Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 14, 2019

Mabula Ashangazwa Halmshauri Misungwi Kutojipanga Fursa Ya Bandari Kavu Na Treni Ya Mwendokasi

Na Munir Shemweta, MISUNGWI
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameishangaa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kushindwa kutumia fursa ya ujio wa treni ya mwendokasi (SGR) na Bandari kavu katika wilaya hiyo kwa kupanga na kupima viwanja kwa ajili ya shughuli mbalimbali ili kunufaika na fursa katika wilaya hiyo.

Dkt Mabula alishangazwa na hali wakati akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi baada ya kubaini halmashauri hiyo kutokuwa na jitihada zozote za kujiandaa na fursa zilizojitokeza katika halmashuri hiyo,

‘’Maeneo ya Usagara itakapojengwa Bndari Kavu, ujio wa treni ya Mwendokasi na  Fela katika eneo la Kituo cha Mabasi ni maeneo ya kimkakati hivyo ni lazima maeneo yanayozunguka yapangwe na kupima  viwanja kwa nia ya kuwa na eneo lililopangika na wakati huo kupanua wigo wa mapato’’ alisema Dkt Mabula.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, tayari wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza imejaa lakini anashangazwa na wilaya ya Misungwi kushindwa kuchangamkia fursa ya kupima viwanja kwa kuwa mahitaji ya viwanja yameongezeka ili wananchi wapate fursa za kupata viwanja.

Alisema maeneo hayo yamekaa kimkakati na halmashauri ikitumia vizuri fursa hiyo kwa kupanga na kupima viwanja itaubadili mji na hivyo kuepukana na ujenzi holela na kusisitiza kuwa ni lazima halmashauri ya Misungwi ipime na kugawa viwanja vya biashara na viwanda na kubainisha kuwa Bandari Kavu katika eneo hilo haikuja kimakosa na kuitaka wilaya kubadilika.

Dkt Mabula alifafanua kuwa, upimaji viwanja katika maeneo hayo mbali na kuwawezesha wananchi kiuchumi lakini pia kutaisadia halmashauri kukusanya mapato mengi yatokanayo na ardhi na kusisistiza kwa kusema ardhi ni mtaji.

Mapema Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili katika halmashauri ya Misungwi Fredrick Nyoka alisema halmashauri yake imejiweka mikakati mbalimbali ya kukusanya mapato ya kodi ya ardhi na mojawapo ni kuhakikisha inatoa ilani za madaia kwa wadaiwa sugu ambapo tayari imetoa ilani 223. Alisema mbali na kutoa ilani halmashauri hiyo pia imepima jumla ya viwanja 250 na kutoa hati 174 ambapo Naibu waziri Mabula alishangazwa na kasi ndogo ya upimaji na utoaji hati kwa kueleza kuwa kwa kasi hiyo halmashauri hiyo haiwema kuongoza kwa ukusanyaji mapato.

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisikitishwa na halmashauri ya Misungwi kutoijali idara ya ardhi hasa baada ya kuelezwa na Afisa Ardhi Mteule Frorida Busheni kuwa pamoja na jitihada zake za kuomba fedha kwa ajili ya kushughulikia suala la upimaji lakini alishindwa kuzipata jambo lililomfanya kuomba msaada ofisi ya Ardhi Kanda ya Ziwa.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameziitaka halmashauri za wilaya ya Kwimba na Misungwi mkoani Mwanza kufanya ukaguzi katika maeneo yote yenye viwanja na mashamba yasiyoendelezwa kwa muda mrefu na kubainisha kuwa watakaobainika kutoyaendeleza wanyanganywe.

Dkt Mabula alisema baadhi ya wananchi wamekuwa na viwanja lakini viwanja hivyo haviendelezwi kwa muda mrefu na vingine vipo kwa zaidi ya miaka kumi na kubakli vichaka vya kufanyia uhuni ambapo aliagiza watakaobainika kutoendeleza wapatiwa notisi kama sheria inavyoelekeza na wasipotii hatua za kuwanyanganya zifanyike.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )