Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 13, 2019

Shilole Atoa ONYO Kwa Wadada Wanaommezea Mate Mume Wake

adv1
Mwanamuziki wa kizazi kipya Shilole amewataka wadada wa mjini maarufu kama wadangaji waache kumendea penzi la mume wake.
 
Muimbaji huyo ameeleza kuwa toka mwanzo aliridhika na hali ya mume wake lakini sasa watu wanapoona anang’aa ndipo wanamnyemelea. Kupitia ukurasa wake Instagram ameandika;
 
"Nililizika na hali yako tangu Mwanzo Mpaka sasa unashaine Ila wadangaji msivyo na haya mnaanza kumwambia Mume wangu Uchebe Umekuwa Handsome 😂😂 Mkome Namtunza! ZAMANI milikuwa wapi?? 🤣🤣" ameandika Shilole.
 
Shilole na Ashraf Uchebe walifunga ndoa Desemba 7, 2017 na awali msanii huyo alipondwa kwa kukubali kufunga ndoa na Uchebe, huku maneno yakiwa kwamba hawaendani kiuwezo.
 
Kwa sasa mwanamuziki huyo ndiye mwenye uwezo wa kipato wa kuhudumia familia kutokana na kazi za muziki, mghawa na kufanya matangazo mbalimbali ya makampuni.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )