia?’
‘Ndio kwani kuna ubaya, kumbuka hawa wanakusaidia kumuangusha adui yako?’
‘Hivi hawato nisaliti kweli?’
 
‘Siwezi kusema ndio au  hapana, ila binadamu wanabadilika kwa kweli?’
‘Tuseme ndio wamebadilika, tunafanyaje?’
‘Nitahakikisha kwamba kila mmoja ana jutia kwa lile ambao amelifanya’
‘Mmmm sawa’
“Kijana”
Sauti ya mwenyekiti wa chama hichi  alinistua kutoka kwenye mazungumzo yangu na Ethan ambayo hakuna hata mmoja wao ambaye ana yasikia.
 
“Ndio”
“Tumeafikiana hapa kwa pamoja kwamba ni lazima tupate waganga kutoka chini nina imani kwamba watatusaidia?”
“Hapan musitafute”
“Kwa nini, kwa maana haya mambo ya kisiasa yana nguvu za ajabu ajabu kijana”
“Kuna rafiki yangu mmoja ata wasaidia, ila ametoa onyo kwa yoyote ambaye atakuwa ni msaliti. Kwangu au kwa chama hichi basi atajutia kwa nini alisaliti, sasa hiyo haijalishi kwamba umesalitije. Mume nielewa?”
Nilizungumza kwa msisitizo na kuwafanya watu hawa wote kukaa kimya huku macho yakiwatoka.
 
“Nyinyi kwa nyinyi mukisalitiana, nina waambia kwamba hamto fanikiwa. Japo wanasema kwamba siri ni ya mtu mmoja basi inabidi iwe ya mtu mmoja kwenu. Sawa jamani”
“Tumekuelewa ndugu”
“Jambo jengine ninalo lihitaji kwenu nyinyi, nitawapatia siri nyeti sana kutoka kwa wapinzani wenu. Ila hakikisheni kwamba hazivuji kati yenu na zikarudishwa kwa wapinzani mume nielewa”
“Tumekuelewa kijana”
“Na kila siri kama ni ya kufanyiwa kazi, basi ifanyiwe kazi haraka sana. Na sasa hivi si munapiga kura kwa mfumo wa kielectronic si ndio?”
“Ndio”
“Basi nitawatafutia watu makini sana kwenye maswala ya tecknolojia. Kitu kingine ninaomba kwamba vinywa vyenu visinizungumzie popote hata kwa wake zenu. Kwasababu musiwaamini wake zenu katika mipango yenu ya kichama. Umenielewa mgombea urasi”
 
“Nimekuelewa mkuu”
“Usije ukasema kwamba huyu anakwenda kuwa first lady wa nchi, na yeye akaanza kujigamba kwa wanawake wezake mwisho mukajikuta jahazi linazama kweupe kabisa.”
“Tumekuelewa kabisa muheshimiwa”
“Nashukuru kwa muda wenu. Mungu akawabariki katika harakati zenu”
Nilizungumza huku nikisimama, nikapeana nao mikono kisha wakaondoka katika nyumba hii na nikabaki na Qeen na Latifa.
 
“Kweli wewe unafaa kuwa kiongozi”
Latifa alizungumza huku akinitazama
“Kwa nini?”
“Unajua saa zote nimekaa pale kwenye sofa, nilikuwa ninakutazamaaa weee unavyo zungumza kwa msisitizo, hadi watu wazima wamejikuta wakikuita mkuu”
“Hahaaaa, kila kitu ni nguvu ya kuzaliwa nayo”
“Kweli”
“Ila hii pesa yangu itarudi jamani?”
“Itarudi tu, kama wakijipanga vizuri itarudi”
“Je wakienda kugawana na kujenga majumba majumba hata kama wakikosa ndio nitolee?”
Qeen alituuliza huku akitutazama.
 
“Itarudi tu, mkataba utawafunga. Si nimewaambia kwamba sifanyi kazi ya kanisa eheee”
“Mmm haya”
“Qeen mpigie simu yule dereva aje kutuchukua”
Qeen akafanya hivyo na ndani ya muda mfupi dereva taksi akafika nyumbani hapa tukaingai kwenye gari hili na kuondoka. Wakanishusha kwenye moja ya kituo waendesha bajaji na pikipiki, nikangia kwenye moja ya bajaji na kuondoka eneo hili na safari ya kurudi hotelini ikaanza majira haya ya saa tatu kasoro usiku. Simu yangu ikaanza kuita, nikaitazama na kukuta ni namba kutoka nchini Ujerumani. Nikaipokea kwa haraka na kuiweka sikioni mwangu.
 
“Ethan”
Niliisikia sauti ya Mery akiniita huku akilia lia.
“Naam”
“Mama hali yake mbaya na kama inawezekana rudi Ujerumani, anahitaji kukuambia neno la mwisho kabla ya kukata roho”
Mwili mzima ukahisi kuzizima na viungo vyote vikafa ganzi, nikajikuta mapigo ya moyo yakinienda kasi hadi jasho likaanza kunitiririka mwilini mwangu.

==>>ITAENDELEA KESHO
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )