Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 14, 2019

Lugola ahoji dereva wa Tundu Lissu kutopigwa risasi

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema kuna haja ya dereva ya Mbunge wa Singida Mashariki, Adam Bakari kueleza kwanini alipohisi kuwa wanafuatiliwa na watu wa siojulikana siku ya kushambuliwa kwa Lissu hawakuchukua hatua ya kulipeleka gari kituo cha polisi.

Kangi Lugoa ametoa kauli hiyo jana Jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema maelezo ya dereva huyo yanatia shaka, wanataka awaeleze mambo kadhaa yatakayosaidia uchunguzi wa tukio hilo.

"Kwa hali ya kawaida ni jambo la kushangaza risasi zote hizo wanasema 38, hata moja haikumpata dereva huyu,” alisema Lugola.

Waziri huyo pia amehoji risasi hizo kutoharibu kisanduku kilichopo katikati ya gari hilo sehemu ya mbele, kinachotenganisha dereva na abiria.

Kuhusu eneo hilo kuondolewa kamera za CCTV, Lugola amesema nyumba za Serikali jijini Dodoma hazina kamera hizo.

“Huu ni upotoshwaji mkubwa ambao unalenga kuwadanganya wananchi na kuwataka waichukie Serikali yao na Rais John Magufuli na mimi kama waziri wa mambo ya ndani sitokubali,” alisema.

Alibainisha kuwa eneo alilokuwa akiishi mbunge huyo linalindwa na askari wa kampuni binafsi za ulinzi, si polisi na kubainisha kuwa kutokana na utata huo ndio maana wanamtaka mbunge huyo na dereva wake kutoa maelezo kukamilisha upelelezi.

“Wao ndio walikuwepo watuambie hawa waliompiga risasi ni wanawake au wanaume, ni wanene au wembamba, warefu au wafupi,” alisema.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )