Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 21, 2019

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza AKANUSHA Taarifa za Kukutwa Vichwa Vya Watoto Kituo cha Polisi

adv1
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro amekanusha uvumi uliosambaa  jana wa kukutwa vichwa vya watoto kituo cha polisi na kusema taarifa hizo hazikuwa za kweli.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza Kamanda Muliro amesema ni watu wachache ambao waliamua kutangaza taarifa hiyo ambayo baadaye ilileta sintofahamu kwa baadhi ya wananchi wa Mwanza.

"Kuna watu walianzisha taarifa kuwa kuna watoto walikuwa wamekufa na vichwa vyao kukutwa kituo cha polisi, uvumi ule uilisababisha watu zaidi ya 500 kukusanyika kuja kituo cha polisi lakini hata tulipowaelewesha kwamba taarifa hizo sio za kweli   hawakuelewa.

"Pamoja na huduma za kiusalama tunazotoa, ilitulazimu tutumie mabomu ya mabomu ya machozi ili kuwatawanya kwa sababu waligoma kuondoka lakini pia tunawashikilia watu kadhaa kwa ajili ya mahojiano ya tukio hilo." amesema Muliro.

==>>Msikilize hapo chini
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )