Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 2, 2019

Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu Akasirika Spidi Ujenzi Jengo Jipya La Wizara Ya Mambo Ya Ndani Katika Mji Wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma

adv1
Na Felix Mwagara, MOHA.
KATIBU Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, amemtaka Mkandarasi anaejenga Jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma, afanye kazi usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari awe amemkabidhi jengo hilo.

Meja Jenerali Kingu amesema kasi ya ujenzi huo umenza kusuasua kwasababu Wizara yake ilifikia hatua kubwa lakini sasa imepitwa na baadhi ya Wizara kutokana na Mkandarasi anayejenga jengo hilo kupunguza kasi ikiwa ni tofauti na ile walioanza nayo awali.

Katibu Mkuu aliyazungumza hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika eneo hilo la ujenzi, jijini humo, leo, na alifanya ukaguzi na baadaye alizungumza na wadau kutoka pande tatu zinazoshirikiana katika kufanikisha ujenzi huo ambao ulianza mwezi Desemba mwaka jana.

Wadau wa pande tatu wanaofanikisha ujenzi huo ni Mmiliki wa Jengo hilo ambaye ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mshauri Mwelekezi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) pamoja na Mkandarasi ambaye ni Jeshi la Magereza.

“Nimepokea taarifa ya ujenzi unaoendelea, lakini sijaridhishwa nayo kutokana na asilimia ya ujenzi huu ulipofikia mpaka sasa, mmenipa ratiba mpya ya kukamilika kwa jengo hili, kasi yenu imekua ndogo mpaka tumeanza kupitwa na baadhi ya Wizara ambazo sisi tulikua tunaongoza, sasa nataka mfanye kazi hii usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari ujenzi huu uwe umekamilika na mnikabidhi jengo hili,” alisema Meja Jenerali Kingu.

Kwa upande wake Mshauri Mwelekezi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka TBA, Arch. Hassan Mnandala alimwambia Katibu Mkuu huyo kuwa, ataendelea kusimamia na kushauri ili Mkandarasi awe amemaliza kazi hiyo kwa wakati kama ratiba ilivyopangwa.

Naye Mkandarasi wa ujenzi huo, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Aron Lunyungu, kwa upande wake amesema ujenzi huo unaendelea na tayari ujenzi wa kuta umefanyika, na imefikia usawa wa kupaua na tayari upigaji wa ripu ndani ya jengo hilo umefanyika.

“Tunamshukuru Katibu Mkuu Meja Jenerali Kingu, leo katutembelea na ametuagiza tujipange ili tuweze kukamilisha kwa wakati ujenzi wa jengo hili, nasi tumejipanga kazi tutaifanya usiku na mchana kuhakikisha jengo hili tunalikamilisha na tunalikabidhi kwa wakati,” alisema ACP Lunyungu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )