Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 23, 2019

Wachimbaji madini waomba kuanzishwa benki yao

adv1
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (Femata), John Bina ameomba kuanzishwa kwa benki ya madini nchini itakayokuwa inatunza madini na kutunza fedha za wachimbaji.

Pia, wameomba Serikali kuweka hati ya utambulisho katika madini ya Tanzanite ili ijulikane inatokea Tanzania peke yake.

Bina akizungumza jana Jumanne Januari 22, 2019 katika mkutano wa wachimbaji, wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini nchini alisema sababu ya benki hiyo itakuwa imesheheni wataalamu wa madini itaweka urahisi kwao kutunza bidhaa zao na kupata mikopo.

“Kwa sababu katika benki hizi za kawaida kukopesheka ni kugumu sana lakini tukiwa nayo ya kwetu tutakuwa huru na wadau wote wa madini watahusika, itakuwa chini ya BoT (Benki Kuu ya Tanzania),” alisema Bina.

Pia, wamewaomba wadau na BoT kushirikiana kununua madini yaliyopo nchini ili kurekebisha na kusimamia soko la madini.

“Kwa sasa matatizo yaliyopo, wanunuzi wapo lakini hawaonekani  likitokea tatizo dogo wanaacha, Geita hali ni mbaya mno gramu moja imetoka kwenye Sh80,000 hadi Sh30,000 hivyo benki itakapokuwapo itaoongoza soko,” alisema Bina.

Alisema Tanzanite kuwekewa utambulisho utasaidia kubaini madini mengine ya aina hiyo ni bandia.

“Hata ikitangazwa katika utalii itaonekana uhalisia wake ni kutoka Tanzania na inakuwa ni nembo pekee ya kutangaza nchi,” alisema.

Pia, ameiomba Serikali kuwasemea wachimbaji wadogo wanaodaiwa katika maeneo ambayo hawakuyachimba kwa kukosa taarifa sahihi za kijiolojia.

Wachimbaji hao wameomba kuanzishwa kwa siku ya madini nchini itakayokuwa inasherehekewa Julai 5 kila mwaka pamoja na kuomba mwakilishi mmoja ndani ya Bunge.

Bina alisema wakati wachimbaji hao wanaomba leseni huangalia sehemu yenye madini lakini pindi yanapoacha kupatikana wanakimbia.

“Kinachotokea zile leseni ukienda TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) unaambiwa unadaiwa katika viwanja vyako Iringa. Tunaomba tukiyachimba mtusamehe madeni kwa sababu ni mzigo kwetu,” alisema.

Akizungumzia siku maalumu ya madini alisema kutokana na nchi kuwa na zaidi ya madini 260, amsema hakuna haja ya wao kupeleka katika maonyesho nchi nyingine.

“Tumekubaliana kuwa siku hii itaitwa Magufuli Day na tutaonyesha bidhaa zetu zote zitokanazo na madini nchini ili kuweza kuitangaza nchi kimataifa,” alisema Bina.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )