Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 6, 2019

CCM Njombe Yaadhimisha Miaka 42 Kwa Kupanda Chai

adv1
Na   AMIRI KILAGALILA
Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Njombe jana kimeungana na wananchi wa kijiji cha uliwa kata ya Ihungilo mkoani Njombe katika zoezi la upandaji wa miche ya chai ili kukuza na kuendeleza zao hilo la kimkakati mkoani humo pamoja na kuadhimisha miaka 42 ya chama hicho tangu kilipozaliwa.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, katibu wa siasa na uenezi wilaya ya Njombe HITLA BENJAMINI MSOLA amesema kuwa chama hicho kimeamua kufanya maadhimisho hayo kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho ili kuakisi ukombozi wa uchumi wa Tanzania.

“kwanza tumefikisha miaka 42 ya chama cha mapinduzi, na huko nyuma tulikuwa tukiadhimisha kwa ngonjera na nyimbo lakini kwa sasa tuko na ccm mpya inayofanya kazi kwa vitendo na tumeamua kufanya hivi na kufanya kazi ambazo zinaakisi ukombozi wa uchumi kwa mtanzania mmoja mmoja na Tanzania kwa ujumla,na chai itakwenda kulisha viwanda vyetu na ukiangalia zao hili la chai ni miongoni mwa zao la kimkakati hususani katika mkoa wetu na katika eneo hili ni zao ambalo linastawi vizuri”alisema MSOLA

DENIS MSIGWA ni mwenyekiti wa kikundi cha Mapinduzi kinachomiliki shamba hilo anasema kuwa,watu wengi katika kijiji chao walikuwa na hamasa ndogo katika kilimo cha chai hivyo kupitia hamasa hiyo anaimani zao la chai litalimwa kwa wingi katika kijiji chao ukilinganisha na vijiji vingine vilivyopo katika tarafa ya IGOMINYI.

“kwa kweli tumehamasika kwa kuona viongozi wetu tuko nao pamoja hapa, na hamasa itakuwa kubwa kwa kuwa watu awali walidhani kilimo hiki hakina tija lakini kwa kuja kwa viongozi hawa tunauhakika sasa wananchi wamehamasika zaidi ya kipindi cha mwanzo licha ya elimu tuliyokuwa tukiipata”alisema DENIS MSIGWA.

Kwa upande wake afisa kilimo wa halmashauri ya ya mji wa Njombe ELNEST NGAPONDA amewataka wakulima wa chai kuonyesha juhudi katika kilimo hicho kwa kuwa kitakuwa na uhakika wa kipato ukilinganisha na mazao mengine ya viazi na mahindi.

“kwasababu soko lipo na bei nzuri ipo inatolewa na kiwanda cha Uniliver wakulima watakuwa na uhakika wa kipato na ukiangalia wataalamu watakaotoa maelekezo ya kitaalamu wapo kwa kufanya hivyo ni lazima tu wakulima hawa watakuwa na kipato kizuri kuliko kutegemea mazao ya mahindi na viazi yanayoathiliwa na bei kila wakati, muhimu wakulima wajiunge katika vikundi ili serikali iweze kuwawezesha baadhi ya pembe jeo”alisema Ngaponda

Naye meneja wa kampuni ya NOSC  PHILBET KAVIA wadau wakubwa wa zao la chai mkoani Njombe amesema kuwa wataendelea kumsaidia mkulima wa chai kwa kila Njia licha ya kuwepo kwa changamoto mbali mbali ikiwemo ubovu wa miundombinu.

“lengo letu Nosc ni kuinua kipato kwa mkulima maskini mmoja mmoja ambao ukiangalia ni mtizimo wa serikali na serikali hii inaongozwa na chama cha mapinduzi sasa kuja kwa viongozi hawa maeneo haya hawa wananchi wanapata faraja na nguvu ya kufanya kazi kupitia serikali yao,lakini changamoto kubwa tulizonazo ni barabara na unajua mashamba hayapo vijijini kwenye village centre  na hazipo chini ya Tarula, na hapa kikubwa ni kuona jinsi gani hizi barabara zinaboreshwa ili kupunguza gharama kwa mkulima na hata kwa kampuni na kufikisha pembejeo kwa urahisi mashambani”alisema KAVIA

Zaidi ya miche 500 ya chai imepandwa na viongozi mbali mbali wa chama na wananchi katika shamba la moja ya kikundi cha wakulima kijijini hapo katika maadhimisho ya miaka 42 ya chama cha mapinduzi yaliyofanyika kiwilaya katika kata ya Ihungilo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )