Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 12, 2019

Amuua Mwanafunzi kwa kumchinja na sime kisa pete

Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia Kereto Likoko [Mmasai] kwa madai ya kumuua Mwanafunzi Samson Conradi anayesoma katika Chuo cha Faraja kwa kumkata na sime shingoni kwa madai ya kushindwa kumlipa fedha ya pete ambayo alikuwa akiuza.

Akizungumza jana Jumatatu Februari 11, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Kilimanjaro, Hamis Issah alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Isah amesema taarifa za awali zinaonyesha kuwa kabla ya kifo marehemu akiwa na mwanafunzi mwenzake, Andrew Charles, walikuwa katika mazungumzo ya kuuziwa pete na mtuhumiwa huyo.

“Wakati wakiendelea na mazungumzo hawakuelewana na mtuhumiwa akitaka kupatiwa fedha yake, na alichomoa sime na kumjeruhi  marehemu shingoni. Alivuja damu nyingi na amefariki dunia,”amesema Kamanda Issah
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )