Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 12, 2019

Katibu Mkuu Vijana CCM Ashangazwa Na Wanasiasa Wanaoichafua Nchi Ughaibuni

Na Amiri kilagalila
Viongozi mbali mbali wa chama cha mapinduzi CCM wamewataka wanasiasa na watanzania kwa ujumla kuungana kwa pamoja katika kupambana na vitendo vinavyoendelea katika baadhi ya maeneo nchini yakiwemo mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe kuliko kuendelea na siasa za uchochezi katika mataifa ya ughaibuni.

Hayo yalisemwa na katibu mkuu wa umoja wa vijana Taifa ndg.Raymond Mwangwala wakati akizungumza na baadhi ya wazee na viongozi wa dini katika ukumbi wa Turbo uliopo  Njombe mjini.

"Wazazi wangu tumepoteza watoto hatuelewi ni nani alikuwa Rais katika hao,hatuelewi nani alikuwa mchungaji katika hao, na hatuelewi na alikuwa mkombozi sahihi wa Njombe inayokuja katika miaka hamsini ijayo,wamepotezwa na watu waliokosa upendo kwa uchungu huu tulioupata wazee tusaidieni,tuonyesheni njia wapi tumekosea vijana wenzangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hakuna kufanikiwa bila kufanya kazi"

"Dawa ni ninyi wazee waambieni vijana nini mmefanya mpaka mmefika hapa ninawaombeni sana,haya yanatokea watanzania tuungane na tushikamane kwa kuwa wamoja lakini kwa bahati mbaya zaidi wapo watanzania wenzetu hata matukio kama haya hawayaoni wanafanya siasa za nje ya nchi,wanachafua Taifa letu huko nje ya nchi 

"Tuna uzalendo wa namna gani kama hujampenda jirani yako wa Njombe unazungumza maswala ya nchi yako huko nje,wako watu wanachafua taswila ya taifa letu ni katika vyama hivi hivi tunavyoviita ni vyama vya upingaji na sio vya upinzani unaenda sehemu mbali mbali unasema mimi sijaonwa 

"Rais ametuma wawakilishi kwenda kumuona,makamu Rais amekwenda kuona lakini unaenda nchi za watu unasema mimi sijaonwa hizi ndio roho za chuki zinazofaa kukemewa kwa namna yeyote ili kuwe na ukweli katika vizazi vijavyo na vya sasa"alisema katibu wa vijana

Aidha katibu huyo amewaonya wanaolenga kufanya tena matukio hayo kwa kuwa serikali ipo macho na ulinzi upo mkoani Njombe na atakayethubutu kufanya hivyo atakutana na mkono wa sheria,hivyo amewaomba wazee kuendelea kutoa ushauri kwa vijana.

Kwa upande wake Frank Awasi katibu wa uchumi na fedha wa CCM Taifa na mlezi wa mkoa wa Njombe  ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo alisema kuwa wameamua kuongea na wazee pamoja na viongozi wa dini kwa kuwa hao ndio wana nafasi kubwa kuhakikisha mji wa Njombe unakuwa na usalama ili kufanya kazi kwa uhuru.

Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Njombe Isaya Japhet Mengele Amekiri Kuwa Serikali Imesikiliza Kilio Cha Wananjombe Kwa Kufanyia  Kazi Vitendo Vya Utekaji na Mauaji ya Watoto Yaliyoshika Kasi mkoani humo,na kuiomba serikali uponyaji kwa watu ambao waliguswa na vyombo vya usalama wakati wa kupata taarifa.

"Tuombe tena baada ya hapo kuwepo na uponyaji wa namna fulani kwa wale ambao kwa namna moja au nyingine vyombo vyetu vya usalama pengine viliwagusa watu fulani kutaka wasaidie kutoa taarifa, ili wasielewe vibaya na kuanza kutoa taarifa tofauti katika jamii yetu kwa kuwa tumejiridhisha kwamba wako salama hawahusiki hivyo ni vizuri kidogo wakapata uponyaji wa nafsi zao"alisema Mengele

Viongozi mbali mbali wa chama hicho Taifa wamefika mkoani Njombe pamoja na kutoa rambi rambi kwa baadhi ya famili zilizopatwa na matatizo hayo ambapo mpaka sasa jumla ya watuhumiwa 30 ambao kesi zao zimekamilika dhidi ya mauaji ya watoto waliofikia 8 mpaka sasa wanategemea kufikishwa mahakamani.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )