Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, January 17, 2019

Wahukumiwa JELA Miezi Miwili Kwa Kosa la Kuondoka Nchini Bila Kufuata Utaratibu

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu wafanyabiashara sita kulipa faini ya Sh. 50,000 ama kwenda jela miezi miwili baada ya kukiri kosa la kuondoka nchini bila kufuata utaratibu.
 
Hata hivyo ni washtakiwa watano ndio wamefanikiwa kulipa faini hiyo hivyo kuachiwa huru na mmoja kurudishwa rumande.
 
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya Wakili wa Uhamiaji, Novatus Mlay kuwasomea mashtaka yao.
 
Washtakiwa hao wanadaiwa Januari 14, mwaka huu walikutwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakiwa wameondoka kwenda Afrika Kusini bila kuwa na vibali.
 
Baada ya kusomewa shtaka hilo, washtakiwa hao ambao wapo tisa, wawili walikana na sita walikiri kosa na kusomewa maelezo ya awali.
 
Katika maelezo ya awali, Wakili Mlay alidai Januari 14, 2019 washtakiwa walishushwa na ndege katika uwanja wa JNIA wakitokea Afrika Kusini ambapo walipelekwa Idara ya Uhamiaji Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.
 
Wakili Mlay alidai, katika maelezo ya onyo, washtakiwa walikiri kosa la kwenda Afrika Kusini bila Passport, ambapo walikamatwa kupitia Operation inayoendelea huko na kurudishwa nchini.
 
Baada ya kueleza hayo, washtakiwa walikubali maelezo hayo ambapo Hakimu Mashauri alisema anawatia hatiani washtakiwa hao.
 
Hakimu Mashauri alisema, ana wahukumu kulipa faini ya Sh. 50,000 ama kwenda jela miezi miwili kwa kila mmoja.
 
Kuhusu washtakiwa waliokana makosa yao, upelelezi umekamilika na kesi imeahirishwa hadi Januari 30, mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.
 
Washtakiwa waliohukumiwa ni Mussa Njogo, Hemed Semi, Mohammed Moshi (27), Carlos Mhando (22), Lista Mlawi (20) na Abdallah Marola (25).
 
Waliokana makosa yao ni Shaibu Mohammed (26), Ibrahim Mketa (30) na Kassim Kitapi (22) ambapo wamerudishwa mahabusu.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )