Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 18, 2019

Maalimu Seif Aomba CAG akawakague lipumba na wenzake

adv1
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif, Amemuomba CAG kwenda kufanya  ukaguzi maalum kwa fedha za ruzuku zilizotolewa na msajili wa vyama vya siasa kwa lipumba na wenzake kwa kipindi chote ambacho walipata uhalali kutoka RITA.

Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo Jumatatu  muda mfupi  baada ya Mahakama Kuu kutengua uteuzi wa wajumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Wananchi (CUF) .

Amesema baada ya uamuzi huo wa mahakama ni vyema CAG, akafanya ukaguzi kwa kuwa bodi hiyo iliyokuwa kambi ya mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba haikuwa halali.

"Tumeupokea kwa furaha uamuzi huu wa Mahakama Kuu, umekata mzizi wa fitina wa madai yetu dhidi ya Rita. Nilishasema toka awali tutapokea uamuzi wowote wa mahakama utakaotolewa.

"Nawaomba wanachama  wa CUF wawe watulivu kwa sasa wakati tukisubiri uamuzi  mwingine utakaotolewa hapo Ijumaa," amesema Maalim Seif.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )