Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 14, 2019

Kiwanda Cha Global Packaging Chapunguza Changamoto Ya Uagizaji Vifungashio

Na Lilian Lundo – MAELEZO
Kiwanda cha Global Packaging (T) Limited kilichopo Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mkoa wa Pwani kimepunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa vifungashio nje ya nchi.

Hayo yameelezwa mapema wiki hii na Meneja Mradi wa kiwanda hicho, Hatibu Njuwila wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.

“Kiwanda kilianza uzalishaji Januari, 2017 na  kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli , kinazalisha tani 150 za mifuko au vifungashio kwa mwezi,” amesema Njuwila.

Ameendelea kusema, wateja wakubwa wa kiwanda hicho ni wakulima wanaozalisha bidhaa za nafaka kama vile mahindi, mtama na mchele, bidhaa zinazotokana na madini na mazao mengine yanayohitaji vifungashio.

Amesema, lengo la uanzishwaji wa kiwanda hicho ni kupunguza uagizaji wa vifungashio nje ya nchi kutokana na kuwepo na uigizaji mkubwa wa vifungashio kutoka nje ya nchi kwa gharama kubwa.

Aidha amesema, mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka miwili tangu kuanza kwa uzalishaji wa kiwanda hicho ni pamoja na kuajili wafanyakazi 98 ambao wote ni Watanzania,  ambapo kwa asilimia kubwa ni kutoka Halmashauri ya Kibaha.

Mafanikio mengine ni kupunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa vifungashio kutoka nje ya nchi, kulipa kodi mbalimbali za Serikali Kuu pamoja na Halmashauri ambapo imeongezea Serikali mapato.

Matarajio ya kiwanda hicho ni kuzalisha vifungashio vyenye ubora na ambavyo vinakidhi mahitaji ya wateja ambayo itaongeza thamani ya mazao na uhifadhi na kupata masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi.

Global Packaging (T) Limited imejipanga vyema kutekeleza sera ya Serikali ya viwanda kwanza kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )