Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, January 29, 2019

Serikali Kuendelea Kukabiliana Na Majanga Nchini

Na.mwandishi Wetu
Serikali kwa ushirikiana na wadau wengine imejipanga kuendelea kukabiliana na majanga yanayoikumba nchi ili kuhakikisha inashughulikia na kutatua majanga hayo pindi yanapotokea.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi Januari 28, 2019 wakati akifungua warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini na kuimarisha uthabiti kwa nchi na jamii dhidi ya majanga ya asili katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Tarishi alibainisha jitihada zinazofanywa na Serikali ili kukabili maafa ikiwa ni pamoja na kuendelea kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kuimarisha ustahimilivu wa majanga ya asili kwa kuongeza idadi ya wilaya zenye mipango ya kupunguza madhara ya maafa, kuboresha mifumo ya tahadhari za awali, kuongeza utoaji wa elimu kwa umma na kuimarisha shughuli za kujiandaa, kukabili na kuimarisha mfumo wa uratibu wa masuala ya maafa.

“Kwa kuzingatia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka wa Mitano, 2016/17- 2020/21 tutaendelea kuimarisha ustahimilivu wa majanga ya asili pamoja na kukabili majanga kwa kuzingatia utekelezaji wa malengo ya msingi ya Mfumo wa Sendai wa Kupunguza Madhara ya Maafa wa mwaka 2015 – 2030, tumedhamiria kuhakikisha tunakabiliana na majanga ili kujiletea maendeleo,”alisema Tarishi

Aliongezea kuwa, kwa kuzingatia majanga yanayoikabili nchi ikiwemo mafuriko nchi haina budi kuwa mikakati hiyo ili kuhakikisha inakabili na kuweka mikakati yenye tija katika masuala ya menejimenti ya maafa nchini.

Tarishi alibainisha kuwa, mafuriko yamekuwa na athari nyingi kwa kulinganisha na majanga mengine yanayoikabili nchi mara kwa mara kwa kuzingatia takwimu zilizopo kwa sasa.

 “Takwimu zinaonesha kuwa kwa kipindi cha Januari hadi Desemba, 2018 mafuriko yameathiri wilaya 50 na kusababisha vifo kwa watu 71, majeruhi kwa watu 64, kuharibiwa nyumba 15,802 kwa viwango tofauti, kuathiri miundombinu katika shule 43, mashamba ya mazao mbalimbali, na vituo vya afya,”alisisitiza Tarishi

Alieleza kuwa, takwimu zilizopo tangu tupate uhuru nchi imeathiriwa na ukame zaidi ya mara 18 ikimo yale  ya mwaka 2006/2007 na 2007/2008 ambayo yaliathiri zaidi mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga, Lindi, Singida, Tabora na Mwanza.

Sambamba na hilo Ukame mwingine mkubwa ulitokea mwaka 2008/2009 ulioathiri zaidi mikoa ya kaskazini ya nchi hasa Arusha na Manyara. Mikoa ambayo mara nyingi huathiriwa na ukame ni Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga, ambayo kawaida hupata mvua ya chini kwa kiwango cha kati ya milimita 200 – 600 kwa mwaka.

Naye Mkuu wa Sekretarieti ya Kupunguza Madhara ya Maafa ya Umoja wa Mataifa kwa Kanda ya Afrika, Amjad Abbashar, alieleza mipango mikakati ya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuzingatia ongezeko la madhara yatokanayo ya maafa ikiwemo vifo, upotevu wa makazi, pamoja na uharibifu wa mali za watu.

“Tutaendelea kushirikiana na kuhakikisha tunakabili na kuzuia maafa yasitokee pale itakapotokea ili kuendelea kuwa na maendeleo endelevu katika mazingira tuliyonayo,”alieleza Abbashar

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,Alvaro Rodriques, aliwataka wajumbe kuitumia fursa ya warsha hiyo kwa kuzingatia mada zitakazowasilishwa ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na wataalam na mikakati yenye kutatua madhara yatokanayo na majanga na kuahidi kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kushughulikia maafa.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )