Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 14, 2019

Waziri Lugola, Mwakilishi UNHCR Wajadiliana Masuala Ya Wakimbizi Waliopo Nchini

adv1
Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya, ofisi ndogo ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo, na kujadiliana masuala mbalimbali ya wakimbizi nchini.

Waziri Lugola pamoja na Mwakilishi huyo, pia walijadiliana masuala ya ushirikiano kati ya Serikali na Shirika hilo la Kimataifa kwa mujibu wa sheria zinazowaongoza.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika jana Jumapili, Lugola alisema Wizara yake haiwezi ikafanikiwa kikamilifu katika masuala ya kuwahudumia wakimbizi nchini kama haitashirikiana ipasavyo na UNHCR.

“Licha ya kuwa baadhi ya wakimbizi wanaendelea kurudishwa kwa hiari nchini kwao Burundi, lakini katika kufanikisha zoezi hili, lazima tushirikiane ipasavyo kati ya Serikali pamoja na nyie UNHCR, naamini Wizara yangu itafanya vikao nanyi mara kwa mara ili kufanikisha zoezi hilo pamoja na mengineo yanafanikiwa,” alisema Lugola.

Kwa upande wake Mwakilishi wa UNHCR, Kapaya, alisema Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika lake vizuri, na jambo lolote la majadiliano linapotokea ujadiliana ili kuweka sawa ushirikiano huo.

“Mheshimiwa Waziri mimi nakushukuru sana kwa kuniruhusu kuja kufanya mazungumza nawe, nimefarijika na haya madiliano na pia tutaendelea kushirikiana zaidi,” alisema Kapaya.

Katika kikao hicho Mwakilishi wa UNHCR aliambatana na Msaidizi wake Zephania Amuiri, na Waziri Lugola aliambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara yake, Harrison Mseke.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )