Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 29, 2019

Waziri Ndalichako atoa siku mbili kwa waliokula fedha za Elimu Wazirudishe

adv1
Wakurugenzi watendaji wa halmashauri waliochepusha fedha za mradi wa malipo kwa matokeo (EP4R) sasa wamekalia kuti kavu baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kuwaagiza wazirejeshe fedha hizo ndani ya siku mbili

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa maofisa na watendaji katika ngazi ya kanda, mikoa na halmashauri za mikoa ya Shinyanga na Mwanza jana Januari 28, 2019, Waziri Ndalichako ameagiza fedha hizo zirejeshwe ifikapo mwisho wa siku ya Jumatano Januari 30, 2019.

Mafunzo hayo yanahudhuriwa na maofisa elimu, wathibiti wa ubora, wakuu wa shule za sekondari na walimu wakuu wa shule za msingi kutoka mikoa hiyo miwili.

Waziri Ndalichako ameelezea kushangazwa na kitendo cha baadhi ya wakurugenzi kulalamikia changamoto ya miundombinu ikiwemo vyumba vya madarasa katika maeneo yao huku fedha ambazo zingetumika kutatua changamoto hizi wakizitumia kwa matumizi mengine ikiwemo kulipana posho.

“Kila nikitazama habari mpaka inakera kila mtu analalamika ujenzi wa madarasa mnamwambia nani? huo ni uzembe wenu

“Mimi naangalia elimu bila malipo watoto wanakaa darasa moja mpaka 200, pesa tunaleta halafu nyie mnagawa mfanyakazi bora ikifika Jumatano tutaongea lugha nyingine.

“Siwezi nikafurahia pesa yeyote inayopita kwenye mikono yangu nataka mrudishe fedha mtazitoa wapi hayatuhusu, nitampasia Jafo yeye atafunga goli” 
Alisema Waziri  Ndalichako
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )