Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 13, 2019

Kero Ya Mpaka Kati Ya Kenya Na Tanzania Kupatiwa Ufumbuzi

adv1
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.  Dkt. Damas Ndumbaro akiwa Kenya na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa Tanzania wakiwa wameshikana mikono kudhihirisha changamoto ya Mpaka huo uliopo Jasini Mkinga Mkoani Tanga.
 *****
Na. Peter Haule WFM, Tanga
Serikali imeahidi kutatua mgogoro wa Mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika Kijiji cha Mahandakini, Wilayani Mkinga mkoani Tanga, baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wanakijiji wanaoishi katika mwambao huo wa Bahari ya Hindi baada ya kuzuiwa kufanya shughuli zao za uvuvi na kuwasababishia hali ngumu ya maisha.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro walipotembelea na kukagua eneo hilo la mpaka na nchi Jirani ya Kenya.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mahandakini,  Bw. Nasoro Mbarook, alisema kuwa wavuvi wa Kijiji hicho wanashindwa kuendelea na shughuli za uvuvi baada ya vifaa vyao vya uvuvi  kukamatwa na wavuvi takribani 112 kukamatwa na vikosi vya ulinzi vya Serikali ya Kenya nakufunguliwa mashtaka kisha kutozwa faini ya Sh. 5000 ya Kenya, jambo ambalo wavuvi hao wanaamini halikua sahihi kwa kuwa walikua wanavua katika maji ya Tanzania katika Bahari ya Hindi hivyo hawakutenda kosa kama ilivyodaiwa.

Manaibu Waziri hao, walisema dhumuni la ziara yao katika mpaka huo ni kujionea hali halisi na pia kuweka mikakati ya namna ya  kutatua changamoto zilizopo ikiwemo ya wananchi kushindwa kulipa kodi kutokana na kukosa kipato kilichotokana na uvuvi ambapo kwa sasa wanazuiwa kufanya shughuli za uvuvi.

Walisema kuwa wamejionea hali halisi ya mpaka huo hivyo Serikali itafanya tathmini kisha kufanya majadiliano na wenzao wa Kenya ili kulitafutia ufumbuzi suala hilo.

Aidha walibaini kuwa eneo la mpaka halijazingatia taratibu  kwa kuwa zipo nyumba ambazo zimejengwa chini ya umbali wa mita 30  mahali ambapo palipaswa kutokuwepo makazi hayo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Bw. Yona Mark, ameiomba Serikali kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Shule ya Msingi katika Kijiji cha Mandakini Wilayani humo ili wanafunzi waanze kusoma kwa kuwa kwa sasa watoto wanasoma katika shule iliyopo eneo la Kenya.

Pia ameomba  kujengwa kwa barabara katika eneo hilo la Kijiji ambalo linawakazi zaidi ya 3666 na Kituo cha kukusanya mapato kwa kuwa eneo hilo kuna bidhaa nyingi zinazoingia na kutoka nchini.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )