Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 27, 2019

Tabora yamwagiwa magari na vifaa tiba

adv1
Shirika la Care Tanzania limetoa msaada wa magari manne ya kubebea wagonjwa pamoja na vifaa tiba vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 600 ili kusaidia kuboresha huduma za Afya mkoani Tabora.

Madhumuni ya msaada huo ni kushirikiana na Serikali katika kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga na kusaidia kutoa huduma za usafiri kwa wagojwa wanahitaji matibabu ya dharura katika ngazi za juu.

Msaada huo umekabidhiwa jana na Mratibu wa Mradi wa Afya ya Mama na Mtoto wa Mkoa wa Tabora (TAMANI) kupitia Shirika la Care Flavian Majenga kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri.

Alisema magari manne ni aina ya Suzuki yana thamani ya shilingi milioni 184,678,396 ambayo yatapelekwa katika Zahanati ya Usinge wilayani Kaliua, Zahanati ya Mibono wilayani Sikonge na mengine mawili kwa ajili ya zahanati za Goweko na Tura zilizopo wilaya ya Uyui.

Majenga alisema Mradi wa TAMANI unalenga kuchangia jitiada za Serikali katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya ya mama na mtoto na kuongeza matumizi ya huduma kwa wajawazito.

Aidha Majenga aliongeza kuwa shughuli zinazotekelezwa chini ya mradi wa Tamani zitachangia mafaniko ya Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama katika maeneo yanayohusu huduma wakati wa ujauzito, kujifungua na baada ya kujifungua.

Alisema unafanya kazi na serikali mkoani Tabora katika kuimarisha mfumo wa rufaa kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga kupitia usafirishaji kutokazahanati kwenda ngazi za juu za matibabu.

Majenga alisema kuwa hii ni mara ya pili kwa Care kutoa msaada wa magari na vifaa tiba kwani katika mradi uliopita wa mradi wa Tabora Adolescents And Safe Motherhood(TABASAMU) uliokuwa unafadhiliwa na Serikali ya Canada kwa miaka mitatu kuanzia 2012 hadi 2015 waliweza kutoa magari 16  ya kubebea wagonjwa kwa Halmashauri zote za mkoa wa Tabora.

Mratibu huyo wa Care alisema sanjari na msaada huo wa  magari hayo Care pia imetoa vifaa tiba aina mbali mbali vyenye thamani ya shilingi milioni 424,174,650/= kwenye zahanati 165 na vituo vya Afya 11 katika halmashauri zote mkoani Tabora.

Alisema vifaa hivyo vimepelekwa katika Wilaya ya Sikonge kwenye zahanati 24 na vituo vya afya vitatu ambavyo vina thamani ya shilingi milioni 49.1, Urambo zahanati 20 na kituo cha afya kimoja vyenye thamani milioni 42.8, Kaliua zahanati 36 na vituo vya afya viwili vyenye thamani ya milioni 75.7 na Nzega DC zahanati 11 na kituo cha afya kimoja vyenye thamani milioni  62.9.

Majengwa aliongeza kuwa Halmashauri nyingine ni Nzega Mji vitapelekwa katika zahanati mbili na kituo cha afya kimoja vyenye thamani milioni  15.1,Manispaa ya Tabora zahanati 19 na kituocha afya kimoja vyenye thamani milioni 46.3 Uyui zahanati 37 na kituo cha afya kimoja vyenye thamani milioni 43.5 na Igunga zahanati 16 na kituo cha afya kimoja vyenye thamani milioni 88.5.

Akipokea msaada huo mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alilishukuru shirika hilo na kushauri mashirika mengine kuendelea kusaidia na serikali kuokoa afya za Watanzania wakimemo mama wajawaziti na watoto wachanga.

Aliwataka Wakuu wa Wilaya na Halmashauri kuhakikisha hakuna mama wajamzito na watoto wanatozwa fedha wakati wa kupata matibabu.

Aidha Mwanri aliwataka kuhakikisha wagonjwa wote wanakwenda jupata huduma za matibabu wanapata dawa kwa kuwa upatikanaji wa dawa muhimu umeboresha ambapo asilimia 94 zinapatikana katika vituo vya afya kupitia bohari kuu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )