Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 23, 2019

TANESCO Yaalika Wawekezaji Jijini Arusha

adv1
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limewataka wawekezaji nchini kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya kuwekezaji kwenye ujenzi wa viwanda kwani umeme upo wa kutosha.

Akizungumza jana Jumanne Januari 22, mjini hapa, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Mhandisi Herini Mhina, alisema uzalishaji huo umeongezeka kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali kwenye miradi mbalimbali ya umeme.

Alisema uwekezaji huo umeliwezesha shirika hilo mkoani humo kutoa huduma za uhakika kwa wateja wakubwa wa umeme, wa kati na wadogo bila usumbufu wowote.

“Tanesco Arusha tunakaribisha wawekezaji wengi zaidi waje kuwekeza kwenye sekta mbalimbali, tuna umeme wa kutosha, tunaamini viwanda ni njia ya kutupeleka katika uchumi wa kati,” alisema Mhandisi Mhina.

Alisema Serikali kupitia Tanesco imetekeleza miradi mingi ya umeme, jamii haifahamu uwekezaji uliofanyika ambao ni mkubwa na wenye gharama kubwa.

Akizungumzia hali ya kukatika umeme, amesema kwa sasa tatizo hilo halipo kabisa, umeme hukatwa yanayofanyika matengenezo na ukataji miti ili kusafisha njia za umeme.

“Kwa sasa mkoa huu unazalisha umeme wa megawati 120 ingawa mahitaji kwa sasa ni megawati 75 jambo linalifanya Tanesco kuwa na bakaa ya umeme wa megawati 50.

“Uwekezaji uliofanywa na serikali katika sekta hii, umemaliza tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara kama ilivyokuwa miaka ya nyuma,” alisema.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )