Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 15, 2019

CHADEMA Kufungua Kesi Mahakamani Kuipinga Sheria ya Vyama vya Siasa

adv1
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitafungua kesi mahakamani kupinga sheria ya vyama vya siasa ambayo sasa inasubiri kusainiwa na Rais  John Magufuli ili kuanza kutumika.

Makamu mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdallah Safari amesema chama hicho kilipinga muswada huo lakini kesi yake ya kuupinga haikusajiliwa mahakamani.

"Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa (wa mwaka 2018) unakuja kunyonga demokrasia, tulishirikiana na wadau kuupinga lakini hatukufanikiwa sasa tutafungua kesi ya kupinga sheria yenyewe itakapoanza kutumika,” amesema Profesa Safari.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amesema chama hicho kinasubiri sheria hiyo itangazwe katika gazeti la Serikali (GN) ili kupeleka mahakamani vipengele ambavyo hawajaridhishwa navyo.

"Mahakama ina mamlaka ya kuondoa vipengele vyote ambavyo vinaminya haki za binadamu lakini pia vinavyokiuka katiba ya nchi. Hata tulipokwenda kusajili kesi ya kupinga muswada tuliambiwa tusubiri iwe sheria," amesema Dr Mashinji.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )