Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 25, 2019

Makamu Wa Rais Aipongeza Halmashauri Ya Wilaya Ya Kaliua Kwa Kuwainua Wanawake

adv1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa kuwa mstari wa mbele katika suala zima la kuwainua Wanawake, Vijana na Walemavu ambapo zaidi ya milioni 450 zimetolewa katika makundi hayo ndani ya kipindi cha 2017 – 2018.

 Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo jana wakati akihutubia wananchi kwenye uwanja wa Kolimba, Kaliua moani Tabora.

 Aidha katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameridhia kuondolewa mara moja kwa Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Kaliua Mhandisi Fikiri Samadi baada ya kushindwa kutekeleza mradi wa maji wa shilingi bilioni 1.5.

 “Ziara hizi ni ziara za kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo na serikali imekuwa mstari wa mbele kuweka pesa nyingi kwenye miradi ya maendeleo hivyo yeyote atakayekwamisha atachukuliwa hatua mara moja”alisema Makamu wa Rais.

 Makamu wa Rais amesema wilaya ya Kaliua ni mfano wa kuigwa kwa kujenga jingo la upasuaji pamoja na wodi ya wazazi yenye uwezo wa kuchukua vitanda 24 katika kituo cha afya Kaliua kwa mapato yao ya ndani pamoja na michango kutoka chama cha msingi Nsungwa ambapo mpaka kukamilika wametumia shilingi 159,703,199.98.

 Kwa upande mwingine Naibu Waziri TAMISEMI alisema vikundi vinavyopewa mikopo na Halmashauri lazima virejeshe mikopo hiyo ili iweze kuwasaidia watu wengine akizungumzia kwa wilaya ya Kaliua peke yake ambapo zaidi ya milioni 450 zimetolewa mpaka sasa zimerudishwa milioni 89 tu.

 Akizungumzia suala la uchaguzi katika kata 3 za Igombe Mkuluu, Mirambo na Kanindo zilizopo katika jimbo la Ulyankulu, Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Waitara alisema lazima usalama wa Taifa uzingatiwe na upewe kipaumbeke kwani kwenye maeneo hayo kuna waliopewa uraia na kuna wakimbizi hivyo Serikali itakapojiridhisha wanaweza shiriki katika uchaguzi ujao.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )