Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, January 27, 2019

Spika Ndugai Asema bado kuna tatizo kubwa katika vipimo sahihi wakati wa ununuzi wa mazao

Na.Alex Sonna,Dodoma
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano La Tanzania Job Ndugai amesema bado kuna tatizo kubwa katika vipimo sahihi wakati wa ununuzi wa mazao kutoka kwa wakulima licha ya kuwepo kwa Sheria ya vipimo.

Hayo ameyasema jana jijini Dodoma alipokuwa  akifungua Semina ya wabunge juu ya changamoto na mafanikio ya sheria ya vipimo ikiwa ni pamoja na wabunge hao kutoa michango yao katika semina hiyo jinsi ya kupambana na rushwa katika vipimo.

Wabunge hao ni wanachama wa hiari wa chama cha kupambana na vitendo vya rushwa APNAC ambao hutoa michango juu ya kupambana na rushwa na kuifikisha panapo husika.

Spika amesema kuwa wakulima wamekuwa wakinyonywa sana na baadhi ya wafanyabisha kwa kutumia vipimo ambavyo si sahihi ikiwemo ufungaji wa mazao kwa njia ya lumbesa.

“Rasilimali nyingi zimekuwa zikipotea kutokana na ufungashaji kwa njia ya lumbesa , na nyinginezo ambazo si rasmi tufikie wakati tuwe na sheria kali zaidi kwani wakulima wetu wamenyonywa  na kupunjwa vya kutosha” amesema Ndugai

Akitolea ufafanuzi kuhusiana na vipimo vya magari ya mizigo Spika alishangazwa kuona kuwa magari hayo licha ya kupita katika mizani mbalimbali lakini bado yanazuiwa sehemu Fulani kwa sababu ya kutakiwa kupimwa tena.

 Aidha amesema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwakera wananchi kwani hawaelewi nini tatizo mpaka kuwepo kwa vipimo kila sehemu na kufanya msururu wa magari kuwa mkubwa kusubiri kupimwa.

“Kama ni magari ya mizigo inawezekana wakaongeza njiani lakini kama wale wanaosafirisha mafuta kweli jamani tuliangalie na hilo tuliangalie” amesisitiza

Spika Ndugai amesema kuwa hali hiyo ni chimbuko la rushwa kwani kama mfanyabishara anayesafirisha mafuta ameshapima vituo vyote hakuna sababu ya kumzuiakwani uwezekano wa kuongeza ujazo wa mafuta njiani ni mdogo.

Awali akitoa taarifa ya awali kwa wabunge wanachama wa chama cha wabunge wanapambana na rushwa (APNAC) Katibu wa APNAC Daniel Mtuka alisema APNEC iliundwa mwaka 2000.

Hata hivyo amesema kuwa  madhumuni ya kuundwa kwake ni kupambana na rushwa mara baada ya kuona vitendo vya rushwa vinazidi.

Pia amesema kuwa wabunge waliokuwepo kipindi hicho waliona kuna umuhimu wa kuanzisha kikundi cha wabunge ambao watapambana na rushwa.

Spika Ndugai amesema kuwa APNAC  ilifanikiwa mwaka 2007 kushiriki kuandaa sheria namba 11 ya TAKUKURU ambapo sheria hiyo ilikuwa na vifungu vine tu lakini sasa vipo 24

Amesema kuwa bado Sheria ya Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa inahitaji marekebisho zaidi. Alisema kutokana na hali hiyo APNAC ilita mawazo wakati wa mchakato wa Bunge la katiba ambao alisema ungewabana zaidi wanaokamatwa na vitendo vya rushwa.

“Tumeweza kutoa marekebisho mengi juu ya Sheria ya TAKUKURU na mengi yameweza kusaidia nchi yetu lakini bado tunaona ipo haja ya kuendelea kutoa mawazo yetu.

Kwa upande wa vipimo  Waziri wa Biashara na Viwanda Josph Kakunda amesema kuwa bado kuna changamoto kubwa katika suala la vipimo.

Hata hivyo amesema kuwa  kumekuwa na udanganyifu mkubwa kwa wafanyabiashara na madalali wanunuapo amzao toka kwa wakulima .

“Vipimo kama vya Lumbesa, Madebe na hata vikopo bado vimekuwa vikitumika katika sehemu nyingi hapa nchini ingawa tunavikataa” amesema

Amesema kuwa Wizara yake imeweza kujenga vituo vya msoko katika mipaka ili wakulima waweze kuuza mazao yao kihalali na uzito unaotakiwa.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )