Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, February 15, 2019

Hukumu kesi ya Malkia wa Tembo Kutolewa Februari 19

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Februari 19, 2019 kutoa hukumu katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili washtakiwa watatu, akiwemo raia wa China, Yang Feng Glan (66).

Glan, maarufu kama Malkia wa Tembo na wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh13 bilioni, kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo ilitakiwa kutolewa leo, Februari 15, 2019 lakini Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, anayesikiliza shauri hilo bado hajamaliza kuandika hukumu.

Hakimu Shaidi amesema, kuna vitu anamalizia kuviandaa katika hukumu hiyo, hivyo amepanga Jumanne ya wiki ijayo ndio atatoa hukumu.

"Nitatoa hukumu hii siku ya Jumanne ya wiki ijayo, kuna vitu namalizia katika uandikaji wa hukumu hii," alisema Hakimu Shaidi.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )