Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 14, 2019

Vyama vya siasa vyaalikwa kutoa maoni muswada wa sheria ya vyama vya Siasa

adv1
Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria inatarajia kukutana na wawakilishi wa vyama vya siasa Januari 19 na 20, 2019  kuwasikiliza na kupokea maoni yao kuhusu muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018.

Kamati hiyo itapokea maoni yao baada ya kumaliza vikao vyake na wadau wengine vitakavyofanyika Januari 17 na 18, 2019  mjini Dodoma kuhusu muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2018 na kufuatiwa na mkutano wake na wawakilishi wa kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu hapa nchini ambao wanapinga muswada huo.

Bunge litapokea maoni hayo wakati leo kesi iliyofunguliwa kupinga Bunge kujadili muswada huo ikiwa inatolewa uamuzi mahakamani.

Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu na wanasiasa watatu ambao ni kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, Joram Bashange na Salim Bimani kutoka Chama cha Wananchi (CUF) kwa niaba ya wanachama wa vyama 10 vya siasa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )