Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 7, 2019

Spika Job Ndugai Kumjibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad na Halima Mdee Mchana Huu

adv1
Kauli zinazodaiwa kulidhalilisha Bunge zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad, na Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, zimemfanya Spika Job Ndugai, kupanga kuzungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo tarehe 7 Jan, 2019.

Kwa mujibu wa taarifa za Bunge iliyotolewa leo Jumatatu, wawili hao wanadaiwa kusema kuwa chombo hicho cha Dola ni dhaifu.

Miongoni mwa kauli hizo ni ile iliyotolewa hivi karibuni na Profesa Assad alipokuwa akihojiwa na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.

Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Arnold Kayanda, alimuuliza CAG kuwa ofisi yake imekuwa ikijitahidi kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa ripoti zenye kuonyesha kuna ubadhirifu lakini baada ya hapo wananchi hawaoni kinachoendelea.

CAG alijibu: "Hilo ni jambo ambalo kimsingi ni kazi ya Bunge. Kama tunatoa ripoti zinazoonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, huo kwangu ni udhaifu wa Bunge. Bunge linatakiwa kusimamia na kuhakikisha pale panapoonekana kuna matatizo basi hatua zinachukuliwa.

"Sisi kazi yetu ni kutoa ripoti. Na huu udhaifu nafikiri ni jambo lenye kusikitisha. Lakini ni jambo ambalo muda si mrefu huenda litarekebishika. Ni tatizo kubwa ambalo tunahisi Bunge linashindwa kufanya kazi yake kama inavyotakiwa."

Akiendelea kufafanua jibu lake, CAG Assad alisema: "Sitaki kuwa labda nasema hili kwa sababu linahusisha watu fulani, lakini ninachotaka kusema ni kuwa Bunge likifanya kazi yake vizuri, hata huu udhaifu unaoonekana utapungua."

Mwaka 2018  lilipoibuka suala upotevu wa Sh1.5 trilioni kwenye hesabu za Serikali mwaka wa fedha 2016-2017, Assad aliulizwa kuhusu nini kifanyike, akataka Bunge liulizwe kwani ndilo lenye kutakiwa kuibana Serikali kuhusu kutoonekana kwa fedha hizo.

Baada ya kauli hiyo ya Profesa Assad, wiki iliyopita Halima Mdee alihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu alichokisema CAG na kukubaliana na hoja zake.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )