Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 8, 2019

Kamati ya Bunge Yashauri Wafungwa waliooa Wajengewe vyumba private ili wapate tendo la ndoa

adv1
Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imeishauri Serikali kuandaa na kutekeleza mpango mkakati chini ya Magereza kuwafanya wafungwa wanapata haki ya kutembelewa na wenza wao na kupata haki ya tendo la ndoa.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kamati hiyo bungeni jijini Dodoma leo Ijumaa Februari 8, 2019 mwenyekiti wake, Mohamed Mchengerwa amesema hatua hiyo itapunguza maambukizi ya magonjwa kwenye magereza ikiwemo Ukimwi.

“Serikali iandae na kutekeleza mpango mkakati chini ya Magereza ambao utahakikisha wafungwa wenye ndoa wanawekewa mazingira yatakayohakikisha wanapata haki ya kutembelewa na wenzi wao na kupata haki ya tendo la ndoa kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa na mamlaka husika,” amesema.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )