Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 30, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 63

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
   
“Tumefika Ujerumani?”
Camila aliniuliza huku akinitazama usoni mwagu”
“Nahisi mke wangu”
Camila akarudi kwenye siti yake na kufunga mkanda, nikafungua kijipazia kidogo cha dirisa na kuchungulia nje, nikaanza kuona baadhi ya majengo marefu ya nchi hii ya Ujerumani, nikashusa pumzi kwani safari hii imetuchukua masaa mengi na sijui ni kwanini tumelala sana. Ndege ikatua uwanja wa ndege, hatukuhitaji kupoteza muda, tukakodi helicopter hadi katika hospitali aliyo lazwa bi Jane Klopp. Da Mery akatupokea, huku akilia kwa uchungu sana, nikakumbatiana naye huku nikihiataji kufahamu ni nini kinacho endelea kwa mama yetu.

ENDELEA
“Mama ana endeleaje?”
Nilimuuliza da Mery huku nikiwa na wasiwasi mkubwa sana. Da Mery hakunijibu jambo lolote zaidi ya kuendelea kumwagikwa na machozi, kwa ishara akanionyesa chumba cha mama alicho lazwa, nikamuachia nami nikaingia ndani ya chumba hicho na kumkuta bi Jane akiwa amezungukwa na madaktari huku wakihangaika  katuka kapandisha mapigo yake ya moyo kwa mashine maalumu za umeme. Zoezi hili hata mimi likaufanya mwili wangu kuzizima, hali ya uchungu na majonzi ikaanza kunitawala, nikajikaza huku nikiendelea kutaza zoezi hili. 

Mashine inayo onyesha asilimia za mapigo ya moyo jinsi yanavyo fanya kazi, taratibu ikaanza kupandisha asilimia hizo kutoka tano hadi kufika asilimia themanini na sita. Madaktari wote wakajawa na furaha kwa maana bi Jane amepunyuka punyuka kwenye kifo.
“Naweza kuzungumza na mama yangu?”
Nilimuuliza mmoja wa madaktari.
 
”Hapana kwa sasa muache apumzike kidogo, akiwa sawa unaweza kuzungumza naye”
“Sawa sawa ninashukuru dokta, ila hali yake ipo vipi?”
“Kama unavyo muona, yupo hapa ICU”
Madaktari walizungumza huku wakinitazama usoni mwangu. Nikwajibu kwa kutingisha kichwa nikimaanisha kwamba nime waelewa. Tukatoka nje ya chumba hichi, da Mery pamoja na Camila wakanyanyuka na kunitazama usoni, tabasamu langu nililo liweka kidogo likawafanya wapate matumaini.
“Vipi mama hali yake?”
“Mapigo ya moyo yameweza kupanda na amerudi katika hali yake ya kawaida”
“Ohoo asante Mungu”
 
Camila alizungumza kwa furaha huku akimkumbatia wifi yake. Tukaendelea kukaa hapa hospitalini na Camila akawasiliana na wazazi wake na kuwajulisha  juu ya uwepo wake hapa nchini Ujerumani. Haikupita lisaa moja, walinzi wa raisi walio ambatana na wazazi wa Camila wakafika hospitalini hapa. Furaha ya kuto kuonana nao kwa kipindi cha muda mrefu ikatawala katikati yetu.
“Mume kua”
Mama Camila alizungumza kwa kututania na kutufanya sote tucheke. Kutokana na majukumu ya kiserikiali baba Camila na mke wake wakaondoka hapa hospitalli na kurudi ikulu huku hapa hospitali ikiwa chini ya ulinzi mkali. “Ethan hivi unatambua kwamba waandishi wa habari wameweka kambi  huko nje?”
“Weeee?”
“Ndio wanahitaji kutuhoji, sasa tutaongea nini kwa maana baadhi nahisi wana amani kwamba tulitekwa kabla ya uchaguzi?”
 
“Usijali tutazungumza nao, ila kwa sasa ngoja tuangalie hali ya mama kwanza”
Daktari mmoja ambaye kichwani mwake ana uwalaza, akaingia ndani ya chumba cha mama, baada ya muda akatoka na kwaishara akaniomba niweze kuingia katika chumba cha mama. Nikanyanyuka kwenye kiti ambacho nilikuwa nimekalia. Nikaingia ndani ya chumba hichi ambacho ni mlio wa mashine ya kuhesabu mapigo ya moyo ndio inasikika kwa sauti ya chini kidogo. Nilipo kisogelea kitanda cha mama, taratibu akatabasamu huku mwili wake ukionekana kudhohofika sana. Nikasimama pemben yake, kwa ishara ya mkono akaniomba niweze kuinama ili anibusu. Nikatii hivyo, taratibu akanibusu mashavuni mwangu, kisha akabalizia busu la upendo kwenye paji la uso wangu.
“Nimerudi mama”
Nilizungumza kwa unyonge sana huku nikimtazama mama usoni mwake. Akatabasamu sana, anaonekana ni mtu anaye hitaji kuzungumza maneno mengi ila anashindwa kutokana na hali yake, akakishika kiganja cha mkono wangu wa kulia na kukiweka kifuani mwake.
 
“Ni…na..k..upe…nda Etha….n”
Bi Jane alizungumza kwa shida kidogo ila niliweza kumuelewa.
“Ninakupenda pia mama”
Nilizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwangu.
“Mli…nde….M…e….ry. A….sij…e aka…p…a…twa na maba…ya”
“Sawa sawa maam nitafanya hivyo”
“Ca…amm…i….la yu….p…o w..p”
“Yupo hapa nje, ngoja nimuite”
Nikatoka ndani humu na kumuita Camil, tukaingia wote ndani ya chumba hichi na Camila na tukasimama pembeni ya bi Jane. Taratibu akavishika viganja vyetu na kuviweka juu ya kifua chake huku machozi yakimwagika usoni mwake.
 
“Pen…da…neni”
“Sawa mama”
“Sawa mama”
Kila mtu alijibu kwa muda wake huku tukiwa na huzuni.
“Ny…ny…I nd..io  ndug…u wa Mery mulio…oo. Sa..lia”
Bi Jane alizungumza huku akihema kwa shida kidogo, japo anapewa msada wa kuhema kwa mashine.
“Mu…pate wa….to….to”
“Tunashukuru sana mama”
“Me…ry….mu…ite”
Camila kwa haraka akatoka ndani humu na baada ya sekunde kadhaa wakaingia na Mery na moja kwa moja wakatudwata hapa kitandani na wakasimama pembeni yangu.
 
“Me…ry”
“Ndio mama”
“Pe…nda neni na E….THAN….ata…kul…inda”
“Sawa mama, nina mpenda sana Ethan”
“N…dio….naj…ua. Ha…ta yey…..e ana….kupe…nd…a”
Bi Jane aliendelea kuzungumza kwa tabu sana huku maneno yake yakiwa ni ya kukata kata.
“Nimekuelewa maama”
“Na….m…fwa..ta mu…me wangu sa…sa. Namuona ana….n…ii..ita”
Wote tukabaki na kigugumizi huku macho yakitutoka, tukabaki tukimuangalia bi Jane na kushindwa kuzungumza chochote.
 
“Nawape…nda. NATAKA KULALA SASA”
Bi Jane mara baada ya kuzungumza hivyo, akatabasamu, kisha akayafumba macho yake taratibu. Mlio wa mashine ya kuhesabu mapigo ya moyo ikaanza kutoa sauti kubwa huku mapigo ya moyo yakianza kushuka chini kwa kasi sana. Kundi la madaktari likaingia ndani humu na wakatuomba tusogee pembeni ya kiitanda hichi. 

Wakaanza kuhakikisha kwamba wana yapandisha mapigo ya moyo, ila kila wanali lifanya, hali ilizidi kuwa mbaya zaidi, kwani pagigo ya moyo yanaendela kushuka. Nikashuhudia sifuri mbili zenye rangi nyekunduhuku mstari mmoja mrefu wa kijani ukionekana kwenye mashine hii. 

Da Mery akaanguka kilio kizito na kuwafanya baadhi ya manesi kumdaka kabla hata ya kuanguka chini. Mwili na akili kwa ujamla vikawa kama vimegandishwa, sikuweza kuelewa ni nini kinacho fanywa zaidi ya kuona heka heka ndani ya chumba hichi. 
 
“ETHAN, ETHAN, ETHAN”
Sauti ya Camila ndio ikanistua kutoka katikwa dibwi la bumbuwazi hili. Nikamtazama huku nikiwa nimemtolea macho makali sana.
“Ehhh”
Nilizungumza, Camila akanikumbatia kwa nguvu huku akilia kwa uchungu sana. Nikamshudia daktari akimfunika bi Jane shuka usoni mwake, nikamuachia Camila na kisogea kilipo kitanda, nikataka kumfunua bi Jane shuka hili ila madaktari wakaniwahi kunikamata, kwa maana wana amani kwamba si akili yangu inayo fanya hivyo.
 
“Nataka kumuoana mama yangu”
Nilizungumza huku nikilia na kujitahidi kujitoa mikononi mwa madaktari hawa. Madaktari wakaongezeka kunishika na kunitoa ndani ya chumba hichi.
“Ethan kazi ya Mungu haina makosa, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu ila tumeshindwa kabisa”
Daktari mmoja alizungumza huku akinitazama, sikumjibu kitu cha aina yoyote kwani akili yangu haina hata uwezo wa kufikiria kwa sasa. Wakaniingiza kwenye chumba cha kupumzikia, nikaka kwenye moja ya kiti huku nikiendelea kushangaa shangaa na kutafakari imekuwaje bi Jane amekufa. Nikamuona Ethan akiwa amesimama mbele yangu huku akiwa amevalia mavazi meupe na usoni mwake akiwa na unyonge mwingi, akakaa pembeni yangu pasipo mtu wa aina yoyote kuweza kumuona.
 
‘Hei’
Ethan alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
‘Jikaze, mama ndio ameondoka hivyo. Yupo kwenye maisha ya furaha kwa sasa’
“Furaha?”
Nilizungumza kwa sauti kubwa na kuwafanya madaktari waliomo ndani humu kunishangaa. Ethana akawatazama madaktari hawa kisha akanishika kifuani mwangu. Mwili ukazidi kunilegea, giza totoro likanitawala machoni mwangu na mwishowe nikajikuta nikilala usingizi fofofo.
                                                                                                          ***
    Nikafumbua macho yangu na kujikuta nikiwa nipo chumbani kwangu katika jumba la mzee Klopp. Nikaa kitako kitandani huku nikisikilizia mziki mlaini unao tumika katika sehemu za misiba, ukisikika kutokea nje ya chumba changu. Nikashuka kitandani kwangu huku nikiwa na boksa tu mwili mwangu, nikaanza kutembea kuelekea mlangoni kabla sijaufikia mlango, mlango ukafunguliwa na akaingia Camila huku akiwa amevalia gauni kubwa jeusi.
“Umeamkaje mume wangu?”
“Nimefikaje hapa?”
 
“Ulipoteza fahamu kwenye chumba cha kupumzikia ambacho madaktari walikuingiza. Nikawashauri waweze kukurudisha nyumbani. Hivyo ni jana ndio umerudishwa nyumbani”
“Sasa hivi saa ngapi?”
“Ni saa mbili asubuhi, tayari maandalizi ya msiba yamefanyika na baadhi ya ndugu na marafiki wamesha kusanyika katika eneo hili”
Camila alizungumza huku akifungua kabati, akatoa suti moja nyeusi pamoja na shati jeusi.
“Inabidi uweze kuingia bafuni mume wangu. Oga uvae kisha upendeze”
“Maiti ya mama imesha letwa hapa nyumbani?”
“Hapana bado ipo hospitalini?”
“Yupo wapi Mery?”
“Sebleni, yupo na baadhi ya marafiki zake wana mfariji”
“Sawa”
 
Nikaingia bafuni, nikauweka sawa mwili wangu ambao bado una uchuvu chovu kidogo. Nikarudi chumbani na kuvaa nguo hizi huku Camila akinisaidia kunifunga vifungo vya shati langu. Tulipo maliza zoezi hili tukatoka chumbani humu na moja kwa moja tukaelekea sebleni, watu wakaanza kunipa pole kwa kufikwa na mama. Nikawashukuru kwa kuja, kisha nikaka eneo alipo kaa da Mery ambaye bado yupo kwenye majonzi mazito sana.
“Hei umepata kifungua kinywa?”
Nilimuuliza da Mary kwa sauti ya chini.
“Hapana”
“Kwa nini?”
“Ethan sijisikii kula chochote”
Da Mery alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu. Sikuona haja ya kumlazimisha kupata kifungua kinywa kwa maana hata mimi kwa upande wangu sijapata kifungua kinywa. Nikamuona Frenando akiwa amesimama pembezoni ya mlango wa kuingilia ndani humu, nikambusu da Mery kwenye shavu la kushoto kisha nikanyanyuka na kumfwata Frenando rafiki yangu wa muda mrefu sana katuka kusoma kwangu. Frenando akanikumbatia huku akiwa na furaha sana ya kuonana nami.
“Niambie rafiki yangu?”
“Poa kaka, pole sana nilisikia juu  ya swala la msiba wa mama nikastuka sana”
 
“Nashukuru ndugu yangu vipi masomo?”
“Kaka tumesha maliza mbona. Umesahau?”
“Akili yangu haipo sawa”
“Twende huku”
Frenando alizungumza huku akinishika mkono wangu wa kulia tukatoka nje na nikakutana na wachezaji wa timu yangu ya shule. Nikasalimiana nao kwa furaha sana huku nikikumbatiana na kila mmoja.
“Nashukuru kwa kuja sana rafiki zangu, hii ni surprise ambayo sikuitarajia kuiona kwa muda kama huu”
“Tupo pamoja ndugu yetu”
“Vipi lile kombe mulilichukua?”
“Ndio tulifanikiwa kupambana hadi dakika ya mwisho na tukafanikiwa kulichukua”
 
“Hongereni sana”
Mchezaji mmoja akaingia kwenye basi kubwa ambalo wamekuja nalo. Akatoka ndani ya basi na kombe ambalo tulikuwa tunaligombania na kunikabidhi jambo lililo nifanya nizidi kujawa na mshangao.
“Tumekuletea kombe hili kapteni ikiwa kama zawadi kwako kwa maana umetufanya tung’are. Yaani hadi tumavyo zungumza hivi sasa, kila mmoja hapa amepata mkataba katika kabla kubwa za hapa Ujerumani na nje ya Ujerumani”
“Weeee”
“Ndio. Mimi Ethan nasubiria jibu lako ni wapi niweze kujiunga kwa maana nimesha tumia ofa na klabu kubwa tatu. Liverpool, Real Madrid na Man Chester City”
Frenando alizungumza kwa furaha huku akinionyesha email za ofa alizo tumiwa na timu hizo.
“Tutalizungumza hilo maswala ya msiba yakiisha”
“Sawa sawa kaka”
“Ethan samahani”
 
Jamaa mmoja mwenye asili ya kijerumani alizungumza huku akiwa amesimama pembeni yangu. Nikamkabidhi Frenando kombe hili kisha tukasogea pembeni kidogo na kuzungumza.
“Ndio”
Akanikabidhi simu yake ya kiganjani.
“Ya nini?”
“Zungumza na huyu mtu”
Nikaiweka simu yangu sikioni.
“Nashukuru sana kwa kurudi Ujerumani. Ulihisi unaweza kulikimbia ili. Tunahitaji BOKSI JEUSI haraka iwezekanavyo kabla ya hatujaharibu msiba wa mama yako”
Maneno ya mwanaume huyu yakanistua sana, jamaa huyu aliye simama eneo hili taratibu akafungua koti lake na kunionyesha bastola aliyo ichomeka kiunoni mwake akiashiria kwamba nikifanya jambo lolote la kijinga anaweza kuniua hapa hapa.
 
==>>ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )