Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, January 4, 2019

Serikali yatoa mtambo wa kuchuja madini ya fluoride

adv1
Wizara  ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikia na kampuni ya O2 and B imetoa mtambo maalum wa kupunguza kiwango cha madini ya ‘fluoride’ kilichozidi kwenye maji yanayotumiwa na wananchi wa kijiji cha Lemanda, kata ya Oldonyo Sambu wilayani Arumeru.

Mtambo huo, umefanyiwa majaribio na wataalamu wa kampuni hiyo kutoka China ambao wanatengeneza mitambo huo.

Akizungumza wakati wa kusimika mtambo huo, zoezi lililofanyika katika Shule ya Msingi ya Oldonyo Sambu, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, Dk. Wilson Mahera, alisema wamepokea mtambo huo kutoka serikali kuu kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Mtambo huo unaojulikana kwa jina la “Capacity of Deionization System,” (CDI), mtambo huo una uwezo wa kuchuja maji kwa kiwango kikubwa na kupunguza kasi ya madini ya fluoride kwenye maji.

“Mtambo huu una uwezo mkubwa wa kupunguza kiwango cha madini ya fluoride kilichozidi pamoja na chumvi chumvi kwenye maji, kwa kutumia teknolojia hii ya kisasa ya kuchuja maji bila kutumia kemikali kitapunguza madhara kwa wananchi wetu,” alisema.

Alisema mtambo huo una uwezo wa kuchuja maji na kupunguza kiwango cha fluoride kutoka miligramu 18.7 kwa lita moja hadi kufikia miligramu 0.37 kwa lita moja.

“Matarajio ya serikali ni kukabiliana na tatizo hii na litamalizika na kutoa matumaini mapya kwa wananchi wa Lemanda ya kutooza meno na kupinda miguu kutokana na matumizi ya maji yenye madini ya fluoride,” alisema Mahera.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )