Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 27, 2019

Wapinzani Waridhishwa na Marekebisho yaliyofanyika Katika Muswada wa Vyama vya Siasa

adv1
Vyama 15 vya upinzani vya siasa 15 vilivyokuwa vikipinga muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa vimesema vimeridhishwa na marekebisho yaliyofanywa na Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba licha ya kasoro chache walizoomba zifanyiwe kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya vyama, leo Jumapili Januari 27, 2019 jijini Dar es Salaam, naibu katibu mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu amesema baada ya kutoa maoni yao mbele ya kamati hiyo hivi karibuni bungeni Dodoma, hoja nyingi walizopigia kelele zimesikilizwa.

"Tulipigia kelele suala la mafunzo na adhabu zake. Kamati baada ya kupitia hoja zetu, kwanza imepunguza adhabu kutoka Sh1 milioni hadi Sh500,000 na jela kutoka miezi 6 hadi mitatu," amesema Mwalimu.

Hata hivyo, amesema bado kuna utata umebaki wa kuchanganya elimu ya uraia na kujengeana uwezo ndani ya chama.

"Jambo kubwa ni kipengele kuamua utoaji wa elimu ya uraia, kimeondolewa. Yeye anazungumzia capacity building, tunaiomba kamati iangalie hili."

Amekitaja kipengele cha 3b kilichosema msajili anaweza kuomba taarifa kutoka kwa mwanachama yeyote na sasa kinasema ataomba taarifa kwa kiongozi yeyote.

"Bado tunaiomba kamati irekebishe iseme mawasiliano yafanywe kwa katibu mkuu kwa kuwa yeye ndiye 'contact person' tunaona nia mbaya ya msajili kuvuruga vyama," amesema.

Hata hivyo, amesema kuna mambo ambayo yamebaki bila kufanyiwa kazi, akiwaomba wabunge kuendelea pale kamati hiyo ilipoishia.

"Yapo mambo ya msingi kabisa tuliyajengea hoja yamefanyiwa kazi, lakini kuna vipengele ambavyo bado havijafanyiwa kazi, tunaomba vifanyiwe na ikishindikana vifafanuliwe na Bunge, asiyeshukuru kwa kidogo hawezi kushukuru kwa kikubwa," alisema Mwalimu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )