Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 5, 2019

Godbless Lema Asema Kufungwa Kwa Maduka ya Kubadilishia Fedha Kutakimbiza Watalii

adv1
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema amesema kufungwa kwa maduka ya kubadilishia fedha kutapunguza idadi ya watalii kutokana na usumbufu wanaoupata kutokana na hatua hiyo.

Lema amesema hayo  jana Jumatatu Bungeni Februari 4, 2019 wakati akichangia taarifa za kamati za Bunge za Miundombinu na Viwanda, Biashara na Mazingira.

Alisema biashara haihitaji nguvu wala polisi ili kuifanikisha na kutoa mfano wa maduka ya kubadilisha fedha yaliyofungwa jijini Arusha miezi miwili iliyopita.

Alisema hakuna duka la fedha linabadilisha fedha jijini humo hivi sasa, ni lazima watalii waende Moshi ama waingie benki kubadilisha fedha.

Hata hivyo, alisema kutokana na usumbufu huo, kampuni za utalii zinaamua kuwahamishia nchi jirani ya Kenya watalii ili kuepuka usumbufu.

Alisema idadi ya watalii itapungua sana mwaka huu na kuhoji inachukuaje miezi miwili kurudishwa.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )