Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 13, 2019

Maafisa Manunuzi na Wakaguzi wa ndani kutoka halmashauri 118 wapigwa msasa

adv1
Na Mathew Kwembe, Morogoro
Jumla ya watumishi 280 ambao ni Maafisa Manunuzi na Wakaguzi wa Ndani kutoka Halmashauri 118 za Mikoa 16 nchini wanashiriki mafunzo ya siku nne ya marekebisho ya sheria ya ununuzi wa umma na mfumo wa utoaji taarifa za manunuzi (PMIS) yanayofanyika mkoani Morogoro kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao ili waweze kuutumia vizuri Mfumo wa utoaji wa taarifa za ununuzi pamoja na marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2016 pamoja na marekebisho ya kanuni zake.
 
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia Programu ya Maboresho ya Fedha za Umma Awamu ya V (PFRMP V)kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
 
Akifungua mafunzo hayo jana mjini Morogoro, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro bwana Clifford Tandari alisema kuwa baada ya serikali kuifanyia marekebisho kadhaa sheria ya manunuzi ya umma kulikuwa na umuhimu mkubwa kwa watendaji hao kujengewa uwezo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
 
Aliongeza kuwa Serikali iliona kulikuwa na haja ya kuifanyia marekebisho sheria hiyo ili iweze kuleta matokeo yaliyokusudiwa hasa kufanikisha lengo la upatikanaji wa thamani halisi ya fedha katika manunuzi kama ilivyokuwa imekusudiwa.
 
Kwa mujibu wa Katibu Tawala huyo, baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiikabili sekta ya Ununuzina kupelekea Sheria na Kanuni hizo kurekebishwa ni pamoja na bei ya manunuzi kuwa kubwa kulinganisha na bei ya soko, gharama za mchakato wa manunuzi kuwa juu kutokana na mpangilio mbaya wa ununuzi na pia kutozingatia sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA.
 
Bwana Tandari alizitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na mchakato wa ununuzi kuchukua muda mrefu jambo ambalo limekuwa likileta athari mbalimbali ikiwemo kupanda kwa bei ya huduma, vifaa au kandarasi kutokana na hali ya soko kubadilika.
 
Changamoto nyingine ni kutotumiwa kwa viwango hasa kwenye huduma na bidhaa kama vile utengenezaji wa magari, ununuzi wa bidhaa mtambuka hasa bidhaa zinazopatikana GPSA na MSD kwani lazima bidhaa hizo zitoke huko.
 
Bwana Tandari alieleza pia tofauti kati ya taratibu za ununuzi zinazotumiwa na Halmashauri na Taasisi nyingine za Umma hasa kutokana na kukosekana kwa taratibu za kisheria zinazowahakikishia wauzaji kuwa ununuzi unazingatia ushindani thabiti, haki, uwazi na uwajibikani, uadilifu na maslahi ya taifa.
 
Katibu Tawala wa Mkoa aliongeza kuwa kutokana na marekebisho ya sheria ya ununuzi serikali inatarajia kuongezeka kwa ushindani na uwazi katika ununuzi wa uma, kuongezeka kwa uwajibikaji na kupungua kwa gharama za ununuzi wa magari kwa kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini na kuboresha ukidhi na uzingatiaji wa sheria ya ununuzi ambapo sheria imetoa fursa kwa PPRA kuzikagua taasisi nunuzi na kupima kama zimezingatia ukidhi wa sheria katika ununuzi.
 
Bwana Tandari alisema kuwa sheria imetoa mwanya pia wa kutumia mfumo wa TEHAMA  ambapo taasisi nunuzi huwasilisha taarifa zake PPRA kwa kutumia mifumo iliyowekwa.
 
Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo hayo bwana Lucas Mrema alisema kuwa mikoa 16 inayoshiriki mafunzo haya ni  mbali na ile mikoa 10 iliyokuwa ilishiriki kwenye utekelezaji wa programu ya usimamizi wa fedha za Umma awamu ya nne.
 
” Katika utekelezaji wa programu ya Usimamizi wa Matumizi ya fedha za Umma awamu ya tano tunatarajia kuwa mikoa yote 26 na halmashauri zake 185 zitashirikishwa,” alisema.
 
Kwa upande wake Mhandisi Mary Swai Kaimu Mkurugenzi Msaidizi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) aliwataka Maafisa Manunuzi kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu zote za manunuzi pindi wanapotekeleza najukumu yao.
 
Aliongeza kuwa Maafisa Manunuzi wanapaswa kuhakikisha kuwa makini katika utekelezaji wa mikataba mbalimbali ambapo alidai kuwa pindi mkataba unaposainiwa wahakikishe kuwa mkataba huo unatekelezwa vizuri.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )