Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, January 26, 2019

Watu Wawili Wakamatwa Na Jeshi La Polisi Njombe Kwa Tuhuma Za Kuhusika Na Utekaji Wa Watoto

Wanaume wawili wanaojulikana kwa majina ya Joseph Nziku(35) Mkazi wa Mkazi wa Mtaa wa Magegele Mjini Makambako na Alphonce Danda(51) Mkazi wa kijiji cha Ibumila wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Njombe kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya utekaji na mauaji ya watoto yalioibuka tangu desemba mwaka jana katika wilaya ya Njombe.

Taarifa zinadai zaidi ya watoto 10 wametekwa na baadhi yao kukutwa wameuwawa katika mapori mbalimbali wilayani humo hali ambayo imeleta taharuki kwa wakazi wa mkoa huo na kuvisukuma vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo kufanya doria na misako ya usiku na mchana kuwabaini wahusika wa matukio hayo.

Akizungumz na vyombo vya habari katika makao makuu ya jeshi la polisi mkoa wa Njombe kaimu kamanda mkoani Humo Rashid Ngonyani amesema jeshi liwashikilia watu hao baada ya kupata taarifa za awali kutoka eneo la tukio kwamba wamehusika na utekaji wa watoto katika kijiji cha Ibumila.

Katika hatua nyingine Kamanda Ngonyani amesema jeshi hilo pia linawashikilia watu wengine wawili wakike na kiume wanaojulikana kwa majina ya Zebedayo Mgulunde(23) ambaye alitishia kutekwa kwa lengo la kukwepa kulipa deni la shilingi laki moja na nusu pamoja na Maria Mgeni(26) aliejaribu kujinyonga ili kukwepa kulipa fedha zaidi ya shilingi laki sita za kikundi cha kuchangishana fedha ambazo alikuwa mezitumia na baadae wawili hao kusambaza taarifa za kutekwa jambo ambalo sio kweli.

Wakati jeshi la polisi likitoa taarifa hiyo nalo baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Njombe wameibua hoja ya kuitaka serikali kuchukua hatua za haraka dhidi ya mauaji hayo ambayo yamewafanya wazazi na walezi kutumia muda mwingi kulinda watoto wao zaidi katika muda wa kwenda na kurudi shule hali ambayo imeathiri shughuli za uchumi wilayani Njombe.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )