Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 4, 2019

Kesi ya Malinzi na Wenzake Yapata Hakimu Mpya

adv1
Kesi inayomkabili, aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake wa wanne imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na Hakimu aliyepangiwa kesi hiyo kuomba muda wa kupitia ushahidi uliotolewa.

Kesi hiyo awali ilikuwa mbele ya Hakimu Wilbard Mashauri ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu hivyo kesi hiyo kupangiwa Hakimu Mkazi Maira Kasonde.

Wakili kutoka Taasisi ya kuzuia kupambana na rushwa (Takukuru) Leonard Swai alidai kuwa kesi hiyo imekuja kwaajili ya uamuzi lakini kwakuwa imepangwa kwa Hakimu mwingine washtakiwa wanahaki yakuomba iendelea au ianze upya.

"Shauri lilikuwa mbele ya Mheshimiwa Mashauri na sasa limehamishiwa kwako hivyo washtakiwa wanaweza kusema tuendelee au shauri lianze upya," alidai Wakili Swai.

Hakimu Kasonde alieleza kuwa kesi hiyo imepangwa kwake asubuhi kwa kuwa ilikuwa kwa Hakimu mwingine hivyo anahitaji nafasi nzuri kwaajili ya kupitia ushahidi na vielelezo ambavyo vimeshatolewa.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Kasonde aliahirisha kesi hiyo hadi February 19, mwaka huu, tayari mashahidi 11 wa upande wa Mashtaka wameshatoa ushahidi katika kesi hiyo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )